Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:23:03 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Viazi mbatata (potato 4 vya wastani) Nyama ya kusaga (mince beef 1 kikombe cha chai) Kitunguu (onion 1 cha wastani) Carrot 1 Hoho (green pepper 1/2) Kitunguu swaum (garlic) Tangawizi (ginger ) Binzari nyembamba (ground cumin 1/2 kijiko cha chai) Binzari manjano (turmeric 1/2 kijiko cha chai) Curry powder 1/2 kijiko cha chai Limao (lemon 1/2) Pilipili ya unga (chilli powder 1/2 kijiko cha chai) Giligilani (coriander kiasi) Chumvi (salt) Mafuta (vegetable oil) Unga wa ngano kiasi
Matayarisho
Katakata vitunguu na hoho katika vipande vidogo vidogo na kisha kwangua carrot na uweke pembeni. Chemsha viazi na chumvi kidogo vikiiva viponde na uviweke pembeni, Baada ya hapo tia nyama limao, chumvi, kitunguu swaum na tangawizi ichemshe mpaka iive na uhakikishe maji yote yamekauka. Kisha Tia binzari zote, pilipili, curry powder, giligilani, vitunguu, hoho na carrot. Pika mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 3 na kisha ipua. Baada ya hapo changanya na viazi kisha tengeneza maduara ya kiasi na uyaweke pembeni. Chukua unga wa ngano kiasi na uchanganye na maji kupata uji usiokuwa mzito au mwepesi sana. baada ya hapo chovya madonge katika huo uji na uyachome katika mafuta. Hakikisha zinaiva na kuwa rangi ya brown na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.Unaweza ukazisevu na chatney yoyote unayopendelea.
Jinsi ya kupika Mboga Za Majani Makavu (Aina Yoyote)
Updated at: 2024-05-25 10:37:57 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Mboga za majani makavu ¼ kg Mafuta vijiko vikubwa 3-4 Karanga zilizosagwa kikombe ½ Maziwa au tui la nazi kikombe 1 Kitunguu 1 Nyanya 2 Chumvi (kama kuna ulazima) Maji baridi
Hatua
• Loweka mboga za majani makavu na maji kwa dakika 10-15. • Osha , mboga na katakata nyanya na vitunguu. • Kangaa, pukusua na saga karanga zilainike. • Kanga kitunguu, weka nyanya, koroga zilainike. • Ongeza mboga zilizolowekwa na maji yake kwenye rojo, koroga na funikia mpaka maji yakaukie na ive. Punguza moto. • Koroga karanga zilizosagwa na maji, ongeza kwenye mboga ukikoroga kwa dakika 5. • Onja chumvi, pakua kama kitoweo. Uwezekano Weka nyanya kidogo. Tumia tui la nazi au krimu badala ya maziwa. Weka nyama au dagaa au Mayai badala ya Karanga.
Jinsi ya kutengeneza Bisikuti Za Kaukau Na Kahawa (Cocoa Coffee Biscuits)
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Maji baridi – kikombe 1
Biskuti za kawaida – paketi 2
Kaukau (cocoa) – vijiko 3 vya kulia
Kahawa ya unga – kijiko 1 cha kulia
Njugu mchanganyiko zilokatwakatwa – kikombe 1
Sukari – kiasi upendavyo
MAANDALIZI
Changanya maji na kaukau na kofi na sukari Katakata biskuti kisha tia paketi moja na nusu uchanganye vizuri. Kisha nusu ya biskuti zilobakia katakata vipande vikubwa na weka juu ya mchanganyiko, kisha changanya kidogo tu. Weka katika foil paper na zungusha (roll) Kisha fungua umwagie njugu au mkassaraat zilosagwa Kisha roll katika foil paper na uweke katika freezer mpaka igande Kisha kata kata slices na iko tayari
Updated at: 2024-05-25 10:37:55 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Mashonanguo mkono 1 Tui la nazi kikombe 1 Karanga zilizosagwa kikombe ½ Mafuta vijiko vikubwa 4 Kitunguu 1 Nyanya ndogo 2 Chumvi kiasi
Hatua
• Chambua mashona nguo mateke, osha na katakata. • Menya osha na katakata kitunguu. • Osha, menya na katakata nyanya. • Kaanga karanga, ondoa maganda na saga zilainike. • Kuna nazi na chuja tui. • Kanga kitunguu, weka nyanya na koroga mpaka zilainike. • Weka mashona nguo na chumvi kisha koroga sawa sawa, funikiakwa dakika 5 -10. • Changanya tui la nazi na karanga, ongeza kwenye hizo mboga ukikoroga kwa dakika 5, punguza moto ili ziive taratibu. • Onja chumvi na pakua kama kitoweo. Uwezekano Changanya mnavu, mgagani, mashonanguo kidogo ki¬dogo au mboga nyingme. Tumia maziwa au krimu badala ya tui la nazi. Weka nyama au dagaa au samaki au mayai badala ya - karanga.