Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
eBooks: Biashara - Mbinu za Ujasiriamali na Biashara Kufanya tofauti - Topic 2 - AckySHINE
Umasikini isiwe sababu wala utajiri isiwe sababu ya kuwa mchafu au kutokuwa na usafi
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:35 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Umasikini sio sababu ya kuwa mchafu wala utajiri Sio kuwa na kila kitu hata kama hukihitaji. Hebu angalia hapo nyumbani kwako!
Vitu msivyovihitaji Leo wala kesho mmeweka vya nini? Umenunua makochi mapya Yale ya zamani mmegawana vyumbani mnaishia kurundika minguo hapo na kufuga mipanya.
Godoro umenunua jipya la zamani umeviringisha juu ya kabati. Kabatini kwako kuna nguo ulivaa ukiwa secondary mpaka Leo unazo eti ukumbusho au utazivaa ukipungua.
Updated at: 2024-05-23 16:07:34 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Sikia haihitaji ukalishwe chini ndo uelewe, Ukweli ni kwamba unajishughulisha Sana na mambo yasiyo Kuhusu katika mafanikio.wazungu husema mind your own business sasa Sijui huu msemo unauchukuliaje?? Imagine unamjua Ali kiba hadi bafuni kwake, tour zote za mwaka huu unazijua hadi nyingine unataka kumpangia, nikuulize wewe ni mwanamziki??
Updated at: 2024-05-23 16:07:17 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu ambao hawana pesa ila wana muda wa bwerere. Hawajui thamani ya muda. Hawa ndo wale ambao hawajui cha kufanya. Anaamka mpaka analala usiku hana specific timetable. Unaweza kumkuta anaenda dukani ukamwambia nisindikize saluni na akakubali. Yupo yupo tu. Unaweza kuta ameingia Facebook hajui hata kwa mini. Basi tu kwa sababu ana bando. Akiperuzi akaona mahali wanaongelea mpira yumo
Updated at: 2024-05-23 16:07:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa miezi 12 au kwa mwaka.
Katika hayo masaa 24 unayoyapata kila siku unayatumiaje katika suala zima la kukufikisha katika ndoto na malengo au mafanikio yako?
Kwa nini kuna matajiri na maskini na wote tunapewa masaa 24??? Tucheki mgawanyo Wa masaa 24 ulivyoβ¦.katika masaa 24 unayopewa kwa siku masaa 8 ni ya kazi,masaa 8 ni ya kulala na masaa 8 ni ya kufanya mambo yako mengine.
Updated at: 2024-05-23 16:07:35 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kama umeajiriwa au pia umejiajiri ni mojawapo ya njia zinazokuingizia kipato maana wengi wanaanzia hapo mpaka kuja kufikia kule wanakohitaji. Ila kuna maswali machache ya kukupa changamoto ambayo nataka ujiulize:-
Updated at: 2024-05-23 16:07:34 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ikiwa leo ni tarehe **1/12Β huwezi amini kuwa hakuna tarehe 1 nyingine tutakayoiona ya mwaka huu hivyo sichelei kusema kuwa mwaka umeisha .Lakini mwaka unaishaje??? pengine hili ndilo swali gumu na la muhimu la kujiuliza .Je, Mwaka unaisha ukiwa umefanya nini cha kujipongeza??? .Je mwaka unakaribia kuisha maarifa yako yakiwa yameongozeka kwa kiasi gani???.Haya ni maswali muhimu sana unavyooanza kufikiria juu ya sherehe za mwisho wa mwaka.
Hichi ndicho unatakiwa uwe nacho kulingana na umri wako
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:26 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
20 - 25 =Iwe kama ni kielimu hujafikia malengo yako,sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kufanya,pigana kufa na kupona ili kama vipi urudi shule kwa pesa yako.
25 - 30 = Hakikisha uwe na angalau na SHUGHULI RASMI kama umeajiliwa au umejiajili.
30 - 35 = Uwe na angalau kama sio nyumba basi kiwanja,tena ujitahidi uwe umeoa/umeolewa kama sio kuishi nae,tena si mbaya ukawa umeshatengeneza familia,kwa maana ya kuwa na watoto kama mungu kakuwezesha.
Updated at: 2024-05-23 16:07:17 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu anayejengaΒ GHOROFAΒ na yule anayejengaΒ Nyumba ya KAWAIDA.
AnayejengaΒ GhorofaΒ anatakiwa achimbe msingi Mrefu kwenda chini kabla hajaanza kuinuaΒ GhorofaΒ yake juu. Hivyo wakati huyu mwingine anapokuwa anajenga Nyumba ya kawaida atakapokuwa tayari anakaribia hata kuezeka, unaweza kukuta yule anayejengaΒ GhorofaΒ bado yuko kwenye Msingi. Ila siku akianza kuinuaΒ GhorofaΒ lake, kila mtu atashangaa urefu wa juu atakaoenda nao.
Wewe ni mshindi: Mambo yakuzingatia ili uweze kushinda chochote katika maisha
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mshindi ni mtu aliyeshinda, Hivyo wewe ni mshindi kwa kuwa umeshinda, kuwa hai leo ni ushindi, kuwa na Mungu mpaka sasa huo ni Ushindi, kuweza kujifunza semina na kufuatilia mafundisho kama haya wewe ni mshindi. Ebu jiulize ni watu wangapi ulikuwa unawafahamu leo hawapo duniani? Wewe umeshinda Mungu kakuweka duniani ili uendelee kushinda.
Updated at: 2024-05-23 16:07:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kazi au shughuli unayoifanya ina thamani gani kwa wengine?unawasaidia au unawaumiza?? Biashara unayoifanya ina thamani gani kwa wengine?ni lazima uwaumize ndipo ufaidike au uwasaidie ili nawe upate faida?
Elimu yako uliyo nayo ina faida au thamani gani kwako na kwa wengine?unawadharau na kujiona wewe ndiye msomi pekee au unawasaidia?
Updated at: 2024-05-23 16:07:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ili kutoka hapo ULIPO uweze kwenda HATUA inayofuata kuna SWALI muhimu sana unahitaji kujiuliza. Watu ambao huwa wanashindwa kupiga hatua katika maisha yao ni kwa sababu huwa wanajiuliza kinyume cha swali hili. Swali hili ndilo wanalojiuliza watu wote waliofanikiwa:
Swali: "Hivi kwa sasa nina nini ambacho naweza kuanza kukitumia kama mtaji wa kwanza kuanza kufanya ninachotaka"?
Ushauri wangu kwa leo: Zingatia hili, hamasika, badilika
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tupo kwenye dunia ambayo tulikuta watu na tutawaacha watu. Vyote tulivyovikuta vilianzishwa na binadamu wengine wenye mawazo mema na wenye mawazo mabaya pia. Vitu vingi tunavyovifanya tunaendeleza tulivyovikuta ni mara chache kukuta kitu kipya ambacho hakitegemei mazingira na asili ya tulivyovikuta.
Updated at: 2024-05-23 16:07:27 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Habari za Leo Rafiki yangu wa Muhimu sana. Ni furaha yangu kujua unaendelea vyema sana na majukumu yako.
Ni wakati mwingine tena tunaenda kujifunza pamoja juu ya mambo mbalimbali ili tuweze kufikia mafanikio kila siku. Leo tunakwenda kujifunza kuhusu pesa na utajua mambo mengi sana juu ya pesa.
Angalia jinsi maamuzi yako ya jana na ya leo yanavyoweza kukuathiri
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nimeitoa kwa Comrade Markus Mpangala na kuitafsiri kwa Kiswahili (kisicho rasmi sana). Mwaka 1998 "Google" walitaka kuiuza kampuni yao kwa "Yahoo" kwa dola Milioni 1 (sawa na Shilingi Bilioni 2) lakini Yahoo wakakataa. Yani Yahoo wakakataa kuinunua Google.
Updated at: 2024-05-23 16:07:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Batiki inatengenezwa kama ifuatavyo
MAHITAJI:
1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali. 2.Sponji zenye urembo mbalimbali. 3.Brash kubwa/ndogo. 4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili. 5.Sufuria. 6.Vitambaa vya mpira. 7.Misumari midogo. 8.Jiko.
Updated at: 2024-05-23 16:07:05 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
1. Epuka kugeuza mshahara wako kuwa mali ya ukoo. Kamwe mshahara wako siyo mali ya ukoo. Siku utakapoacha kuufanya mshahara wako mali ya ukoo ndipo siku mshahara huo utakuwa mkubwa! Hapo ndipo mshahara utatosha.
2. Siku utakapokuwa na vyanzo vya mapato zaidi ya mshahara wako ndipo mshahara wako utakapotosha mahitaji yako ya kila mwezi.
Updated at: 2024-05-23 16:07:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tafuta fursa kila kona. Tumia kipaji chako. Kuwa na nidhamu katika fedha - matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk.
Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyoteΒ - kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.
JITAMBUE : Maisha yako ya kesho hayalingani na maisha yako ya jana, Anza sasa
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:24 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
THERE IS NO FUTURE IN THE PAST.** Ukitaka kufanikiwa usiangalie nyuma yako kunanini na ulishindwa mara ngapi. Siku zote kukaa Chini nakuanza kujuta kwa makosa uliofanya uko nyuma nikupoteza muda, huo muda Utumie kwa kupanga ya kesho.
Updated at: 2024-05-23 16:07:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ebu fikiria Dada anayechoma mahindi maeneo ya Manzese Darajani kuanzia saa 12 jioni mpaka SAA 2 usiku, kwa siku moja anauwezo wa kuchoma mahindi .50. Kila hindi moja ananunua shambani kwa shilingi 100/- Na Anauza kwa sh.600/-
Updated at: 2024-05-23 16:07:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ndoto ni nini? Ndoto ambayo tunakwenda kuizungumzia sio ndoto unayoota ukiwa umelala ni ndoto ya mchana. Ni kile kitu unachotamani kuja kukipata siku moja kabla hujaondoka duniani Ndoto inaweza kua katika makundi ya aina mbalimbali, unaweza kua na ndoto ya kuwa Rais, Mwimbaji bora, Mchezaji bora, Mwandishi Bora, Mfanyabiashara maarufu. Vile vile unaweza kuwa na ndoto ya kumiliki vitu, nyumba nzuri ya kifahari sana labda ya milioni 300, Gari la kifahari sana, Unaweza kuwa na ndoto ya kumiliki utajiri au kuwa Bilionea,Kutembelea nchi fulani na kadhalika.
FURSA HAIJI MARA MBILI: Jinsi unavyoweza kupata faida au hasara ukitumia Nafasi au fursa uliyonayo
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:29 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwenye maisha fursa moja tu inatosha kabisa kubadilisha hali yako ya sasa na kukuweka kwenye kiwango kingine kabisa cha mafanikio.Kuna watu wengi sana ambao waliwahi kufikiria kuwa maisha yao yatachukua miaka mingi sana kabla hayajabadilika na kwa mshangao wao walipoanza kufanya vitu sahihi wakakutana na mabadiliko makubwa sana katika maisha yao kwa kupitia fursa moja tu.