Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.

UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Je, watu wanapendelea kutumia vitu kama vile nguo za ndani za kimapenzi wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kutumia vitu kama vile nguo za ndani za kimapenzi wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Karibu tena kwenye blogu yetu ya mapenzi. Leo tutaangazia swali linaloulizwa mara kwa mara kuhusu... Read More

Jinsi ya kushirikiana na mke wako katika Kulea Watoto

Jinsi ya kushirikiana na mke wako katika Kulea Watoto

Kushirikiana na mke wako katika kulea watoto ni muhimu katika kujenga familia yenye nguvu na yenye u... Read More
Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Kuwa na Maisha ya Kijamii katika Familia

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Kuwa na Maisha ya Kijamii katika Familia

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Kuwa na Maisha ya Kijamii katika Familia

Fami... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Nafasi ya Kujifunza na Kupata Maarifa katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Nafasi ya Kujifunza na Kupata Maarifa katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Nafasi ya Kujifunza na Kupata Maarifa katika Familia

  1. ... Read More
Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kujifunza na Kukua katika Familia

Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kujifunza na Kukua katika Familia

Karibu katika makala hii ambapo tutaangazia jinsi ya kuunda mazingira ya kujifunza na kukua katik... Read More

Faida na Hasara za Kufanya Mapenzi

Faida na Hasara za Kufanya Mapenzi

Mapenzi ni kitu cha maana sana katika maisha yetu. Yana faida nyingi sana lakini pia yanaweza kuw... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha stadi za mawasiliano

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha stadi za mawasiliano

Kama wapenzi, tunahitaji kuwa na uhusiano mzuri na kudumisha stadi za mawasiliano ili kuboresha u... Read More

Njia za Kupunguza Mizozo ya Kifedha katika Familia yako

Njia za Kupunguza Mizozo ya Kifedha katika Familia yako

  1. Elewa matumizi na mapato: Njia mojawapo ya kupunguza mizozo ya kifedha katika familia y... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mazingira ya upendo na uaminifu katika ndoa

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mazingira ya upendo na uaminifu katika ndoa

Ndani ya ndoa, upendo na uaminifu ni vitu ambavyo vinatakiwa kujengwa na kudumishwa kila wakati. ... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kusawazisha Majukumu na Kupanga Ratiba katika Familia Yako

Kuweka Kipaumbele cha Kusawazisha Majukumu na Kupanga Ratiba katika Familia Yako

Hakuna jambo bora kuliko kuwa na familia yenye maadili, mshikamano, na usawa. Kuweka kipaumbele c... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu ndoto na malengo ya kazi na kazi ya kila mmoja

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu ndoto na malengo ya kazi na kazi ya kila mmoja

Kwa wapenzi wengi, kuwa na ndoto za kazi na malengo ni sehemu muhimu ya maisha yao. Kwa hiyo, ni ... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kutowajali na Kukosa Ushirikiano katika Familia Yako

Kukabiliana na Mazoea ya Kutowajali na Kukosa Ushirikiano katika Familia Yako

Kukabiliana na Mazoea ya Kutowajali na Kukosa Ushirikiano katika Familia Yako

Familia ni k... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About