Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua.
Nini husababisha.
Tatizo ili mara nyingi husababishwa na huambatana na mambo yafuatayo:
1. Kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo huchelewesha tumbo kufunguka kwa ajili ya usagaji wa chakula.
2. Kunywa vinywaji vyenye Carbonates, cola na kula vyakula vyenye gesi kama maharage, bigiji, vitunguu, kabichi n.k
3. Msongo wa mawazo na hasira.
4. Kula haraka haraka na kula unaongea.
5. Uvutaji wa Sigara
6. Magonjwa na maambukizi katika mfumo wa chakula asa kwenye tumbo na utumbo ambayo huzuia kusagwa na kufyonzwa kwa chakula.
Jinsi ya kujitibu.
· Kunywa chai ya tangawizi au karafuu itasaidia kupunguza gesi.
· Unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya Limao baada ya kula.
· Tafuna mbegu za maboga zinasaidia kulainisha mfumo wa chakula
· Lalia ubavu wa kushoto na pumua kwa kasi ili kupunguza gesi tumboni.
· Kunja miguu na ikalie uku ukinyoosha mikono na kuinamia mbele itasaidia.
· kuongeza kasi ya mfumo wa chakula kufanya kazi na kuondoa gesi.
· Fanya mazoezi mepesi ya kutembea na kuruka ruka.
· Kula na tafuna chakula taratibu na epuka vyakula vyenye gesi na mafuta mengi,.
· Nenda hospitali kama tatizo ili linaambatana na kuharisha, kutapika, maumivu makali ya tumbo, kinyesi chenye rangi tofauti au damu na maumivu ya kifua.
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
1.Usichelewe kwenda HAJA. Kutunza mkojo kweye kibofu chako kwa muda mrefu ni wazo ...
Read More
Dawa nyingine madhubuti ya chunusi ni papai. Tunda hili ni moja ya matunda yanayotumika kwa ajili...
Read More
Kumekuwepo na tatizo la vifo vya ghafla sana tena kwa watu ambao wana afya njema na hii inatokana...
Read More
Mchanganyiko wa mdalasini na asali unasaidia katika mambo ya aiana tofauti tofauti kama ifutavto:...
Read More
Tezi dume kila mwanaume anazaliwa nayo ambayo inasaidia kutoa maji maji ambayo yanaweza kusaidia ...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!