Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Madhara ya kuwa mnene kupindukia

Featured Image
Unene(obesity), ni ugonjwa unaokua kwa kasi kipindi hiki ukiambatana na madhara makubwa kiafya hata vifo. Unene hupimwa kwa kutumia kipimo kinachotambulika kitaalamu kama BMI (yaani uzito kwa Kilogram kugawa kwa urefu kwa mita mara mbili). Tatizo la unene uliopindukia huweza kusababisha mhusika kutengwa katika jamii, kubaguliwa, kudhihakiwa hata kunyanyapaliwa hivyo kuleta madhara kisaikologia kwa mgonjwa. Sababu za unene uliopindukia ni pamoja na kurithi. Mtoto aliyezaliwa na wazazi wanene, ana asilimia 80 ya kuwa mnene, aliyezaliwa na wazazi wembamba, ana asilimia 10 ya kuwa mnene. Utamaduni na ukosefu wa nidhamu katika vyakula, pia unachangia unene uliopindukia. Mfano; kuna ongezeko kubwa la watoto na vijana wanene kwa sasa mijini kuliko vijijini. Madhara yaletwayo na unene uliopindukia ni mengi, lakini kwa uchache ni pamoja na kulika kwa jointi hasa za miguu, maumivu kiunoni na katika nyonga, shinikizo la damu, kisukari, pia kukosa usingizi kutokana na kubanwa kwa hewa. Mengine ni athma, kiungulia, mafuta mengi mwilini, magonjwa ya moyo na moyo kushidwa kufanya kazi na mawe katika kibofu cha nyongo. Wagonjwa hujikuta wakishindwa kufanyakazi vyema ili kujipatia kipato, hivyo kuwa tegemezi, kunyanyapaliwa pia huleta matatizo ya kisaikologia kama nilivyoeleza awali. Matibabu ya ugonjwa huu ni pamoja na kubadili mfumo na aina ya maisha. Hii ni pamoja na kuwa na nidhamu katika chakula na kufanya mazoezi. Ni wazi kwamba wazazi na watoto wanaoishi mjini, wanakabiliwa na tatizo hili, kutokana na maisha ya mfumo mgando ( kula kazi bila jasho-kulala, au kula-kusoma-kulala). Matibabu ya muda mrefu ya tatizo hili na ambayo husaidia mgonjwa kwa kiwango kikubwa ni kufanyiwa upasuaji. Upasuaji katika tumbo ndiyo tiba mwafaka kwa unene uliopindukia.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Namna ya kutibu chunusi kwa kutumia asprin

Namna ya kutibu chunusi kwa kutumia asprin

Aspirin inaweza kuwa ni moja ya dawa nzuri za chunusi. Chukua vidonge viwili au vitatu vya aspir... Read More

Mambo usiyoyajua kuhusu ugonjwa wa Pumu

Mambo usiyoyajua kuhusu ugonjwa wa Pumu

Asthma /pumu ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia ya hewa ambazo huingiza na kutoa hewa katika mapafu... Read More
Jinsi ya kutibu tatizo la kukosa choo bila kutumia dawa

Jinsi ya kutibu tatizo la kukosa choo bila kutumia dawa

Kukosa choo ni tatizo kubwa katika jamii zetu japo huwa halionekani kama ni tatizo. Hata hivyo ku... Read More

Faida za matumizi ya Ukwaju kiafya

Faida za matumizi ya Ukwaju kiafya

Faida kuu za ukwaju ni kama ifuatavyo:

Huondoa sumu Mwilini

Chanzo kizuri cha viua ... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia Mtindi na asali

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia Mtindi na asali

Kutumia mtindi na asali ni moja ya dawa rahisi zaidi za kutibu chunusi.

Unahitaji:

... Read More

Matumizi ya maji kutibu shinikizo la chini la damu

Matumizi ya maji kutibu shinikizo la chini la damu

Matumizi ya maji ya kunywa ni moja ya dawa rahisi kabisa ya shinikizo la chini la damu.

Hii... Read More

Mambo ya Muhimu kuyajua kuhusu maumivu ya Korodani

Mambo ya Muhimu kuyajua kuhusu maumivu ya Korodani

Kuna wakati mwanaume huweza kupata maumivu ya korodani, ambapo inawezekana ikawa ni maumivu kwa k... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa Chumvi na mafuta ya zeituni

Jinsi ya kutibu chunusi kwa Chumvi na mafuta ya zeituni

Mchanganyiko wa chumvi na mafuta ya zeituni (olive oil) ni dawa nyingine inayotibu chunusi. Mafut... Read More

Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

Tezi Dume ni nini?