Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe
Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki; MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu atakubariki zaidi
Updated at: 2024-05-25 18:06:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi
PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!
Updated at: 2024-05-25 17:09:19 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nimefumaniwa hapa na jamaa ameniambia nitulie tuyamalize kishikaji, yaani nisijali sasa ametoka nje nasikia ananoa kisu nadhani anataka anichinjie kuku!
Dogo alivyomchomea dada wa kazi kwa mama yake kuhusu baba
Dogo: mama hivi malaika si wanapaa?
Mama: ndiyo wanapaa, kwanini umeniuliza hivyo?
Dogo: nimesikia baba jana anamuita dada (housegir) malaika wangu, kwa hiyo nae atapaa?
Updated at: 2024-05-25 18:06:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dogo: mama hivi malaika si wanapaa?
Mama: ndiyo wanapaa, kwanini umeniuliza hivyo?
Dogo: nimesikia baba jana anamuita dada (housegir) malaika wangu, kwa hiyo nae atapaa?
Mama: ndiyo atapaa kuelekea kijijini kwao kesho, pumbavu zake.
Updated at: 2024-05-25 17:51:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
UTOFAUTI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME 1. Kwenye mshituko; mwanaume hushituka halafu huangalia nini kimemshitua, mwanamke hushituka halafu huzimia hivyo ataambiwa na mwanaume kilichomshitua😂😂 2. Kwenye kupenda; mwanaume huanza kutamani alafu hupenda, mwanamke huanza kupenda moja kwa moja bila kumjua vizuri huyo ampendae😂😂😂 3.Kwenye kusaidia; mwanaume hutoa msaada alafu uhuzunika, mwanamke huuzunika badae ndo anakumbuka km msaada unahitajika😂😂😂 4.Kwenye maamuzi; mwanaume hufikiri ndipo hutenda, mwanamke hutenda halafu hufikiri😂😂😂 5.Kwenye kudanganya; Mwanaume hudanganya ili kumlinda mwanamke, mwanamke hudanganya ili kumkomoa mwanaume😂😂😂 6.Kwenye ugomvi; wanaume hupigana halafu hueshimiana, wanawake hupiga mikelele alafu kila mmoja hurud kwake, kexho tena😂😂😂 7.Kwenye ndoa; mwanaume hutafuta maixha ndipo huoa, mwanamke huolewa ndipo atafute maisha😂😂😂 8.Kwenye kukata tamaa; mwanaume hukata tamaa mapema ili jambo lisimsumbue, mwanamke hajui kukata tamaa hadi aumizwe😂😂😂 9.Kwenye kula;Mwanaume hushiba alafu huanza madoido, mwanamke huanza na madoido alafu badae hujilaumu hakushiba😂😂 10.Kwenye siri; Mwanaume hutunza siri hasa za aibu, mwanamke humueleza shoga yake badae hugombana nae baada ya kumrudia mwenyewe kwa siku 2 tu😂😂😂 Hizi ni baadhi tu ya sifa tofauti kati ya mwanaume na mwanamke….. VIVA GENTLEMEN👊🏽👊
Jamaa kaenda kanisani akakaa karibu na mrembo.
Wakati mahubiri yakiendlea jamaa akaanza kuingiza vocal:
Jamaa: dada mi nakupenda saana
Dem: Kaka naomba umsikilize mchungaji
Updated at: 2024-05-25 18:03:29 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa kaenda kanisani akakaa karibu na mrembo.
Wakati mahubiri yakiendlea jamaa akaanza kuingiza vocal:
Jamaa: dada mi nakupenda saana
Dem: Kaka naomba umsikilize mchungaji
Jamaa: nipe nafasi uwe msimamizi wa serikali ya moyo wangu…
Dem: niache…
Jamaa: kweli nakupenda mpnz
Dem: (kwa sauti kubwa) nmesema NIACHEEEE!!
Watu wote kanisani wakageuka… Jamaa kaona noma na ili atulize msala
Jamaa: sikuachi hadi ukiri YESU kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yako.
Haya ndiyo madhara ya kutowapeleka watoto kanisani ⛪
Updated at: 2024-05-25 17:08:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MTOTO aliibiwa yeboyebo KANISANI akawa analia sana kwa uchungu mpaka MCHUNGAJI akamwambia usilie mwachie MUNGU. MTOTO akajibu Mungu hazimtoshi zile yebo ni ndogo! Usicheke,
Huu ni Mtihani Tuwapeleke Watoto KANISANI Wamjue MUNGU.
Jamaa kaingia Bar; Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,
Updated at: 2023-04-29 22:53:32 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Jamaa kaingia Bar; Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,
Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi. Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapo…….