Sidebar with Floating Button
AckySHINE 🔁
AckyShine

SALA YA KUOMBEA FAMILIA

Featured Image

Ewe Mungu Mwenyezi, sisi kama familia tunakushukuru kwa zawadi ya Mama Kanisa Katoliki ambaye siku zote hutupatia malezi bora kwa ajili ya wokovu wetu. Kanisa halichoki kutuhimiza tutafakari na kuishi utakatifu wa familia ya Nazareti ya Yesu, Maria na Yosefu. Familia hii iliishi upendo uliojengwa kwa fadhila za imani, uaminifu, utii, uvumilivu na upole hata wakawa watakatifu. Tunapoadhimisha mwaka wa Familia, tunaiweka mbele yetu familia ya Nazareti iwe dira, baraka na mfano kwa familia zetu.

83 💬 ⬇️

Sala fupi ya Asubuhi

Featured Image

Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu Mwenyezi, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, milele na milele, Amina.

Ee Utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, nasadiki kuwa upo hapa na mahali pote. Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristo, umenizidishia neema zako hapa duniani, umenitayarishia makao yangu mbinguni, umenijalia na siku hii nikutumikie. 

83 💬 ⬇️

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU KWA SIKU ZOTE TISA

Featured Image

Ufuatao ni mtiririko wa Novena ya Roho Mtakatifu kwa siku zote tisa.

Kusali novena hii unaanza nia wimbo/nyimbo kisha unasali sala ya kila siku na kumalizia na litania na Atukuzwe Baba….x3 kwa siku zote tisa

86 💬 ⬇️

SALA KWA MT. YOSEFU KUOMBA KUFAHAMU WITO WAKO

Featured Image

Ee uliye Mkuu, Mt. Yosefu, uliyatii kabisa maongozi ya Roho Mt. Unijalie neema ya kufahamu aina ya maisha ambayo Mungu anapenda mimi niishi. Usiniache nidanganyike katika jambo muhimu kama hili, ambalo furaha yangu hapa duniani inalitegemea, na hata pia wokovu wa roho yangu.

83 💬 ⬇️

ATUKUZWE BABA

Featured Image

Atukuzwe Baba
na Mwana
na Roho Mtakatifu
Kama mwanzo
na sasa,
na siku zote,
na milele.
Amina.

83 💬 ⬇️

Sala ya Baba Yetu: Sala ya Bwana

Featured Image
Baba Yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe; ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
83 💬 ⬇️

SALA YA NOVENA KWA MOYO MTAKATIFU WA YESU

Featured Image

Ee Moyo Mtakatifu sana wa Yesu, chemchemi ya kila baraka, ninakuabudu, ninakupenda, na kwa majuto halisi ya dhambi zangu, nakutolea moyo wangu dhaifu. Nifanye mnyenyekevu, mvumilivu na safi, nikikubali na kuyatii kabisa mapenzi yako. Ee Yesu mwema, unijalie niishi nawe na kwa ajili yako.

83 💬 ⬇️

LITANIA YA KUWAOMBEA MAPADRE WOTE II

Featured Image
Kwa ajili ya Baba Mtakatifu wetu ..(N); Bwana, umpe moyo wako wa uchungaji mwema Kwa ajili ya makardinali na maaskofu wakuu; Uwape moyo wa kichungaji ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wa majimbo; Uwajaze na Roho wako ee Bwana Kwa ajili ya mapadre watawa; Wakamilishe katika wito wao ee Bwana Kwa ajili ya mapadre walioko hatarini; Uwaokoe ee Bwana
83 💬 ⬇️

SALA YA MTAKATIFU INYASI

Featured Image

Roho ya Kristo unitakase
Mwili wa Kristo uniokoe
Damu ya Kristo unifurahishe
Maji ya ubavu wake Kristo yanioshe
Mateso ya Kristo nguvu yanizidishie
Ee Yesu mwema unisikilize

85 💬 ⬇️

SALA YA MATUMAINI

Featured Image

Mungu wangu, natumaini kwako nitapewa kwa njia ya Yesu Kristu, neema zako duniani na utukufu mbinguni, kwani ndiwe uliyeagana hayo nasi, nawe mwamini. Amina

83 💬 ⬇️
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About