Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:37:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mshale 10 Utumbo wa ng'ombe 1/2 kilo Nazi ya kopo 1 Nyanya 1 Kitunguu kikubwa 1 Tangawizi/ swaum 1 kijiko cha chakula Olive oil kiasi Limao 1 Chumvi Curry powder 1 kijiko cha chai Turmaric 1/2 kijiko cha chai Coriander ya powder 1/2 kijiko cha chai Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai Pilipili kali nzima (usiipasue)
Matayarisho
Safisha utumbo kisha uweke ktk pressure cooker pamoja na chumvi kiasi, limao, tangawizi, swaum na maji kiasi kisha uchemshe kwa muda wa nusu saa. Baada ya hapo menya ndizi kisha zikate vipande vidogo kiasi ili ziwahi kuiva, kisha ktk sufuria ya kupikia tia vitunguu na nyanya kisha ndizi kwa juu yake na supu ya utumbo kiasi chumvi kidogo na mafuta kiasi kisha bandika jikoni na uchemshe mpaka ndizi zikaribie kuiva. Zikisha karibia kuiva tia utumbo na spice zote, pilipili nzima na tui la nazi kisha changanya vizuri na uache vichemke mpaka ndizi na tui la nazi vitakapoiva na rojo ibaki kiasi. Baada ya hapo Ndizi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Piga piga mayai vizuri kwenye bakuli na weka chumvi kidogo kisha weka kikaango kwenye moto na mafuta kidogo.
Kikisha pata moto miminia mchanganyiko wa mayai na uanze kukorogo pale tu unapomiminia, endelea kukoroga hadi uone yanakuwa magumu na kuanza kuiva. Pika kwa kiwango unachopendelea na kusha epua na weka kwenye sahani.
Weka mafuta kijiko kimoja kwenye kikaango na kisha weka soseji zako na uzipike kiasi pande zote kisha epua na weka pembeni.
Weka slesi za mikate kwenye toster na zikiwa tayari unaweza weka siagi ili kuongeza ladha na mvuto. Andaa mlo wako pamoja na juice, maziwa au chai.
Updated at: 2024-05-25 10:34:45 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Soda ni kiburudisho ambacho si muhimu sana kwa afya.
Aina nyingi za soda zina kafeini ambayo huzuia usharabu (ufyonzwaji) wa madini ya chuma mwilini hasa yatokanayo na vyakula vya mimea Hata hivyo soda zinaweza kutumika kwa kiasi kidogo kama kiburudisho, ila tunapotaka ubora zaidi wa afya zetu inafaa kupunguza matumizi ya soda na badala yake kutumia vinywaji vyenye virutubishi muhimu kama vile maji ya matunda, maziwa, madafu au asusa kama vile matunda, karanga na aina mbalimbali za mboga mfano karoti.
Hii inasaidia pia kutumia fedha kidogo tuliyo nayo kwa vyakula muhimu, hasa ukizingatia badala ya soda moja unaweza kupata mayai matatu au nusu lita hadi lita moja ya maziwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Maziwa ya unga - 2 vikombe
Sukari - 3 vikombe
Maji - 3 vikombe
Unga wa ngano - ½ kikombe
Mafuta - ½ kikombe
Iliki - kiasi
MAPISHI
Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri Kisha mimina mafuta koroga Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza. Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Tende zilizotolewa kokwa - 1 Kilo
Cornflakes - 1 ½ kikombe
Lozi Zilokatwa katwa - 1 kikombe
Siagi - ¼ kilo
MANDALIZI
Mimina tende na siagi kwenye sufuria bandika motoni moto mdogo mdogo mpaka zilainike. Kwa muda wa dakika 10. Isonge kidogo kwa mwiko au kuikoroga ichanganyike vizuri. Changanya Cornflakes na lozi kwenye tende mpaka zichanganyika vizuri. Pakaza treya au sinia mafuta au siagi kidogo. Mimina mchanganyiko wa tende, zitandaze vizuri na ukate vipande saizi unayopenda. Zikiwa tayari kuliwa kwa kahawa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga wa ngano - 2 - 2 ¼ Vikombe
Siagi - 1 ½ Kikombe
Sukari - 1 Kikombe
Yai - 1
Vanilla -Tone moja
Baking Powder -kijiko 1 cha chai
Chumvi - Kiasi kidogo (pinch)
Unga wa Kastadi - 2 Vijiko vya supu
MATAYARISHO
Changanya vitu vyote isipokuwa unga. Tia unga kidogo kidogo mpaka mchanganyiko uwe sawa. Kisha fanya duara ndogo ndogo uzipange kwenye treya na utie rangi katikati. Halafu zichome katika moto wa 300°F kwa muda wa dakika 20 - 25 na zisiwe browni . Kisha panga kwenye sahani tayari kuliwa na chai.
Updated at: 2024-05-25 10:22:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai) Sukari (sugar 1/2 kijiko cha chakula) Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai) Hamira (yeast 1/2 kijiko cha chakula) Baking powder 1/2 kijiko cha chai Siagi (butter 1/4 ya kikombe cha chai) Maziwa (fresh milk 3/4 ya kikombe cha chai)(unaweza kutumia maji badala ya maziwa)
Matayarisho
Pasha maziwa yawe ya uvuguvugu kisha weka pembeni, pia yeyusha siagi na uweke pembeni.Baada ya hapo tia kila kitu kwenye bakuli la kukandia kasoro maziwa, na uchanganye vizuri kisha tia maziwa kidogo kidogo katika mchanganyiko huo kisha ukande. Ukimaliza uweke kwenye sehemu ya joto na uache uumuke. Ukisha umuka utawanyishe katika madonge saba Kisha .pakaza mafuta au siagi katika chombo cha kuokea kisha yapange hayo madonge katika hicho chombo na uyaache yaumuke tena (kwa mara ya pili). Baada ya hapo pakaza mafuta juu ya hayo madonge na uyaoke (bake) katika oven (moto 200°C ) kwa muda wa dakika 25 na hapo scones au maskonzi yatakuwa tayari
Mapishi ya Wali Wa Tambi Na Kuku Wa Sosi Ya Mtindi
Updated at: 2024-05-25 10:23:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo Vya Wali
Mchele - 3 vikombe
Tambi - 2 vikombe
Mafuta - ¼ kikombe
Chumvi
Vipimo Vya Kuku
Kuku kidari (boneless) aliyekatwa katwa vipande - 1 Kilo
Kitunguu maji kilichokatwa katwa - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Paprika - 1 kijiko cha supu
Masala ya kuku (tanduri au yoyote) - 1 kijiko cha supu
Ndimu - 2 vijiko vya supu
Mtindi (yoghurt) au malai (cream) - 1 kikombe
Mafuta - ¼ kikombe
Majani ya kotmiri (coriander) - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali:
Osha Mchele, uroweke. Tia mafuta katika sufuria, kaanga tambi zilizokatwakatwa hadi zigeuke rangi kuwa nyekundu. Tia mchele endelea kukaanga kidogo. Tia maji kiasi cha wali kupikika kama unavyopika pilau. Kiasi cha maji kinategemea aina ya mchele Funika katika moto mdogo mdogo hadi uive ukiwa tayari.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku
Katika bakuli, changanya vitu vyote isipokuwa mtindi na kitunguu. Tia mafuta katika karai, kisha tia kitunguu ukaange muda mdogo tu, usikiache kugeuka rangi. Tia kuku na masala yake, endelea kukaanga, kisha tia mtindi au malai ufunike apikike na kuiva vizuri. Nyunyuzia kotmiri iliyokatwakatwa ikiwa tayari kuliwa na wali wa tambi.
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele Kisamvu kilichotwangwa Samaki Mbaazi Nyanya chungu Vitunguu Nyanya ya kopo Tangawizi Kitunguu swaum Vegetable oil Curry powder Tui la nazi (kopo 2) Chumvi Pilipili Limao
Matayarisho
Safisha samaki kisha wamarineti na kitunguu swaum, tangawizi, pilipili, chumvi na limao kwa muda wa masaa 3.Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana na uwaweke pembeni kwa ajili ya kuungwa.Katakata vitunguu maji, saga tangawizi na kitunguu swaum. Baada ya hapo injika sufuria ya mchuzi jikoni na mafuta kiasi ya kupikia, mafuta yakisha pata moto, tia vitunguu maji na vikaange mpaka viwe vya rangi ya brown. kisha tia kitunguu swaum na tangawizi.kaanga kidogo kisha tia nyanya ya kopo moja na ufunike. acha mpaka nyanya ziive. Kisha tia chumvi na curry powder na uache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia samaki na nyanya chungu nakisha kamulia nusu ya limao. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi kopo moja na uache ichemke mpaka mchuzi uive.
Baada ya hapo chemsha kisamvu pamoja na mbaazi Kikisha iva, kaanga kitu na nyanya pembeni mpaka ziive kisha tia kisamvu. geuza mchanganyiko mpaka uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi na chumvi na aacha ichemke mpaka tui liive kisha ipua.malizia kwa kupika wali ambapo utachemsha maji kisha tia mafuta,chumvi na mchele na uupike mpaka uive kisha sevu na mboga ulizopika na mlo wako utakuwa tayari kwa kuliwa.