Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Je, wasichana wana viungo gani vya uzazi na kazi zake ni zipi?
Updated at: 2024-05-25 16:24:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viungo vya uzazi vya ndani vinaonekana katika michoro inayofuata:
Ukiangalia mchoro huu hapo juu, ambao unaonyesha via vya uzazi vya ndani, utaona uke, mfuko wa uzazi, kokwa za mayai na mirija ya kupitisha mayai. Uke ni mfereji ulio kati ya mfuko wa uzazi na sehemu ya nje ya via vya uzazi. Uke unatumiwa wakati wa kujamii ana, damu ya hedhi na mtoto hupita hapa. Urefu wa uke kwa wastani ni sentimita 7 hadi 8. Mfuko wa uzazi kwa kawaida huwa na ukubwa unaofikia embe ndogo. Yai moja lililorutubishwa hujishikilia kwenye kuta zake nazo huitunza mimba mpaka siku ya kuzaliwa mtoto. Wakati wa ujauzito mfuko wa uzazi hukua taratibu ukistahimili ukuaji wa mtoto. Kila upande wa mfuko wa uzazi i i ipo kokwa ya mayai, ambayo i ina ukubwa kama mbegu ya harage. Kila mwezi yai moja hukomaa kwa upande wa kulia au kwa upande wa kushoto na husafiri kwa kupitia katika mrija wa falopia. Kazi ya mirija ni kupitisha yai lililopevuka kila mwezi kutoka kwenye kokwa za mayai mpaka mfuko wa uzazi. Yai hutungishwa ndani ya mirija hii.
Ukiangalia mchoro huu unaoonyesha via vya uzazi vya nje, utaona midomo ya nje na midomo ya ndani, halafu kisimi, tundu la mkojo, sehemu ya haja kubwa na mlango wa uke. Midomo ya nje na ya ndani ni mii nuko ya ngozi na i iko hapo kuhifadhi sehemu za ndani za uke. Kisimi (au kinembe) ni sehemu ya juu kabisa ndani ya uke na ni sehemu ya uke ambayo humsaidia mwanamke awe na msisimko au asikie utamu wakati wa kujamii ana. Kama tulivyoona hapo juu, mlango wa uke ni tundu ambalo damu hutokea wakati wa hedhi. Pia ni sehemu unapoingia uume wakati wa kujamii ana na mtoto hutokea sehemu hii anapozaliwa. Tundu la mkojo ni juu ya mlango wa uke na ni tundu ambalo mkojo hutokea. Sehemu ya haja kubwa ni sehemu i inapopita haja kubwa (kinyesi).
Kama wewe ni msichana, unaweza kuamua kutumia kioo kujiangalia sehemu zako za via vya uzazi vya nje. Kwa njia hii unaweza kuyaelewa vizuri maumbile yako.
Updated at: 2024-05-25 16:22:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hakuna jibu la ujumla kwa swali hili, kwa sababu tiba ya ugumba inategemea chanzo maalum cha ugumba huo kwa mhusika. Kuna matatizo ya ugumba ambayo yanaweza kutibiwa, lakini mara nyingi ni vigumu au hata haiwezekani kumtibu mwanaume au mwanamke mgumba. Kwanza kabisa, lazima daktari atafute sababu za ugumba kwa kufanya uchunguzi wa kitaalamu kwa mwanamke na mwanaume. Baada ya uchunguzi daktari anaweza akawashauri kuhusu uwezekano wa kuwatibu. Mara nyingine tiba ni rahisi, lakini matatizo mengine ni mazito na ni vigumu au haiwezekani kuyatibu.
Kwa nini hairuhususiwi kuotesha au kuvuta bangi, iwapo kupanda na kuvuta tumbaku kunaruhusiwa?
Updated at: 2024-05-25 16:24:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Sheria ya Tanzania inaeleza dawa zilizo halali na zisizo halali. Tumbaku imekubalika na jamii kwa muda mrefu, na ni katika miaka kama hamsini iliyopita ndipo madhara yatakanayo na nikotini iliyomo kwenye tumbaku yalipoanza kukubalika. Hata hivyo, hadi sasa tumbaku ni halali, lakini ni bangi kwa upande mwingine si halali kisheria Tanzania. Kwa hivyo, kutokana na kwamba nikotini kwenye sigara ina madhara, basi serikali ilichukua hatua ya kuanza kuwatahadhadharisha wavutaji na kuwazuia vijana kuvuta sigara. Kuna sheria mpya Tanzania ambayo inawalazimisha watengenezaji wa bidhaa za tumbaku kuandika tahadhari ya afya kwenye bidhaa wanazotengeneza na kuuza. Kuanzia mwaka 2000 bidhaa za tumbaku zote zililazimika kuwa na onyo kwamba “Uvutuaji wa sigara ni hatari kwa afya yako.”
Ni hatua zipi zinazochukuliwa na Serikali kuhusu matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya?
Updated at: 2024-05-25 16:22:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Serikali i i inatambua kukua kwa tatizo la dawa za kulevya nchini, kwani dawa za kulevya nyingi zinazotumika zinapitishwa na kuingizwa kwa magendo nchini. Kutokana na hali hii serikali imepitisha sheria kuhusu tuhuma za dawa za kulevya yaani Sheria ya Kuzuia Matumizi ya Dawa za Kulevya ya mwaka 1995.
Sheria hii i ii inatoa maelekezo ya kumshughulikia mtuhumiwa wa dawa za kulevya na hutoa adhabu kali kwa waliopatikana na hatia. Katika kusaidia vita dhidi ya dawa za kulevya, Serikali ya Tanzania iliunda tume ya wataalamu mwaka 1996 iitwayo Tume ya Taifa ya Kuzuia na Kuratibu Dawa za Kulevya ili kuendeleza vita hivyo. Tume hii inawasaidia polisi, polisi wa mipakani na forodha ambao wanazuia uinizaji na usambazaji wa dawa za kulevya kupitia mipakani na kuharibu mashamba ya bangi na mirungi. Wakala hawa kwa sasa wanafanya kazi bega kwa bega na nchi jirani i i ili kuzuia uingizaji wa dawa za kulevya kupitia mipakani. Vilevile inaandaa wataalamu kwa kutumia ASIZE mbalimbali ambazo kazi zao ni kuelimisha jamii kuhusu athari na hatari ya dawa za kulevya na kuwasaidia waathirika. Tume hii ya wataalamu vilevile inafikiria kuhusu kampeni za kitaifa zinazolenga kuelimisha kuhusu athari za dawa za kulevya. Lakini kazi ya tume hii ni ngumu kutekelezwa kwani vita dhidi ya dawa za kulevya ni jukumu la kila mtu na sio serikali peke yake. Inahitaji msaada kutoka kwa kila mtu na jamii kwa ujumla.
Updated at: 2024-05-25 16:24:04 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Siyo haki kwa mtoa huduma wa afya kukataa kumtibu. Kama kijana, una haki sawa ya kutibiwa kama vile mtu yoyote. Iwapo mtoa huduma anakataa kukutibu wewe, jaribu kuzungumza naye kuhusu jambo hilo na umuulize sababu za kukataa kukutibu. Iwapo yeye anashikilia uamuzi wa kutokutibu basi amua ama unatafuta mhudumu mwingine au zungumza na mkubwa wake kuhusu tatizo lako. Ni jambo la maana kuzungumza na rafiki yako au mwone mtu unayemwamini akusaidie kutatua tatizo lako.
Vituo vingi vya Umma na vya binafsi vya huduma za afya vinajitahidi kutoa huduma rafiki kwa vijana. Tafuta kituo cha karibu au shirika linalotoa huduma za afya ya uzazi. Kumbuka, haki ya afya ambayo pia inabeba haki ya huduma ya afya ya uzazi, Kimataifa inatambuliwa kupitia ICESCR4 na pia imetiwa saini na kuridhiwa hapa Tanzania. Hivyo usisite kuulizia huduma kama hii.
Albino anaathirikaje na unyanyapaa na ubaguzi katika jamii?
Updated at: 2024-05-25 16:24:16 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu wengi huwaona Albino kama watu tofauti na watu wengine na kuwakwepa, wanaweza hata kubadili upande wa barabara ili wasikutane nao au kukaa karibu nao katika daladala. Wengi wanaamini katika uongo na uvumi unaosambazwa. Jamii inawatenga katika matukio mengi na kwa hiyo kuimarisha uvumi usiyo na usahihi uliopo kuhusu Albino. Hii inapelekea kunyanyapaliwa, kubagulliwa na kuwekwa pembeni. Mbaya zaidi, ni kuwa ubaguzi huu huchangia katika kushuka kujithamini kwa kijana Albino. Akisha kuwa hajithamini ni vigumu kukubalika au kupata kazi. Kwa hiyo, ubaguzi unaleta mzunguko wa madhara kwa Albino. Hitaji muhimu kwa binadamu ni kupendwa, kukubalika na kutunzwa. Kwani ualbino unatokea katika familia bila kutarajiwa. Kuwepo kwa ualbino katika familia kunaweza kuwa kichocheo cha kukubalika na kupendwa miongoni mwa ndugu, wazazi, mababu na mabibi. Changamoto kubwa iliyopo Tanzania ni kupambana na unyanyapaa na ubaguzi na kugombea haki sawa kwa ajili ya Albino.
Je, watu wana amini nini katika kutumia vifaa vya ngono/kufanya mapenzi?
Je, unajua nini watu wanaamini kuhusu matumizi ya vifaa vya ngono? Tumezungumza na watu na tunakuletea majibu kwa mtindo wa kusisimua!
Updated at: 2024-05-25 16:18:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Je, umewahi kujiuliza watu wana amini nini katika kutumia vifaa vya ngono/kufanya mapenzi? Kuna maoni tofauti tofauti kuhusu hili ambayo yanaathiri jinsi watu wanavyoona na kutumia vifaa hivyo.
Kwanza kabisa, kuna wale ambao wanaamini kwamba kutumia vifaa vya ngono ni jambo baya na kinyume na maadili. Hawa huona kufanya mapenzi kwa kutumia vifaa hivyo ni kujihusisha na mambo ya kitoto na yanaweza kusababisha madhara makubwa kwenye maisha yao ya baadaye.
Kwa upande mwingine, kuna wale ambao wanaamini kwamba kutumia vifaa vya ngono/kufanya mapenzi ni sehemu ya maisha ya kawaida ya mtu mzima. Hawa huona kwamba kutumia vifaa hivyo ni jambo la kawaida na halina tatizo lolote. Kwa kuwa kila mtu ni tofauti, tunapaswa kuwaheshimu watu hawa na maoni yao.
Watu wengine huamini kwamba kutumia vifaa vya ngono/kufanya mapenzi ni njia nzuri ya kuongeza ufahamu wao wa kujamiiana na kujifunza zaidi kuhusu miili yetu na jinsi inavyofanya kazi. Hawa huona kwamba kujaribu vitu vipya ni muhimu katika maisha ya ngono na inaweza kusababisha furaha ya kipekee.
Kuna pia wale ambao huamini kwamba kutumia vifaa vya ngono/kufanya mapenzi ni njia ya kuepuka magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa. Hawa huamini kwamba kutumia vifaa hivyo ni salama na njia nzuri ya kufurahia ngono bila kuhatarisha afya zao na wale wa karibu nao.
Watu wengine huamini kwamba kutumia vifaa vya ngono/kufanya mapenzi ni njia ya kuongeza uhusiano wao na wenzi wao. Hawa huona kwamba kutumia vifaa hivyo ni njia ya kujifunza jinsi ya kumfurahisha mwenzako na kuleta furaha zaidi kwenye uhusiano wao wa kimapenzi.
Kama unavyoweza kuona, kuna maoni mengi tofauti kuhusu kutumia vifaa vya ngono/kufanya mapenzi. Ni muhimu kukumbuka kwamba kila mtu ni tofauti na ana maoni yake kuhusu suala hili. Hivyo, unapaswa kufanya uamuzi wako mwenyewe kulingana na maoni yako na kuwaheshimu wengine ambao huenda wana maoni tofauti.
Kama unataka kutumia vifaa vya ngono/kufanya mapenzi, ni muhimu kutumia vifaa vilivyo salama na kujitunza wewe mwenyewe na wenzi wako wa karibu. Unapaswa kujifunza jinsi ya kutumia vifaa hivyo vizuri na kuzingatia usafi na afya yako.
Kumbuka, kutumia vifaa vya ngono/kufanya mapenzi ni jambo la kawaida na inaweza kusaidia kuongeza furaha yako na ya wenzi wako. Hivyo, usiogope kujaribu vitu vipya na kujifunza zaidi kuhusu miili yetu na jinsi inavyofanya kazi.
Msichana ambaye hajawahi kujamiiana anaitwa bikira, je mvulana huitwaje?
Updated at: 2024-05-25 16:22:16 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Neno “bikira” ni mtu yeyote ambaye hajawahi kujamii ana maishani mwake, awe mwanamke au mwanaume. Zamani, watu walimtambua msichana bikira kwa njia ya kuhakikisha kwamba kile kiwambo chembamba ndani ya uke kipo. Lakini kwa sababu ngozi hii huweza kuchanika kwa njia nyingine zaidi ya kujamii ana, siyo kipimo kizuri cha kumtambua msichana ambaye hajajamii ana kabisa (yaani bikira). Katika jamii nyingi ni kawaida kuwaita `bikira` wanawake ambao hawajawahi kujamii ana. Pia, jamii nyingi wanasisitiza umuhimu wa mwanamke kuwa bikira mpaka siku ya kuolewa. Hata hivyo, neno “bikira” hutumiwa kwa wanawake na wanaume.
Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hukufanya uwe na nguvu?
Updated at: 2024-05-25 16:22:37 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Si kweli kabisa! Baada ya kuvuta bangi mtu hujiona kama jasiri sana na mwenye nguvu. Lakini madhara ya bangi ni kinyume na matarajio ya mtumiaji kwani mishipa husinyaa na ubongo hushindwa kufanya kazi zake vyema na kutoa uamuzi usio sahihi wa utendaji sahihi wa kazi za mwili.
Ni katika umri gani vijana wana haki ya kujihusisha na mambo ya kujamiiana?
Updated at: 2024-05-25 16:24:04 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kujamiiana ni uamuzi wa mtu binafsi. Ni uamuzi wako na hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kukuamulia. Lakini unapoamua kujamiiana hakikisha kwamba ni maamuzi uliojulishwa na kwamba unaelewa matokeo ya kujamiiana. Usisahau kuchukua hadhari muhimu. kumbuka kutumia kondomu kujikinga wewe na mwenzi wako kutokana na mimba usizotarajia na magonjwa kama vile Virusi vya UKIMWI. Madhari mwili wako unaendelea kukua, kujamiiana bila ya kondomu ni hatari zaidi kuliko mtu mzima, kwa sababu maambukizo mengine haswa kwa vijana yanaweza kukuletea matatizo kama vile ugumba baadaye katika maisha. Pia jiulize mwenyewe kwa uangalifu kama kweli unataka kujamiiana. Ni muhimu pia kujadiliana na mwenzi wako na kuwa na hakika kama wote wawili mnataka kujamiiana. Usijamiiane kwa sababu tu unafikiria kwamba watu wengine wanajamiiana au unajitosa kwa kuwa unashawishiwa na marafiki au watu wazima.