Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Mapenzi salama ni yapi?

Featured Image

Mapenzi salama ni yale yanayofanyika bila wasiwasi wa kupata mimba zisizotarajiwa, magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Mapenzi salama yanaweza kuwa ni vitendo vya kumaliza hamu bila uume kuingizwa ukeni. Ngono ya kuingiza uume ukeni inaweza kuwa ngono salama kama tahadhari husika zinatumika.
Vitendo vya kumaliza hamu bila kujamiiana ni kupiga busu, kukumbatia, kunyonyana ndimi, kushikana mikono na kupiga punyeto. Matendo haya yote ni salama kabisa kuhusiana na mimba zisizotarajiwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Ili kuhakikisha mnafanya mapenzi salama wakati mnahusisha mwingiliano kati ya uume na uke, lazima mchukue tahadhari. Tahadhari mojawapo ni uaminifu katika mapenzi, kwa maana wewe uwe mwaminifu na yeye awe mwaminifu. Lakini pia inabidi muwe na uhakika kwamba wote wawili hamjaambukizwa magonjwa wakati mnapojamiiana kwa mara ya kwanza. Tahadhari nyingine ni kutumia kondomu. Kondomu inazuia mimba pamoja na magonjwa ya zinaa. Kuwa mwaminifu pekee yake haitoshi kama mmoja wenu au wote wawili mliwahi kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi ambao haukuwa salama. Kama kweli mnataka kuwa upande wa uhakika wote ni vyema kwenda kupima Virusi vya Ukimwi kwa hiari.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, kuna tofauti za umri katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za umri katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za umri katika ngono/kufanya mapenzi? Ndio, kuna tofauti nyingi sana! Hiyo ndiyo... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Mazungumzo ya Kina na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Mazungumzo ya Kina na Msichana

Kama kijana, kuna wakati unaweza kukutana na msichana na unataka kuzungumza naye kwa kina lakini ... Read More

Jinsi ya Kuwa na Muda Mzuri na Msichana Bila Kutumia Fedha Nyingi

Jinsi ya Kuwa na Muda Mzuri na Msichana Bila Kutumia Fedha Nyingi

Kutumia fedha nyingi kupata muda mzuri na msichana siyo lazima. Kuna njia nyingi za kuwa na muda ... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili matakwa ya kujamiiana na ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kujadili matakwa ya kujamiiana na ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Habari wapendwa wasomaji, leo tutaangazia swali muhimu sana ambalo wapenzi wengi hujiuliza. Je, k... Read More

Kwa nini kuna Watanzania wanaovuta bangi?

Kwa nini kuna Watanzania wanaovuta bangi?

Sababu mojawapo ni kuwa bangi hulimwa hapa nchini na
hivyo hupatikana kwa urahisi. Bangi huu... Read More

Njia za Kujenga Uhusiano Imara na Msichana

Njia za Kujenga Uhusiano Imara na Msichana

Kujenga uhusiano na msichana ni jambo muhimu katika maisha ya kimapenzi. Uhusiano unapokuwa imara... Read More

Je, ni tabia zipi zinazochangia kuenea kwa virusi vya UKIMWI?

Je, ni tabia zipi zinazochangia kuenea kwa virusi vya UKIMWI?

Virusi vya UKIMWI kwa kiasi kikubwa vinaenea kwa njia ya kujamii ana. Kama mtu ana wapenzi wengi ... Read More

Unyanyasaji wa kijinsia

Unyanyasaji wa kijinsia

Kuna aina nyingi za unyanyasaji wa jinsia na unaweza kutokea kwa wote wanaume na wanawake. Kwa kawai... Read More
Kulambana sehemu za siri ni salama kiafya? Je, tendo hili ni la kawaida?

Kulambana sehemu za siri ni salama kiafya? Je, tendo hili ni la kawaida?

Si rahisi kusema ni kitendo kipi kilicho cha kawaida na kisicho cha kawaida. Kulamba ni jambo linalo... Read More
Je, Tanzania kuna Albino wangapi?

Je, Tanzania kuna Albino wangapi?

Idadi kamili ya Albino Tanzania haijulikani kwani hakuna
aliyewahesabu. Inakisiwa kufuatana ... Read More

Je, uke wa mwanamke unaweza kupanuka kiasi gani?

Je, uke wa mwanamke unaweza kupanuka kiasi gani?

Wakati wa kujifungua, uke wa mwanamke mzima hupanuka kuanzia kipenyo cha sentimeta kumi mpaka kum... Read More

Jinsi ya Kuonyesha Heshima kwa Msichana Wako

Jinsi ya Kuonyesha Heshima kwa Msichana Wako

Jinsi ya Kuonyesha Heshima kwa Msichana Wako

Wanawake ni vipenzi vya thamani sana katika m... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About