Dalili na matibabu ya tatizo la upungufu wa damu
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Upungufu wa damu ni tatizo linalosababishwa na kupoteza damu nyingi, kupungua kwa uzalishaji wa chembe hai za da damu na uharibifu wa chembe za damu kutokana na matatizo na magonjwa mbali mbali seli mundu, ujauzito, hedhi nzito, kurithi, magonjwa sugu na Lishe duni yenye ukosefu wa madini ya folic, chuma na vitamini B12.
Dalili
Dalili zifuatazo zinakuwezesha kutambua kama una tatizo la upungufu wa damu hivyo kukusaidia kuwahi hospitali au kubadili mfumo wa chakula ili kuepuka madhara makubwa ya baadae.
· Kushindwa kupumua vizuri
· Vidonda kwenye ulimi au mdomoni
· Sehemu nyeupe ya jicho kuwa bluu
· Ngozi kuwa na rangi ya kijivu
· Kucha kuwa dhaifu
· Kusikia hasira na kuhamasika haraka
· Kuchoka sana kuliko kawaida
· Maumivu makali ya kichwa
· Kupungua kwa uwezo wa kufikiria
· Kusikia kichwa chepesi pale unaposimama
· Miguu na mikono kuwa ya baridi sana
· Uchovu wa mara kwa mara
Matibabu.
Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya Chuma kutokana na visababishi vya tatizo. Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizi huweza kutumika hosipitali na matibabu ya tatizo linalosababisha na iwapo mgonjwa yuko katika hali mahututi huweza kuongezewa damu.
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Ulaji wa vyakula vingi vya wanga na mafuta ni chanzo kikubwa cha unene na uzito kuongezeka. Vyaku...
Read More
Huzuia na kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu
Wakati mafuta ya nazi yakiwa yamemeng’en...
Read More
Mshubiri au Aloe Vera kama ilivyozoeleka na namna nzuri kwa wale wote wanaotaka kubaki na ngozi ...
Read More
Wapo baadhi ya watu wanashindwa hata kuachia kicheko chenye bashasha hii ni kwa sababu meno yao y...
Read More
Asilimia kubwa tunapenda kutumia karoti katika kuunga katika mboga ya nyama na si kuila karoti ka...
Read More
Hypotension ndio jina linalotumika kuelezea presha ya kushuka ambayo mpaka sasa chanzo chake hakijaw...
Read More
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na kuathiri afya zao kw...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!