Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Mambo ya msingi kwa mwanamke kuyajua unapojiremba

Featured Image
Kope nazo humpendezesha mwanamke kuna aina ya rangi za kupaka kwenye kope, lakini zinatofautiana. Ni vyema ukawasiliana na wataalamu wa mambo ya urembo kwa ushauri na siyo kukurupuka. Siyo umemuona fulani kapendeza na aina fulani ya rangi ya kwenye kope halafu na wewe ukakimbilia kupaka, utachekesha. Rangi ya mdomo nayo ni eneo lingine linalompendezesha mwanamke. Ukweli ni kwamba tunatofautiana sana midomo wazungu wanaita โ€˜Lipsโ€™ Kila mwanamke ana tofautiana midomo na mwingine kwa hiyo hata rangi ya midomo nayo inakwenda sambambana aina ya lips na rangi ya ngozi ya mwili aliyo nayo mwanamke, siyo unajisiriba rangi ya mdomo halafu unaonekana kituko. Wasiliana na wataalamu wa urembo kwa ushauri zaidi. Kucha kwa wanawake ni eneo lingine linolatakiwa kuwekwa katika unadhifu. Kuna baadhi ya wanawake unaweza kukutana nao kucha zao zimelika aidha kwa kung'atwa au kwa kuliwa na fangasi. Ni vyema wanawake wenye tatizo hilo kumuona mtaalamu wa ngozi kwa msaada wa tiba. Unaweza kukutana na mwanamke kucha zake zimelika na zina sharp edges kiasi kwamba akikugusa utadhani umeguswa na msasa. Au akishika Glasi ya Kinywaji ukiangalia kucha utadhani mkono ni wa mwanaume maana kwa jinsi kucha zake zilivyo hata hafanani nazo. Kuna kucha za bandia kama mwanamke ana matatizo ya kucha basi akazinunue kusitiri aibu. Marashi, manukato au unyunyu kama wanavyoita vijana wa mjini ni muhimu kwa wanawake lakini ni vyema nikaweka angalizo. Haipendezi kwa mwanamke anayepulizia manukato yanayonukia sana mpaka yakawakera wengine ni vyema wanawake wakajipulizia marashi yenye staha na yasiyokera. Ngozi ya mwanamke ni bora โ€˜sensitiveโ€™ sana na inaakiwa ipakwe aina ya mafuta au lotion yenye virutubisho kulingana na aina ya Ngozi. Kuna wanawake wenye Ngozi ya mafuta โ€˜Oil Skinโ€™ kuna wenye Ngozi mchanganyiko na kuna wale wenye ngozi kavu (Dry Skin). Ni vyema mwanamke kujua aina ya ngozi yake ili ajie aina ya product ya ngozi anayopaswa kutumia na siyo kwa sababu umemuona mwenzio anapaka aina fulani ya losheni na wewe unakimbilia kununua. Omba ushauri kwa wataalamu wa ngozi watakusaidia. Kuna baadhi ya maduka yanyouza vipodozi wanatoa msaada huo bure kabisa.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuvaa hereni kwa Mpangilio kuongeza Mvuto wako

Jinsi ya Kuvaa hereni kwa Mpangilio kuongeza Mvuto wako

HERENI ni pambo linavoliwa masikioni na kwa kiasi kikubwa linachangia kuongeza mvuto na muonekano... Read More

Namna ndizi inavyotumika katika urembo

Namna ndizi inavyotumika katika urembo

Mbali na kulika, ndizi zina manufaa mengine, hasa katika urembo wa ngozi.
Ndizi zina virutub... Read More

Namna ya kuondoa Mikunjo ya ngozi

Namna ya kuondoa Mikunjo ya ngozi

MIKUNJO katika ngozi ni miongoni mwa matatizo yanayowakabili wanawake wengi.
Tofauti na miku... Read More

Tiba mbadala ya chunusi na vipele usoni

Tiba mbadala ya chunusi na vipele usoni

Kuna idadi kubwa ya watu wanao kabiliwa na tatizo la vipele vya usoni ( Chunusi ). Kuwa na chunus... Read More

Jinsi ya Kujiremba Macho

Jinsi ya Kujiremba Macho

Kuna urembo mbalimbali wa macho kulingana na taste ya mtu na mapendeleo yake . Leo nitazungumzia ... Read More

Madhara ya Kujichubua

Madhara ya Kujichubua

Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwez... Read More

Jinsi ya Kuondoa Makovu Mwilini

Jinsi ya Kuondoa Makovu Mwilini

Makovu sio kidonda naomba hili uelewe, ila makovu ni alama ya majeraha ambayo yamebaki kwenye ngo... Read More

Njia za kutunza nywele zako

Njia za kutunza nywele zako

Suala la kutunza nywele za asili wengi hutamani japokuwa ukweli kwamba kuna changamoto kadhaa, la... Read More

Namna nzuri ya kuhudumia nywele zako za asili kirahisi

Namna nzuri ya kuhudumia nywele zako za asili kirahisi

Kwa wale ambao tuna nywele asilia (natural hair), tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana ... Read More
Sababu, tiba na jinsi ya kujikinga na Tatizo la uke kutoa harufu

Sababu, tiba na jinsi ya kujikinga na Tatizo la uke kutoa harufu

Ni matumaini nyote mnaendelea vyema, nami alhamdulillah ala kul Hali naendelea vyema
Leo nao... Read More

Utengenezaji wa Makalio ni Hatari na Hutakiwi kufanya

Utengenezaji wa Makalio ni Hatari na Hutakiwi kufanya

Mwanamke wa miaka mitatu amefariki baada ya kuripotiwa kuelekea Uturuki kwa aina ya upasuaji kwa ... Read More

Mambo ya kuzingatia kama una ngozi yenye Mafuta

Mambo ya kuzingatia kama una ngozi yenye Mafuta

Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi ... Read More

๐Ÿ“– Explore More Articles
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About