Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
FURSA HAIJI MARA MBILI: Jinsi unavyoweza kupata faida au hasara ukitumia Nafasi au fursa uliyonayo
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:29 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwenye maisha fursa moja tu inatosha kabisa kubadilisha hali yako ya sasa na kukuweka kwenye kiwango kingine kabisa cha mafanikio.Kuna watu wengi sana ambao waliwahi kufikiria kuwa maisha yao yatachukua miaka mingi sana kabla hayajabadilika na kwa mshangao wao walipoanza kufanya vitu sahihi wakakutana na mabadiliko makubwa sana katika maisha yao kwa kupitia fursa moja tu.
USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:03 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako.
Ndio maana licha ya kwamba elimu ni yako wewe, maarifa ni yako wewe, vyeti ni vyako wewe; na kazi unafanya wewe; lakini hao waliokuajiri ndio wanakuamulia kiasi gani wakulipe! Si hivyo tu bali pia wanao uhuru wa kukupiga mkwara, kukutishia na hata kukufukuza muda wowote (utakapowakosea, watakapojisikia ama watakapokuchoka)! Nini nakwambia? Kama umeajiriwa, usiridhike wala usibweteke na mshahara pekee kwa 100%, hebu jiongeze aiseee, una uwezo wa kuzalisha zaidi sambamba na mshahara (waliojisikia) kukulipa.
Angalia jinsi maamuzi yako ya jana na ya leo yanavyoweza kukuathiri
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nimeitoa kwa Comrade Markus Mpangala na kuitafsiri kwa Kiswahili (kisicho rasmi sana). Mwaka 1998 "Google" walitaka kuiuza kampuni yao kwa "Yahoo" kwa dola Milioni 1 (sawa na Shilingi Bilioni 2) lakini Yahoo wakakataa. Yani Yahoo wakakataa kuinunua Google.
Siri 39 za kuwa Milionea, Jinsi ya kupata pesa na kuwa tajiri
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:16 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
1. Tafuta fursa kila kona. 2. Tumia kipaji chako. 3. Kuwa na nidhamu katika fedha - matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk. 4. Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyote - kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.
Wewe ni mshindi: Mambo yakuzingatia ili uweze kushinda chochote katika maisha
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mshindi ni mtu aliyeshinda, Hivyo wewe ni mshindi kwa kuwa umeshinda, kuwa hai leo ni ushindi, kuwa na Mungu mpaka sasa huo ni Ushindi, kuweza kujifunza semina na kufuatilia mafundisho kama haya wewe ni mshindi. Ebu jiulize ni watu wangapi ulikuwa unawafahamu leo hawapo duniani? Wewe umeshinda Mungu kakuweka duniani ili uendelee kushinda.