Canibalism Kwa Kuku Au Tatizo La Kudonoana
Inafahamika kuku kutaga mayai mengi hutokana na aina ya mbegu ya kuku, ila jua kwamba hata aina ya mbegu ya kuku yenye sifa ya kutaga mayai mengi kama haitapewa matunzo mazuri basi sifa yake ya utagaji itapotea.
Wigo wa mimea ni kinga nzuri ya mazao shambani. Mimea ya wigo inaweza kutumika kama kizuizi cha wadudu kuhama hama.
Wigo hutatiza vidukari kuhama na kuingia bustanini. Kwa mfano, mimea kama tithonia ni kizuizi kwa aina nyingi sana za wadudu.
Kutifua udongo ni jambo la muhimu sana ili kuufanya udongo kuwa bora.
Umuhimu wa kutifua udongo ni kama ifuatavyo
1. Hulainisha udongo ili kuruhusu mizizi ya mimea kupenya kwa urahisi.
2. Kutifua kunaboresha uwezekano wa kupenya kwa nitrogen na oxygen kutoka kwenye hewa.
Mashonanguo kwa kiingereza ni Blackjack au kwa kisayansi yanajulikana kama (Bidens
pilosa)
Mashona nguo yanazuia wadudukama vile Vidukari, Siafu, bungo, katapila, chenene (crickets), nyenyere, siafu na inzi weupe.
Pilipili hoho ni zao la jamii ya pilipili isiyo kali, tunda lake ni nene kiasi la duara pia linaweza kuwa lililochongoka. Pilipili hoho hutumika katika kutengeneza rangi za asili za vyakula ambazo kwa sasa hupendwa zaidi kuliko zile zinazotokana na kemikali na pia huongeza ladha na harufu katika vyakula.
Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa baada ya kufunga na kukomaa vizuri. Kwa kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka.
Vitungu saumu vina manufaa sana katika kukabiliana na aina mbalimbali za wadudu waharibifu na baadhi ya magonjwa kutokana na kuwa na harufu kali inayosaidia kuwafukuza wadudu kama vidukari, bungo na hata panya.
Huu ni ugonjwa hatari sana kwa maisha ya binadamu. Kinyesi cha punda kinabeba vimelea vijulikanavyo kama clostindium tetanii vinavyosababisha ugonjwa wa tetanasi.
Wadudu hawa wanaweza kuishi katika viumbe wote wenye damu moto maarufu kama mamalia na ndege, na wanapotoka ndani ya miili ya viumbe hao wadudu hao wanaweza kuishi kwenye udongo kwa miaka mingi