Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
SMS nzuri ya kumtumia mpenzi wako mnapogombana na kukorofishana
Updated at: 2024-05-25 15:22:26 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
teke la kuku halimuumzi mwanaye sawa na dhati ya mapenzi haiumzi moyo wa ampendaye,tugombane sasa hivi tupatane badaye,najua hakuna wasiogombana ,kama wapo siku wakigombana wataachana.
SMS ya ujumbe wa kimahaba wa kifumbo kwa mpenzi wako
Updated at: 2024-05-25 15:25:36 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kila mtu anataka kuwa jua linalong’arisha maisha yako, lakini ni afadhali niwe mwezi, ili nikuangazie wakati wa giza ambapo jua limechwea na haliangazi tena.
Ujumbe wa kumhasa mpenzi wako akupende kama unavyompenda
Updated at: 2024-05-25 15:37:04 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
yakumbuke haya sana katika maisha yako wahurumie wenye kukupenda hasa mwenye pendo la dhati kama langu,wapende wanaokupenda japo kwa chembe ya upendo,thamini pendo la akupendae kwa kila mara japo sekunde moja.
SMS kali sana yenye ujumbe wa kimahaba kwa mpenzi wako
Updated at: 2024-05-25 15:25:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Natamani ningekuwa chozi jichoni mwako ambapo ningetelemka na kuishia midomoni mwako, lakini kamwe sitamani uwe chozi jichoni mwangu nitakupoteza kila muda niliapo.
Ujumbe wa kimahaba wa kumtumia mpenzi wako aliyeko mbali na wewe kumwambia unavyommisi
Updated at: 2024-05-25 15:27:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mawingu yametanda napanda kwenye kitanda, macho nayaangaza, taratibu navuta shuka na kujitanda, mishumaa pembezoni inaniangaza, mziki laini wanibembeleza kitu pekee nilichokikosa ni joto lako na vijimambo vyako kunako kitanda!
Ujumbe mzuri wa kumwambia mpenzi wako kuwa yeye tuu mdiye kakutawala
Updated at: 2024-05-25 15:36:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.
SMS ya kumsisitiza mpenzi wako asiende kwa mwingine
Updated at: 2024-05-25 15:26:03 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
chekecho la huba ,toka uvunguni mwa moyo wangu navika moyo wako taji la upendo,na kupulizia marashi ya hubaa ,usimpe mwingine mi ndiye ninayejua kulea.