Tatizo la maumivu wakati na baada ya kufanya mapenzi
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Wakati wa kufanya tendo la ndoa wapo baadhi ya watu hupatwa na maumivu wakati au baada ya kushiriki tendo, Maumivu haya yaweza kuwa;- Wakati tu uume unaingia,
Unapoingiza kitu chochote hata kidole, Wakati uume ukiwa ndani na Maumivu ya kupita (throbbing pain) yanayodumu masaa kadhaa baada ya tendo.
Sababu za maumivu
Sababu zaweza kuwa za kimwili (physical) au za kisaikolojia.
Sababu za kimwili baadhi ni kama;
Kutokua na ute wa kutosha kwa ajili ya kulainisha uke kutokana na kukosa maandalizi ya kutosha, kupungua kwa homoni baada ya ukomo wa hedhi, kujifungua au kunyonyesha, baadhi ya dawa za magonjwa ya akili, presha na uzazi wa mpango.
Ajali au upasuaji maeneo ya nyonga, ukeketaji na kuongezewa njia wakati wa kujifungua. Pia matibabu ya kutumia mionzi eneo la nyonga.
Tatizo la mishipa ya uke kusinyaa yenyewe (Vaginismus).
Tatizo la uumbaji linalopelekea mtu kuzaliwa wakati uke haujatengenezwa vizuri mfano “vaginal agenesis na imperforate hymen.”
Magonjwa ya kizazi kama “endometriosis, PID,fibroids.”
Sababu za kisaikolojia;
Msongo wa mawazo, wasiwasi, sonona, matatizo ya mahusiano, woga wa mimba, historia ya kuumizwa kimapenzi (sexual abuse) siku za nyuma.
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Tatizo hili huwakumba watu wengi sana kwenye jamii yetu lakini kwa bahati mbaya watu wengi huchuk...
Read More
Mchanganyiko wa chumvi na mafuta ya zeituni (olive oil) ni dawa nyingine inayotibu chunusi. Mafut...
Read More
UNYWAJI wa maji baridi, hasa katika joto kali kama la Dar es Salaam, ni kiburudisho kikubwa cha k...
Read More
☘☘piga chini kitambi☘☘
Mahitaji
🌹Tikiti🍉 1
🌹Tangawizi kid...
Read More
Uti wa mgongo ulio wazi( Spinal bifida) ni hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku uti wa mgongo (m...
Read More
Kunywa Maji yenye chumvi husaidia kutibu shinikizo la chini la damu sababu sodiamu iliyomo kweny...
Read More
Vifaa vya kieletroniki
Vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa ...
Read More
Juisi hii ni nzuri sana katika kutibu shinikizo la juu la damu.
Lakini inaweza pia kutumika...
Read More
Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wak...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!