Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha mume na mke

Featured Image

Mwanaume mmoja alimuoa mwanamke mrembo. Alikuwa akimpenda sana. Siku moja mwanamke alipatwa na maradhi ya ngozi. Kidogokidogo alianza kupoteza urembo wake.
.
.
.

Mume alipata safari na wakati akirudi alipata ajali iliyomfanya apoteze uwezo wake wa kuona. Hata hivyo, maisha yao ya ndoa yaliendelea kama kawaida. Lakini kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo mke alivyoendelea kupoteza urembo wake. Kwa kuwa mume alikuwa kipofu hakulijua hilo na hivyo hakuna kilichobadilika kwenye upendo wao. Aliendelea kumpenda, na mke alimpenda sana mumewe.
.
.
.

Siku moja mke alifariki dunia. Ilikuwa huzuni kubwa sana kwa mume.
Baada ya kumaliza taratibu zote za maziko, mazishi na kutandua msiba, alipanga kuhama kwenye mji huo na kwenda kuishi kwenye mji mwingine.
.
.
.

Mtu mmoja aliposikia habari hiyo alimwendea na kumuuliza: โ€œSasa utawezaje kutembea peke yako? Maana siku zote hizi mkeo alikuwa akikusaidia kukuonesha njia.โ€

Akajibu: โ€œMimi si kipofu. Nilifanya ionekane hivyo kwa sababu angejua kwamba ninauona mwili wake ulivyobadilika kuwa mbaya angepata maumivu makubwa zaidi kuliko ugonjwa wake wenyewe. Alikuwa mke mwema sana. Nilitaka aendelee kuwa na furaha.โ€
.
.
.

FUNZO:

Wakati fulani ni vizuri ukajifanya kipofu na kuyapuuza mapungufu ya mwenzako ili kumfanya awe mwenye furaha.

Meno huungโ€™ata ulimi mara nyingi, lakini vinaendelea kuishi pamoja kinywani. Huo ndio moyo wa KUSAMEHEANA. Macho hayaonani, lakini yanatazama na kuona vitu kwa pamoja, hupepesa na kulia pamoja. Huo unaitwa UMOJA.

1. Ukiwa peke yako unaweza kuongea, lakini ukiwa pamoja na mwenzako mnaweza KUZUNGUMZA.

2. Ukiwa peke yako unaweza KUFURAHI, lakini ukiwa na mwenzako unaweza KUFURAHIA.

3. Ukiwa peke yako unaweza KUTABASAMU, lakini ukiwa na mwenzako mnaweza KUCHEKA.

Huo ndio UZURI wa mahusiano yetu kama binadamu. Tunategemeana.

Kiwembe kina ukali lakini hakiwezi kukata mti; shoka lina nguvu na imara lakini haliwezi kukata nywele.

*Kila mtu ni muhimu kulingana na kusudio na lengo la uwepo wake. Usimdharau mtu yeyote kwa hali yoyote, kwa sababu huwezi kuwa yeye.

Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu na moyo wa kusamehe, kustahmiliana na kuishi kwa umoja.
.
Tafakari
Mm na ww tunaweza kufanya haya!!!

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke

Kitabu hiki niย Soft copy [pdf]ย kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Furaha na Kusudi katika Mahusiano yako

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Furaha na Kusudi katika Mahusiano yako

Mahusiano ni jambo muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Kujenga ushirikiano wenye furaha na ku... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Ukaribu wa Kihisia katika Mahusiano yako

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Ukaribu wa Kihisia katika Mahusiano yako

Mahusiano ni jambo muhimu sana katika maisha yetu na yanahitaji kipaumbele cha kujenga ukaribu wa... Read More

Jinsi ya Kujenga Maisha ya Ndoa yenye Furaha na Maana na mke wako

Jinsi ya Kujenga Maisha ya Ndoa yenye Furaha na Maana na mke wako

Kujenga maisha ya ndoa yenye furaha na maana na mke wako ni lengo kubwa ambalo linahitaji jitihada n... Read More
Kuunganisha Kufanya Mapenzi na Intimiteti: Kuleta Uhusiano wa Karibu zaidi

Kuunganisha Kufanya Mapenzi na Intimiteti: Kuleta Uhusiano wa Karibu zaidi

Hapana shaka, mapenzi na intimiteti ni sehemu muhimu ya uhusiano. Kuunganisha kufanya mapenzi na ... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kuishi kwa sasa na kuthamini maisha ya pamoja

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kuishi kwa sasa na kuthamini maisha ya pamoja

Kusaidiana na mpenzi wako katika kuishi kwa sasa na kuthamini maisha ya pamoja ni njia nzuri ya kuim... Read More
Jinsi ya Kuweka mipango ya likizo na mapumziko pamoja na mpenzi wako

Jinsi ya Kuweka mipango ya likizo na mapumziko pamoja na mpenzi wako

Kuweka mipango ya likizo na mapumziko pamoja na mpenzi wako ni njia nzuri ya kujenga uhusiano thabit... Read More
Jukumu la Kujielewa katika Kufanya Mapenzi: Kukuza Uhuru na Urahisi

Jukumu la Kujielewa katika Kufanya Mapenzi: Kukuza Uhuru na Urahisi

Mapenzi yana jukumu muhimu katika maisha ya mwanadamu. Ni kitendo cha kupenda na kuthamini mtu mw... Read More

Vidokezo vya Kufanya Msichana Aonekuwa Muhimu katika Maisha Yako

Vidokezo vya Kufanya Msichana Aonekuwa Muhimu katika Maisha Yako

Mwanamke ni hazina kubwa katika maisha ya kila mwanaume. Ni kiumbe chenye thamani, cha thabiti na... Read More

Kuhamasisha Uhuru na Kuunga Mkono Maendeleo ya Kibinafsi katika Mahusiano

Kuhamasisha Uhuru na Kuunga Mkono Maendeleo ya Kibinafsi katika Mahusiano

Kuhamasisha Uhuru na Kuunga Mkono Maendeleo ya Kibinafsi katika Mahusiano

Katika mahusiano... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Heshima na Uwazi katika Familia

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Heshima na Uwazi katika Familia

Kama unataka kuwa na familia yenye amani na furaha, mazungumzo ya heshima na uwazi ni muhimu sana... Read More

Kuhamasisha Utatuzi wa Migogoro kwa Amani na Furaha katika Familia

Kuhamasisha Utatuzi wa Migogoro kwa Amani na Furaha katika Familia

Kuhamasisha Utatuzi wa Migogoro kwa Amani na Furaha katika Familia

Migogoro kwenye familia... Read More

Jinsi ya Kuunganisha Kizazi: Kuweka Mipango na Kujenga Ushirikiano katika Familia

Jinsi ya Kuunganisha Kizazi: Kuweka Mipango na Kujenga Ushirikiano katika Familia

Kuunganisha kizazi ni muhimu sana katika familia. Ni jambo linalofanya familia iwe na nguvu na ku... Read More

๐Ÿ“– Explore More Articles
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About