Log in to access your menu with tools for managing ๐ tasks, ๐ฅ clients, ๐ฐ finances, ๐ learning, ๐ personal growth, and ๐ spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 17:54:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kama umesoma st Kayumba utakuwa una aidia na hayaโฆ
1.Unaenda shule umechelewa unakuta mwalim anakamata wachelewaj unaamua urudi nyumbani 2.unachukua kimbegu cha ubuyu unasugua sakafuni af unamuunguza mwenzio 3.mkiruhusiwa tu unakimbia unataka uwe wa kwanza kwenye njia yenu y kurudia nyumban 4.MTU akikukera unamfungia shule (mnapigana baada ya kufunga shule) 5.MTU akikunyima kitu chake unamwambia "Ahaa eeh utaona sa nne" 6.wadada wembamba ndo wanaongoza kwa kusuta wenzao 7.ukiibiwa daftar jipya unalia kuliko hata uliloandika 8.unajaza mapeni kwenye mkebe(compass) na mengine hayaandiki 9.vifaa vingine kwenye mkebe hujawahi hata kuvitumia mfano bikari labda utolee mwiba๐ 10.hakuna habari nzur kama kuambiwa Leo hamna shule mwalim haupo 11.habari mbaya zaidi n kurud nyumban kutoka shule una njaa af unaambiwa chakula mgeni kaja tumempa 12.mtoto wa mwalim utamgundua tu kwanzia sweta begi na viatu vyake 13.usiombee umpige mtoto wa mwalim utataman uache shule 14.unatengeneza kifutio cha ndala af unatishia eti kinafuta hadi peni๐ 15.ukaguzi na huna ufagio.. unaomba chelewa kwa watu af unaongeza kijiti katikati 16.siku ukienda na ufagio wanakagua maji, ukienda na naji wanakagua kuni au mbolea๐ ๐ Dah shule zetu hizi kiboko!!
Updated at: 2024-05-25 17:45:32 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae maana hta hela ya kula Jana sikua nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu?
Updated at: 2024-05-25 17:14:03 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAMBO YA FEDHA AISEEโฆโฆ. Kuna jamaa alipewa shilingi 983628763600/= โฆacha uvivu, najua hujasoma ni kiasi gani hicho cha fedha na mbaya zaidi hujagundua kwamba katikati ya namba hizo kuna herufi Aโฆ safi sana, najua umeangalia tena kuiona hiyo herufi, bahati mbaya hujaiona. ๐๐๐๐๐๐๐
Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
"Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana."
Padri, "Endeleaโฆ"
Updated at: 2023-04-29 22:53:14 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani peke yake. Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama {confess} "Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana." Padri, "Endeleaโฆ"
"Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa kufungwa. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu,nikatoa bastola nikamuuaโฆ.. Yesu atanisamehe?"
Padri: "Utasamehewa." "Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona kilichotokea akasema anapiga polisi simu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye piaโฆ Yesu atanisamehe hilo?" Padri: "Utasamehewa."
Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuuaโฆ.. Yesu atanisamehe?" Padri:"Utasamehewa."
"Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua? Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke yetu, nikamuuaโฆ.. Yesu atanisamehe na hilo?"
Kimyaaโฆ. "Padri yesu atanisamehe?" kimyaโฆ.
Jamaa akatazama kwenye confession booth padri hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.
Jamaa, "Sasa baba mbona umekimbia?" Padri kwa taabu akajibu, "Nilitazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetuโฆโฆ."
Updated at: 2023-04-29 22:53:42 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
FACT! 1.Ukiona geto lina feni, sabufa, meza ya plastic na kitanda ch sita kwa sita na Pc UJUE ni jamaa wa UDSM.
2. Ukaona geto lina nguo nyingi za watu tofauti tofauti, unga mwingi, vtunguu vng, nyanya halaf pembeni, Vitabu vya kutosha na lundo la karatasi za betting ujue huyu JAMAA ni wa SAUT.
3. Ukaona geto halina kitu ndani zaidi ya mkate wa bakheresa na kopo la maji UJUE huyu jamaa ni wa UDOM๐โ
4. Ukaona geto lina visamaki vikavu mezani, Notes za kutosha mezani na jaba pembeni UJUE huyu ni MJAMAA WA MWENGE/MWECAU๐๐ค
5. Ukaona geto lina Mawigi mengi na dressing table pembeni, ngazi ya kuwekea viatu UJUE huyu mjamaa ni wa RUCO IRINGA๐
6. Ukaona geto lina spray za kila aina, Nguo nyingi hasa za mitumba ambazo zimemodolewa mpaka tight UJUE huyu MJAMAA ni wa USHIRIKA MOSHI.
7.Ukiona geto lina Nyanya na mikungu ya ndizi halafu halafu nje kuna jiko la Mkaa UJUE huyu mjamaa ni wa TEKU mbeya๐ณ
8. Ukiona geto lina tranka na nje wamevulia buti, viatu vya matope UJUE huyu Mjamaa ni Wa SMUCO MWIKA.
9. Ukaona geto ndan mashuka ya kimasai kinabao, hapa usipatwe na Mashaka, Jua huyu ni Mjamaa wa MAKUMIRA. ๐๐๐๐
10. Ukaona geto lina vimodo, vimini, miwani za tittled, jiko la mafuta ya taa, kitandani mito zaidi ya Minne,Visarafu kwenye meza, Tshirt nyingi za semina za family planning, Ukimwi n.k halafu chini tv ya chogo na king'amuz cha continental Ujue huyu MJAMAA ni wa TIA DSM ๐ฑ๐ฑ๐ฑ๐ฑ๐ฑ๐ฑ๐ฑ
โฌโฌโฌโฌโฌโฌโฌโฌโคตโฌ๐๐๐๐ JE, KWAKO KUKOJE? ??? ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Updated at: 2024-05-25 17:03:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mama mwenye nyumba anajipodoa anashinda saloon kujipodoa lakini house girl hata mafuta usoni hapaki lakini akipita na khanga yake moja tuu nyumba inatetemeka๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐ huu mchezo hautaki mekapu