Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Kwa nini watu hutaka kufanya mapenzi baada ya kutumia dawa za kulevya?
Updated at: 2024-05-25 16:22:35 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dawa za kulevya huathiri ubongo jinsi unavyofanya kazi. Hubadili hisia na husaidia kuondoa aibu na vizuizi vingine. Mtu hujisikia jasiri na mwenye nguvu na hivyo ni rahisi zaidi kwake kushawishika kufanya ngono kuliko asipozitumia dawa hizo.
Updated at: 2024-05-25 16:24:05 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Haki za binadamu ni haki zinazohusiana na mambo ya msingi na
asili ya uhuru na heshima ya ubinadamu ambapo watu wote wamepewa
haki ya kupata heshima kama
binadamu. Mara mtu azaliwapo
mume au mke hupata
haki hizi. Haki hizi
zinatambuliwa kimataifa
na zina usawa kwa watu
wote. Nchi mbalimbali
zimetia saini na kuidhinisha
haki hizi za kimataifa
na kufanya ni sehemu
ya sheria zao
pamoja na kuweka sera
zinazolinda haki hizi.
Haki za uzazi zina misingi yake katika haki za binadamu na pia
zinahusiana na haki za mtu mmojammoja.
Kupata habari juu ya ujinsia na mada zinazohusu afya
ya uzazi.
Mwanamke au mwanaume kuamua kwa uhuru na
kuwajibika, kama unataka kujamiaana lini na nani.
Uhuru wa maamuzi.
Kuamua kwa hiari na kuwajibika juu ya idadi na muda wa
kupishana katika kupata watoto.
Kupata huduma za afya ya uzazi kwa urahisi.
Haki za kufanya maamuzi kuhusu afya ya uzazi, kwa
uhuru, bila kunyanyaswa, kulazimishwa, bila kutumia
nguvu pamoja na maamuzi nani wa kufunga naye ndoa.
Kujilinda kutokana na mila zenye madhara kama vile
ukeketaji wa wanawake.
Haki hizi zimerekebishwa tangu mkutano uliofanyika Cairo mwaka
19941.
Updated at: 2024-05-25 16:24:25 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ndiyo hatari kuu ya matumizi ya dawa za kulevya ambayo unayazoea na kufikiri huwezi kufanya lolote bila ya kutumia.
Kwa upande wa sigara unaweza kuzoea hali yake ya kukutuliza na hali ya kutamani kila unapojisikia. Kwa wengi hamu hiyo hutokea baada ya kazi nzito, pamoja na pombe, au baada kula. Kwa hiyo, kama unataka kuacha uvutaji wa sigara inabidi ubadili tabia na kuepuka vishawishi na pia kupambana na nafsi na matamanio yako. Hii ni hatua kubwa inayohitaji msimamo mkali. Utakapoanza kupunguza matumizi ya sigara au kuacha kabisa utajisikia mpweke au mkiwa. Hali hii inaweza ikawa mbaya na kuumiza. Mara nyingi utajihisi kujawa na wasiwasi, utakosa usikivu, utajisikia kusinzia ingawa utakosa usingizi usiku, mapigo ya moyo hushuka na pia shinikizo. Hamu ya kula na uzito kuongezeka iwapo utendaji wako wa kazi hupungua. Ukishatawaliwa na sigara basi kuvuta kwako si tabia bali ni ugonjwa. Watu wengi wanaotegemea nikotini hawavuti kwa starehe inayoletwa na starehe ya uvutaji, bali kuepuka maumivu yanayosababishwa na kuacha sigara.
Njia za Kufanya Msichana Amevutiwa na Wewe kwa Muda Mrefu
Kuwa Mvuto Mrefu: Njia za Kumvutia Msichana
Updated at: 2024-05-25 16:21:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Habari wapendwa, leo tutazungumzia njia za kufanya msichana amevutiwa na wewe kwa muda mrefu. Kuna mambo mengi unayoweza kufanya, lakini hapa nitakupa vidokezo kadhaa. Kwanza, kabla hatujaanza, ni muhimu kufahamu kuwa hakuna njia rahisi ya kumvutia msichana. Hivyo, unahitaji kuwa na subira, uvumilivu na kujituma.
Kuwa Mwepesi wa Kujibu Ujumbe Wake
Kuwa mwepesi wa kujibu ujumbe wake ni muhimu sana. Kama unaona ujumbe wake, jibu haraka iwezekanavyo. Kuonesha kwamba unajali na unafuatilia ujumbe wake ni njia nzuri ya kuonesha kwamba wewe ni mtu wa kuaminika na mwenye nia njema.
Mjulishe Kuhusu Maisha Yako
Hakikisha kuwa unamjulisha kwa kina kuhusu maisha yako. Mjulishe kuhusu familia yako, masomo yako na kazi yako. Kwa njia hii, atajisikia kuwa karibu zaidi na wewe na atahisi kuwa una nia njema na yeye.
Mfanye Aone Uwezo Wako
Msichana anapenda kuona mtu anayeweza kufanya kitu kizuri na anayejiamini. Hivyo, hakikisha unamfanya aone uwezo wako. Kwa mfano, unaweza kuimba wimbo kwa ajili yake, kumwandalia chakula chake anachopenda, au kumvutia kwa kucheza muziki au kuonesha kipaji chako cha kuvuta picha.
Kuwa Romantiki
Kuwa romantiki ni sehemu muhimu ya kumvutia msichana. Kwa mfano, unaweza kumtumia ujumbe wa kimapenzi mara kwa mara, kumpa zawadi ya kimapenzi, au kupanga siku maalum ya kimapenzi kama vile kumwandalia chakula cha usiku, kukaa naye mbele ya moto au kutembea sehemu nzuri.
Kuwa Mtu wa Kuaminika
Kuwa mtu wa kuaminika ni muhimu sana katika mahusiano. Hakikisha kuwa unakuwa mtu wa kuaminika, unayesikiliza na unayeshauri. Kusikiliza kwa makini na kutoa ushauri wake wa kina kunaweza kumfanya msichana kuona kwamba unajali na unatafuta kumfanya awe mwenye furaha.
Kukutana na Familia na Marafiki
Kukutana na familia na marafiki wa msichana ni muhimu sana katika kujenga uhusiano mzuri. Kwa hiyo, tafuta nafasi ya kukutana na familia yake na marafiki zake. Kupata uhusiano mzuri na familia na marafiki wa msichana kunaweza kumfanya aone kwamba unamtambua na unajali zaidi juu ya mahusiano yenu.
Kwa hitimisho, hizi ni njia kadhaa ambazo unaweza kutumia kumvutia msichana kwa muda mrefu. Kumbuka, hakuna njia rahisi ya kumvutia msichana. Kuwa na subira, uvumilivu na kujituma ndiyo mambo muhimu zaidi. Kwa hiyo, fanya bidii na uwe na nia njema na msichana, na hakika utafanikiwa katika kumvutia kwa muda mrefu.
Je, mtu anawezaje kuacha kutumia dawa za kulevya na itamchukua muda gani kurudia hali yake ya kawaida?
Updated at: 2024-05-25 16:22:36 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kitu muhimu ni kwamba, kweli uwe umedhamiria kuacha. Hatua ya kwanza ni kujiuliza kwa nini unatumia dawa za kulevya. Pale utakapojua ni nini ulikuwa unahitaji katika dawa za kulevya ni rahisi kutimiza malengo hayo kwa njia za kiafya zaidi. Jaribu kupunguza taratibu kiasi na muda wa kutumia dawa za kulevya. Pia tumia vitamini na madini kuimarisha afya yako. Jitenge na watumiaji wengine wa dawa za kulevya na sehemu ulizokuwa ukienda kupata dawa za kulevya. Kama hutofanikiwa katika hatua ya kwanza usikate tamaa! Watu hushindwa kuacha katika jaribio la kwanza! Jaribu tena!
Kuacha dawa za kulevya ni sawasawa na kupata nafuu ya ugonjwa, ni rahisi zaidi kufanikiwa kama utapata ushirikiano zaidi kutoka kwa marafiki au wanafamilia. Unaweza vilevile kuomba ushauri kutoka kwa watoa nasaha au madaktari. Msaada wa kitabibu ni muhimu kwa wale waliozoea kutumia hiroini na pombe, kwani mara nyingi hupata madhara yatishiayo maisha pale wanapojaribu kuacha dawa za kulevya. Ni vigumu kusema utachukua muda gani kuacha kutumia dawa za kulevya, kwa sababu i natofautiana kati ya mtu na mtu.
Madhara yanayotokea kwa unyanyasaji wa jinsia kwa mtu
Updated at: 2024-05-25 16:24:00 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Unyanyasaji wa ujinsia una matatizo mabaya ya kimwili na yanayochukua muda mrefu kwa mwathiriwa kupona. Unyanyasaji wa jinsia mara nyingi humuumiza mwathiriwa, matendo ya ubakaji, majaribio ya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia kwa mtoto, na ukeketaji kwa wanawake yanamhusu moja kwa moja mwili wa mwathiriwa. Mwathiriwa anaweza kupata maumivu makali wakati wa kitendo, viungo vyake vya uzazi akiwa mwanamume au mwanamke kuna uwezekano ukapata majeraha wakati wa ubakaji. Zaidi ya hayo mbakaji anaweza kumuumiza mwathiriwa katika sehemu nyingie za mwili. Na jambo baya zaidi ukatili wa kijinsia wakati mwingine unaweza kusababisha ulemavu wa maisha na mara nyingine hata kifo cha mwathiriwa. Ubakaji unaweza kusababisha mimba, na uenezaji wa magonjwa hatari kama Virusi vya Ukimwi. Watoto wanadhuriwa zaidi na vitendo vya ukatili wa ujinsia katika miili yao kwa sababu ukubwa wa viungo vyao vya sehemu za siri ni vidogo kuliko vile vya watu wazima. Athari za kisaikolojia kwa mwathiriwa pia ni hatari sana. Uonevu wa ujinsia kwa mwathirika unaweza kusababisha kuchanganyikiwa na kupata kiwewe na hali ya hatari sana inayoweza kusababisha mtu akapata kichaa katika miezi ya kwanza. Baada ya uonevu wa ujinsia na hata baada ya miaka, mwathiriwa bado atakuwa na kumbukumbu ya maumivu aliyopata na hivyo kukumbuka katika akili yake. Waathiriwa wengi wa ubakaji wana matatizo ya kutokuwa na uhusiano mzuri wa kujamiiana, kwani kila mara atahusisha kujamiiana na alipobakwa. Ndiyo maana waathiriwa wa ubakaji wanahitaji msaada, uelewa na uvumilivu toka kwa wazazi wao, wenzi wao na marafiki.
Updated at: 2024-05-25 16:22:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwa ujumla dawa zote za kulevya zinaweza kuwa ni za hatari. Kati ya dawa zilizohalalishwa kisheria nikotini, ambayo i ipo kwenye sigara, ndiyo hasa ya hatari. Inawezekana kuwa umeshakuwa tegemezi kwa sigara. Hii i ii ina maana ubongo wako utaizoea nikotini na utahitaji nikotini zaidi na zaidi i i ili kuendelea kuwa na hali nzuri. Nikotini pia ni hatari zaidi kwa sababu vijana mara nyingi huanza kutumia sigara kabla ya kuanza kutumia dawa kali zaidi.
Miongoni mwa dawa zisizoruhusiwa kisheria nchini Tanzania, heroini ndiyo labda yenye kusababisha utegemezi. Vilevile inahusishwa na makosa mengi ya jinai. Utumiaji wa heroini ni hatari hasa katika maambukizi ya UKIMWI. Watu wanaposhirikiana katika kutumia sindano za kujidungia heroini wanajiweka katika hatari na uwezekano mkubwa sana wa kuambukizana virusi vya UKIMWI. Hili hutokea pia pale watumiaji wa heroini wanapojiuza mii li yao katika ngono i ili wapate dawa za kulevya au fedha za kununulia dawa hizo. Uvutaji bangi husaidia kuondoa aibu na vizuizi. Hii i ii inamaanisha kuwa wavuta bangi wanaweza wakasahau kufanya ngono salama na hivyo kuwa katika hatari zaidi ya kupata au kueneza UKIMWI. Matumizi mabaya ya dawa huweza kuwa hatari sana na pengine kusababisha kifo pale zitakapotumiwa kupita kipimo ama zitakapochanganywa na dawa nyngine au pombe.
Haki zinazokiukwa iwapo mvulana au msichana wamelazimishwa kuoa au kuolewa
Updated at: 2024-05-25 16:23:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nani na lini unaoa ni maamuzi yako binafsi wewe mwenyewe, hata kama rafiki na wazazi wanakushauri juu ya jambo hilo. Kumlazimisha mtoto kuoa au kuolewa ni kumchukulia mtu uhuru wa anavyopenda kuishi. Haki ya kuchagua kuoa, ama kuolewa au kuanzisha familia yako huwa imegeukwa. Haki hii ni sehemu ya makubaliano ya kimataifa na sehemu ya programu na hatua ya Umoja wa Mataifa tangu mkutano wa Cairo 1994. Sheria ya ndoa, Tanzania13 inasisitiza kwamba hakuna ndoa halali, isipokuwa ipate ridhaa na iwe ya uhuru na hiari kutoka pande zote za wanaokusudia kuoana. Ndoa yoyote ambapo pande zimehusika hazikubaliani ndoa hiyo si halali.
Wakati mtoto amelazimishwa kuingia katika maisha ya ndoa bado hayupo tayari na ndoa hiyo itakuwa inavunja haki za msichana kama haki ya elimu.14 Msichana ana haki kupata elimu, msichana ana haki kupata elimu. Haki ya kuoa inakamilika kwa msichana kuwa na umri sahihi, naye kuwafanya maamuzi/uchaguzi wake mwenyewe, kuanzisha familia. Kwa hiyo inaingilia kuvunja haki ya msingi ya mtoto ya kumtoa shule kabla ya kumaliza elimu ya msingi, ambayo ni shuruti kwa watoto wote, hapa Tanzania.
Vidonge vya kuzuia mimba vinasababisha vidonda vya tumbo?
Updated at: 2024-05-25 16:23:51 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wanawake wengine wanapata vidonda vya tumbo, lakini haya hayana uhusiano na vidonge vya kuzuia mimba. Vyanzo vya vidonda vya tumbo mara nyingi ni maambukizi yatokanayo na msongo wa mawazo, kula vyakula vyenye mafuta mengi na viungo vingi, au kuwa na historia ya ugonjwa huu katika familia. Baadhi ya dawa huathiri tumbo kama vile asprini na ndiyo maana sio kila mtu anashauriwa kuzitumia. Vidonge vya kuzuia mimba havisababishi vidonda vya tumbo.
Je, Virusi vya UKIMWI na UKIMWI vinaambukiza kwa kujamiiana kwa njia ya sehemu ya haja kubwa au mdomoni?
Updated at: 2024-05-25 16:22:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ndiyo, kuna hatari kubwa ya kuambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI wakati wa kujamii ana kwa njia ya sehemu ya haja kubwa au mdomoni. Ngozi ya ndani ya sehemu ya haja kubwa ni laini sana na uwezekano wa kupata michubuko wakati wa kujamii ana ni mkubwa, kwa sababu hakuna majimaji kama ukeni yanoyorahisisha uume kuingia. Kwahiyo virusi vya UKIMWI ni rahisi sana kuingia mwilini mwa mwanamke kupitia kwenye michubuko hii .. Pia ngono kwa njia ya mdomoni ( „kula koni, chumvi chumvi , kulamba ukeni) hatari sana kama mwanamke ana vidonda au michubuko mdomoni na mwanaume au vidonda au michubuko uumeni, wanaweza kuambukizana. Watu wote wanashauriwa kutumia kondomu i ili kuzuia maambukizi.