Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?
Date: April 17, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Kuchagua mchumba ni moja ya maamuzi ambayo kijana anahitaji kuyafanya kwa uangalifu mkubwa sana. Kwa sababu huyo ndiye atakayekuwa mwenzi wake wa maisha. Katika kuchagua mchumba kila mtu ana mawazo yake kuhusiana na kilicho muhimu kuzingatiwa. Mara nyingi mhemuko una nguvu zaidi kuliko uamuzi wa kimantiki
Hata hivyo, vifuatavyo ni kati ya vigezo ambavyo vinaweza kuangaliwa:
β’ Chagua mtu anayekuheshimu wewe na wengine; Chagua mtu unayemwamini;
β’ Chagua mtu ambaye unaweza kuongea, kujadiliana, na kuhojiana naye kwa uwazi bila kugombana;
β’ Chagua mtu mwenye umri unaokaribiana na wa kwako;
β’ Chagua mtu anayependelea vile unavyopendelea;
β’ Chagua mtu ambaye ataelewa matatizo yako na yuko tayari kukusaidia kuyatatua; na
β’ Chagua mtu mwenye afya nzuri.
Hii inamaanisha pia kumpata mtu ambaye kabla ya kuanza kujaamiana naye, atakuwa tayari kwenda kupima kwa hiari kujua hali yake ya VVU na pia kuwa tayari kutumia kinga kwa maana ya kondomu hadi hapo mtakapojua hali zenu.
Wafahamishe wazazi wako mtu uliyemchagua kama mchumba na mtambulishe kwao i ili wamfahamu na yeye awafahamu wazazi wako. Wakati huohuo na wewe jaribu kuwafahamu wazazi wake. Usifanye uchumba wa haraka. Pata muda wa kutosha kumwelewa rafiki yako.
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Mwanamke ni hazina kubwa katika maisha ya kila mwanaume. Ni kiumbe chenye thamani, cha thabiti na...
Read More
Lengo kuu la kujamiiana ni kutafuta watoto. Lakini si sababu pekee. Sababu hizo ni pamoja na;
...
Read More
Habari za leo wapenzi wangu! Nami nina furaha sana kuwa hapa leo kuongelea kuhusu swala la ngono ...
Read More
Kwa vile Albino hana tofauti na watu wengine inopokuja
kwenye suala la idadi ya watoto wa ku...
Read More
Kumwonyesha shukrani msichana wako ni njia moja ya kumfanya ajisikie muhimu na kupendwa. Kwa hiyo...
Read More
Ukishatambua kwamba una mimba kuna mambo mbalimbali tofauti ya kufanya. Kwanza kabisa mweleze mwe...
Read More
Ni kweli hiyo ni dhuluma na inaitwa unyanyasaji wa kijinsia kwa
mtoto. Watoto wanaweza kusha...
Read More
Je, ngono/kufanya mapenzi ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kimapenzi?
Kwa wengi, kufanya ma...
Read More
Sheria ya Tanzania inaeleza dawa zilizo halali na zisizo halali.
Tumbaku imekubalika na jami...
Read More
Si kweli kabisa! Baada ya kuvuta bangi mtu hujiona kama jasiri sana na mwenye nguvu. Lakini madha...
Read More
Je, kuna haja ya kuzungumzia historia ya ngono/kufanya mapenzi ya kila mmoja katika uhusiano? Jib...
Read More
Mawasiliano mazuri ya ana kwa ana na msichana ni muhimu sana katika uhusiano wowote. Ni njia bora...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!