Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Namna ya kuongeza nguvu za kiume bila kutumia dawa

Featured Image
Upungufu wa nguvu za kiume umekua tatizo kubwa sana kwa wanaume wengi. Tatizo hili limewakumba wanaume wengi walio katika ndoa na hata wale ambao bado hawajaoa. Watu wengi wamekuwa wakisumbuka kutafuta utatuzi kwani tatizo hili huwafanya kuwa na wasiwasi wa maisha. Ndoa nyingi zimevunjika na mahusiano kuharibika kwa sababu ya tatizo hili. Kwa wanaume wenye umri mkubwa, upungufu wa nguvu za kiume unaweza usiwe ni tatizo kwani miili yao inakuwa tayari imechoka. Hizi hapa ni baadhi ya njia zitakazokusaidia kurudisha nguvu za kiume zilizokuwa zimepotea, au kuimarisha uwezo wako wa tendo la ndoa.

Epuka unywaji wa Pombe.

Tafiti zinaonesha kwamba pombe inakupa hamu au shauku ya kufanya tendo la ndoa lakini inakunyima uwezo wa kufanya tendo hilo, kwani hupunguza kiwango cha maji mwilini.

Fanya mazoezi ya viungo.

Watu wengi wameelemewa na magonjwa kwa sababu tu mwili haupatishi damu ya kutosha kwenda sehemu mbali mbali kama vile ubongo, ini na figo ambazo ndio sehemu zenye kuufanya mwili wako ufanye kazi katika uhalisia wake. Uume ili usimame kwa uimara, unatakiwa upate damu ya kutosha. Kufanya mazoezi hupunguza kiwango cha mafuta katika mishipa ya damu na kuiwezesha kupeleka damu ya kutosha katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo uume.

Jitahidi kutumia vinywaji na vyakula visivyokuwa na sukari nyingi.

Epuka vinywaji vyote vyenye sukari nyingi kwani ni adui mkubwa sana wa afya yako hasa wakati unataka kurudisha nguvu za kiume. Kula vyakula asili na nafaka ambayo haijakobolewa, kula matunda kwa wingi pamoja na mboga za majani. Utafurahia maisha ya kula vyakula asili na utakuwa imara katika tendo la ndoa.

Epukana na msongo wa mawazo.

Ufanyaji wa tendo la ndoa huwa unahusisha mambo mengi. Unaweza ukawa umekamilika kiafya lakini ukashindwa kufanya mapenzi kwa kuwa una msongo wa mawazo. Hakikisha kabla ya kwenda faragha na mpenzi wako, unauituliza akili na usiwaze mambo mengine nje ya tendo linaloenda kufanyika. Hii itakupa muda mzuri wa ubongo wako kupeleka damu ya kutosha katika uume.

Rudisha virutubisho ambavyo vimepotea mwilini mwako.

Hakikisha mwili wako unaupa madini ya msingi kama zinki, chuma, selenium, manganese na vitamin nyingi, kwani madini haya ndiyo yanafanya mwili wako ufanye kazi katika kiwango stahiki. Madni haya huwezesha viendesha shughuli za mwili yani enzymes kufanya kazi katika kiwango kizuri na kuimarisha mwili wako. Madini haya hupatikana katika mboga, samaki na matunda ya aina mbalimbali.

Kunywa maji ya kutosha kila siku.

Kunywa maji ya kutosha kila siku, usingoje mpaka kiu ikupate. Mtu mzima anapaswa kunywa maji glass 8 mpaka 10 kwa siku. Maji husaidia kuongeza kiwango cha damu na kuondoa sumu mbalimbali mwilini.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Mambo ya Msingi kujua kuhusu rangi ya mkojo wako

Mambo ya Msingi kujua kuhusu rangi ya mkojo wako

Je unafahamu ya kwamba rangi ya mkoja inakupa matokea sahihi kuhusu afya yako? Kama jibu ni hapan... Read More

Faida 14 za kufunga chakula

Faida 14 za kufunga chakula

Watu wengi wanafahamu kuwa kufunga kula ni swala linalohusiana na imani zaidi. Wengi hawafahamu k... Read More

Mambo ya Muhimu kufahamu kuhusu tatizo la mgongo wazi

Mambo ya Muhimu kufahamu kuhusu tatizo la mgongo wazi

Uti wa mgongo ulio wazi( Spinal bifida) ni hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku uti wa mgongo (m... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia tango

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia tango

Tango ni tunda na ni mboga pia na ni chanzo kizuri cha potasiamu na vitamini nyingi ambazo zina k... Read More

Dondoo muhimu za afya

Dondoo muhimu za afya

Tafadhali soma na uwapelekee wengine.

Dr. Chriss Mosby wa Tanzania amegundua kensa mpya kwa... Read More

Fahamu kuhusu kitambi na uzito uliopitiliza

Fahamu kuhusu kitambi na uzito uliopitiliza

Mwili wa binadamu umeundwa kwa organs na mifumo mbalimbali ili kuuwezesha kufanya kazi sawia. Mfa... Read More

Dondoo kuhusu tezi dume

Dondoo kuhusu tezi dume

Tezi dume kila mwanaume anazaliwa nayo ambayo inasaidia kutoa maji maji ambayo yanaweza kusaidia ... Read More

Sababu na tiba ya tatizo la kukoroma usiku: Kukoroma unapolala

Sababu na tiba ya tatizo la kukoroma usiku: Kukoroma unapolala

Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila ... Read More
Kutibu chunusi kwa ute mweupe wa yai

Kutibu chunusi kwa ute mweupe wa yai

Hii inaweza kuchukuliwa kama njia rahisi na isiyo na gharma katika kutibu chunusi. Kwa mjibu wa ... Read More

Dondoo muhimu kwa Afya yako unapostuka usiku

Dondoo muhimu kwa Afya yako unapostuka usiku

Kumekuwepo na tatizo la vifo vya ghafla sana tena kwa watu ambao wana afya njema na hii inatokana... Read More

Njia za kutibu shinikizo la chini la damu au presha ya kushuka

Njia za kutibu shinikizo la chini la damu au presha ya kushuka

πŸ‘‰Kutibu shinikizo la chini la damu kwa kutumia maji chum... Read More

Athari za Moshi wa sigara kwa mtoto

Athari za Moshi wa sigara kwa mtoto

Utafiti uliofanyika nchini Marekani umebaini kwamba watu wazima wasiovuta sigara lakini walipokuw... Read More

πŸ“– Explore More Articles