Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 1 Kikombe
Sukari ya kusaga - 3/4 Kikombe
Siagi - 125 gms
Yai - 1
Baking powder - 1/2 kijiko cha chai
Zabibu kavu - 1/2 kikombe
Cornflakes iliyovunjwa (crushed) - 2 Vikombe
Vanilla - 1 kijiko cha chai
MAANDALIZI
Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri. Tia baking powder, zabibu na unga na changanya vizuri. Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni. Tengeneza viduara vidogo vidogo. Weka cornflakes katika sahani ya chali (flat) na zungusha viduara humo kisha upange katika sinia ya oveni. Pika katika moto wa 350ºF kwa muda wa dakika 20-25 hadi vigeuke rangi na viwive.
Updated at: 2024-05-25 10:22:57 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kidali cha kuku 1 (chicken breast) Kitunguu maji 1/2 (onion) Kitunguu swaum/tangawizi (garlic and ginger paste) 1 kijiko cha chai Limao ( lemon)1/4 kijiko cha chai Curry powder 1/4 kijiko cha chai Pilipili ya unga kidogo (Chilli powder) Coriander powder 1/4 kijiko cha chai Soy sauce 1kijiko cha chai Mafuta 2 vijiko vya chai. Chumvi kiasi (salt) Vijiti vya mishkaki
Matayarisho
Osha kidali kisha kikaushe maji na kitchen towel na ukate vipande(cubes) vidogodogo na uweke pembeni. Baada ya hapo changanya vitu vyote (kasoro vijiti )na utie vimaji kidogo kisha visage katika breda kupata paste nzito. Baada ya hapo changanya hiyo paste na kuku na uache zimarinate kwa muda wa saa moja. Baada ya hapo zitunge kuku katika vijiti vya kuchomea na uzichome katika oven mpaka ziive (inaweza kuchukua kama dakika 10). Baada ya hapo chicken satay yako itakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viambaupishi Vya Masala
Nyama vipande - 3 LB
Mtindi - ½ kopo
Kitunguu (thomu/galic) - 1½ kijiko cha supu
Tangawizi - 1½ kijiko cha supu
Nyanya - 2
Pilipili mbichi - kiasi
Nyanya kopo - 4 vijiko vya supu
Vidonge supu - 2
Pilipili nyekundu paprika - kiasi
Bizari zote saga - 2 vijiko vya supu
Viazi - 4
Mafuta - 2 mug
Samli - ½ kikombe
Vitungu - 6
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika masala
Kwenye sufuria tia nyama, saga nyanya na thomu, pilipili mbichi, tangawizi. Mimina kwenye nyama na mtindi, tia na nyanya kopo, bizari paprika, vidonge vya supu, chumvi kisha changanya vyote pamoja weka motoni. Katika sufuria nyengine tia mafuta na samli kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi toa weka pembeni. Kanga viazi weka pembeni. Chukua mafuta kidogo uliyokangia tia kwenye nyama acha katika moto wa kiasi mpaka nyama iwive na maji ya punguke. Tia viazi na vitunguu vivunje vunje tia ndani ya nyama acha moto mdogo.
Vipimo Vya Wali
Mchele - 5 mug
Maji - kiasi
Chumvi - kiasi
Mafuta uliyokaanga vitungu - kiasi
Rangi ya biriani - ¼ kijiko cha chai
*Zafarani - ½ kijiko cha chai
*roweka rangi na zafarani
Namna Ya Kutarisha Na Kupika Wali
Osha mchele roweka muda wa saa. Chemsha maji kama magi 10 hivi na chumvi tia mchele. Uache uchemke ukishaiva kiini nusu, mwaga maji chuja. Mimina juu ya nyama tia rangi na mafuta kwa juu funika. Aacha kidogo katika oveni kwa muda wa dakika 20 hivi kisha epua ikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kabichi 1/2 kilo Nyanya ya kopo 1/2 Kitunguu 1 Curry powder 1/2 kijiko cha chai Chumvi Olive oil
Matayarisho
Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga ngano vikombc 3 Unga mbegu za mchicha kikombe 1 Baking powder vijiko vidogo Maziwa kikombe 1 Sukari kikombe 1 Blue band kikombe ½ Mayai 10-12
Hatua
• Chagua, osha, kausha mbegu za mchicha mweupe, kisha saga zilainike. • Chekecha unga wa ngano, unga wa mbegu za mchicha na baking powder Kwenye bakuli kubwa. • Ongeza sukari na changanya. • Ongeza mayai kidogo, kidogo ukikoroga na mwiko kwenda njia moja mpaka ilainike. • Kama rojo ni zito ongeza mayai, au maziwa ili iwe laini, ongeza vanilla na koroga. • Paka mafuta kwenye chombo cha kuoka au sufuria na chekechea unga kidogo. • Mimina rojo ya keki na oka kwenye oveni au kama ni sufuria funika, weka moto mwingi juu, chini weka moto kidogo. • Ukinusia harufu nzuri ya vanilla, funua, choma kisu katikati ya keki, kama ni kavu epua, pozesha na pakua kama kitafunio.
Updated at: 2024-05-25 10:23:00 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour) kikombe 1na 1/2 Sukari (sugar) 1/4 kikombe Barking powder 1/2 kijiko cha chai Magadi soda (bicarbonate soda) 1 kijiko cha chai Mafuta 2 vijiko vya chai Mafuta ya kukaangia Maji ya uvuguvugu kiasi
Matayarisho
Changanya unga na vitu vyote (kasoro mafuta ya kuchomea) kisha ukande (hakikisha unakuwa mgumu) Baada ya hapo sukuma na ukate shape uipendayo (hakikisha unakata vipande vinene kiasi na sio kama mandazi) Baada ya hapo ziweke sehemu yenye joto na uache ziumuke. Zikisha umuka zikaange katika moto mdogo ili ziive mpaka ndani. Zikisha iva zitoe na uziweke katika kitchen towel ili zichuje mafuta. Ziache zipoe na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:27 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kupata takriban gilasi 6
Mabungo - 3
Maji - 6 au 7 Gilasi
Sukari - kiasi upendacho
Chumvi - kidogo sana
Namna Ya Kutayarisha:
Kata mabungo na toa nyama yake tia katika mashine ya kusagia. Tia maji, sukari na chumvi usage kidogo tu. Chuja kisha mimina katika jagi uweke katika friji. Mimina katika gilasi.
Updated at: 2024-05-25 10:23:02 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (plain flour) 1/4 Kitunguu kikubwa (chopped/slice onion) 1 Yai (egg) 1 Chumvi (salt) Mafuta (cooking oil)
Matayarisho
Tia unga, chumvi na maji kiasi katika bakuli kisha koroga mpaka madonge yote yaondoke. Baada ya hapo tia yai na vitunguu kisha koroga tena mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. baada ya hapo choma chapati zako kama kawaida (jinsi ya kuchoma unaweza kuangalia kwenye recipe yangu ya chapati za maji katika older posts) na baada ya hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.