Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE 🔁
AckyShine

Mambo ya Msingi kuyajua kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu

Featured Image
Mojawapo kati ya magonjwa yanayohusishwa na umaskini na uchafu wa kupindukia ni ugonjwa wa Kipindupindu. Inaripotiwa kuwa Kipingupindu ni miongoni mwa magonjwa ambayo huathiri jamii maskini zaidi kwa kiasi kikubwa hasa hasa kwenye nchi zinazoendelea, kiasi kwamba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeuweka ugonjwa huu kama mojawapo ya viashiria vya maendeleo ya jamii husika.

Kwanini nchi zinazoendelea ndizo zinazokumbwa na ugonjwa huu?

Moja wapo ya changamoto zinazokabili nchi zinazoendelea ni jamii kutokuwa na uhakika wa kupata Maji safi na salama, pamoja na kutokuwa na mazingira safi kwa ujumla. Ndio maana mpaka leo nchi zinazoendelea ndizo zinazokumbwa na mlipuko wa kipundupindu au huwa katika hatari ya mlipuko wa ugonjwa huo.

Kipindupindu husababishwa na nini?

Ugonjwa huu hutokana na maambukizi katika utumbo mdogo wa binadamu uletwao na vimelea vya bacteria vijulikanavyo kitaalamu kama Vibrio cholerae.

Jinsi unavyoweza kuambukizwa

Kwa kawaida vimelea hawa hupendelea kuishi katika kinyesi cha binadamu. Mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa huu kwa kunywa maji ama chakula kilichochafuliwa na kinyesi chenye vimelea hivi vya kipindupindu. Mara baada kula chakula au kunywa maji yaliyochafuliwa, baadhi ya vimelea hivi huuwawa kwa tindikali iliyopo kwenye tumbo (stomach) pindi chakula au maji haya yanapoingia tumboni. Hata hivyo baadhi ya vimelea hawa hufanikiwa kukwepa ukali wa hii tindikali na hivyo kuendelea kuishi. Vimelea waliofanikiwa kuepukali tindikali ya tumbo la binadamu, hujongea kwenda kwenye ukuta wa utumbo mdogo kwa kutumia ‘maumbo’ maalum yaliyo kwenye miili ya ambayo huwawezesha kusafiri ama kwa kitaalamu huitwa flagella. Wawapo kwenye ukuta wa utumbo mdogo Vibrio cholerae hutoa sumu iitwayo CTX au CT (cholera Toxin) ambayo husababisha mtu kuharisha choo chenye majimaji, papo hapo kuendelea kutoa kizazi kingine cha vimelea hao nje kwa njia ya haja kubwa. Iwapo choo hicho cha mtu aliyeambukizwa kipindupindu kitachanganyika na chanzo cha maji au chakula, watu wengine huambikzwa kirahisi. Hali kadhalika iwapo ni kwenye choo ambacho hakipo kwenye mazingira ya usafi kuna hatari ya choo cha mwambukizwa kuchanganyika na chanzo cha maji au chakula na hivyo kupelekea watu wengi zaidi kuambukizwa ugonjwa huu.

Dalili za kipindupindu ni zipi?

Dalili za mwanzo kabisa za kipindupindu ni

• Kuanza Kuharisha ghafla choo chenye majimaji (ambacho rangi yake ni kama maji ya mchele) na chenye harufu mbaya kama shombo ya samaki. • Kutapika

Aidha mgonjwa wa kipindupindu huonesha dalili zakupungukiwa maji mwilini kama vile

• ngozi huwa kavu, • midomo kukauka, • mgonjwa kuhisi kiu kikali, • machozi kutoweza kutoka, • kupata mkojo kidogo sana, • Kuishiwa nguvu na kujisikia mchovu sana. • Macho kutumbukia ndani hasa kwa watoto.

Vipimo vya utambuzi wa Kipindupindu

Kwa kawaida kipindupindu huweza kugunduliwa na kutambuliwa kwa kutumia dalili. Hata hivyo ili kuthibitisha kuwa mlipuko uliotokea ni kweli kipindupindu, vipimo vifuatavyo huweza kufanyika; Kupima damu kwa ajili ya kuotesha vimelea vya kipindupindu maabara. Kuchunguza choo kwa kutumia darubini (dark field microscope) ambapo vimelea hivi vya V. cholerae huweza kuonekana. Vile vile choo hiki hutumika kuotesha vimelea vya v. cholerae kwa ajili ya utambuzi zaidi.

Tiba ya Kipindupindu

Lengo kuu katika kutibu kipindupindu ni kurejesha maji na madini ambayo mgonjwa wa kipindupindu hupoteza kwa wingi baada ya kuharisha na kutapika. Njia kuu zitumikazo katika kumrejeshea mgonjwa wa kipindupindu maji na madini aliyopoteza ni kwa kumpatia maji maalum yenye madini hayo kwa njia ya mdomo, yaani kwa kumpa anywe au kwa njia ya mshipa wa damu ambayo kitaalamu huitwa intravenously (i.v). ORS Pamoja na ORS hiyo ambayo imetengenezwa na kuwekwa kwenye paketi tayari kwa matumizi, Shirika la afya duniani (WHO) limetoa pia mwongozo wa kutengeneza maji yenye madini yanayohitajika mwilini (oral rehydration fluid) ambao ni rahisi na usio na gharama. ORS ya kutengeneza nyumbani kwa kadiri ya muongozo huo huitaji kuchanganya na • Lita moja ya maji safi na salama, • Changanya na vijiko vidogo vinane vya sukari, kisha • Ongeza na kijiko kidogo kimoja cha chumvi • Aidha, unaweza kuongeza nusu glasi ya juice ya machungwa au nusu ya ndizi (tunda) lilipondwapondwa kwa kila lita, ili kuongeza madini ya potassium na pia kuboresha ladha. Kwa wagonjwa wenye hali mbaya na wale wasioweza kunywa wenyewe, hupewa maji yenye madini mbambali kwa njia ya mshipa wa damu. Maji haya huitwa kitaalamu kama Ringer’s Lactate.

Mwongozo wa kufuata katika kutibu kipindupindu

Baada wa mgonjwa kuwasili katika kituo cha afya, hupimwa kiwango cha upungufu wa maji kilichopo mwilini. Kisha muhudumu wa afya husahihisha upungufu wowote wa maji utakaonekana kwa awamu mbili. Kwanza kwa kati ya masaa 4-6 ya kwanza tangu kuwasili kituoni na kuendelea mpaka hali ya kuishiwa kwa maji mwilini itakapoonekana imekwisha. Mhudumu wa afya hutakiwa kurekodi kwenye cheti maalum kiasi cha maji anayokunywa mgonjwa na kiasi cha mojo anachokojoa. Njia ya mshipa hutumika pale tu, hali ya mgonjwa inapokuwa mbaya sana au pale ambapo mgonjwa hawezi kunywa chochote mwenyewe. Aidha kiasi cha maji kitolewacho kwa njia hii ya mshipa wa damu hwa ni kati ya 50-100 mL kwa kilo za uzito wa mgonjwa kwa saa. Baada ya hapo, mgonjwa huendelea kupewa ORS anywe kwa kiwango cha 800 mpaka lita moja kwa saa.

Matumizi ya dawa katika kutibu kipindupindu

Ieleweke kuwa tiba sahihi na makini ya ugonjwa huu wa kipindupindu ni kumrejeshea mgonjwa maji na madini aliyopoteza wakati wa kuharisha na kutapika kwa njia ambazo zimeelezwa hapo juu. Matumizi ya dawa (antibayotiki) husaidia tu kufupisha muda wa kuwatoa wadudu na wala yasitumike kama tiba kuu ya ugonjwa huu. Baadhi ya dawa ambazo hutumika katika matibabu ya ugonjwa huu ni Azithromycin na Tetracycline.

Jinsi ya kuzuia kipindupindu

Mara kwa mara serikali na taasisi zake zimekuwa zikihimiza watu jinsi ya kujikinga na ugonjwa huu wa kupindupindu. Miongoni mwa njia zinazofaa katika kuzuia milipuko ya ugonjwa huu ni Upatikanaji wa maji safi na salama, watu hawana budi kuhakikisha kuwa maji ya kunywa yanachemshwa vyema kabla ya kuyanywa. Vile vile wanaweza kutumia chlorine katika maji ambayo huua vimelea hawa wa V. cholerae. Ni muhimu kunawa mikono baada ya kutoka chooni na kabla ya kula Tunashauriwa kufunika chakula kikiwa mezani ili nzi wasitue juu yake Inashauriwa kujenga choo umbali wa angalau mita 30 kutoka chanzo cha maji Inashauriwa kwa wasafiri watokao nchi zilizoendelea kupata chanjo iitwayo Dukoral, pindi wanaposafiri kwenda nchi zinazoendelea.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Faida na jinsi ya kutumia mbegu ya Parachichi kiafya

Faida na jinsi ya kutumia mbegu ya Parachichi kiafya

Leo nimekuletea matumizi ya mbegu ya parachichi yenyewe yaani ile inayokuwa katikati ya tunda la ... Read More

Matumizi ya kahawa kutibu presha ya kushuka au shinikizo la chini la damu

Matumizi ya kahawa kutibu presha ya kushuka au shinikizo la chini la damu

Kahawa husaidia kuongeza presha au shinikizo la damu. Unashauriwa Kunywa kikombe kimoja cha kahaw... Read More

Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume

Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume

Kula lishe bora

Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula... Read More

Utajuaje kama una upungufu wa maji mwilini? Dalili ni hizi

Utajuaje kama una upungufu wa maji mwilini? Dalili ni hizi

Upungufu wa maji ni pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho n... Read More
Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia Uwatu (Fenugreek)

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia Uwatu (Fenugreek)

Uwatu ni dawa nyingine ya asili inayotumika kutibu chunusi. Uwatu unaondoa sumu na maambukizi mba... Read More

Vyakula vinavyosaidia kuongeza kinga ya mwili

Vyakula vinavyosaidia kuongeza kinga ya mwili

Watu wengi tumekuwa tukijali kazi zetu za kila siku bila kujali hali ya afya zetu matokeo yake ku... Read More

Vyakula 7 vya kuepuka kula ili uwe na afya nzuri

Vyakula 7 vya kuepuka kula ili uwe na afya nzuri

Inasemwa kuwa “wewe ni kile unachokula” kwa kumaanisha kuwa mwonekano wetu na afya ya mwili n... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia baking soda

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia baking soda

Moja ya sababu za kutokea chunusi katika ngozi yako ni kuwepo kwa takataka au uchafu juu ya ngozi... Read More

Jinsi ya kujisaidia unapotokwa na damu Puani

Jinsi ya kujisaidia unapotokwa na damu Puani

Unapotokwa na damu puani fanya yafuatayo;
1. Simama wima na inamisha kichwa kwa mbele, kusim... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi za usoni kwa kutumia Parachichi na asali

Jinsi ya kutibu chunusi za usoni kwa kutumia Parachichi na asali

Unahitaji:

a)Kijiko kimoja cha asali
b)Parachichi 1

Hatua kwa hatua namna ya ... Read More

Sababu ya meno kubadilika rangi

Sababu ya meno kubadilika rangi

Wapo baadhi ya watu wanashindwa hata kuachia kicheko chenye bashasha hii ni kwa sababu meno yao y... Read More

Faida za kunywa juisi ya ubuyu

Faida za kunywa juisi ya ubuyu

Mungu ameumba miti na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni ... Read More

📖 Explore More Articles
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About