Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Jinsi ya kumfanya mwanamke afurahi na akupende kwa kumfanyia mambo anayoyataka

Featured Image

Kuna mambo ya msingi ambayo mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanamme ili kufurahi na kutulia katika mahusiano japokuwa sio rahisi kukwambia mojakwa moja.

Mambo hayo ni kama ifuatavyo;

Kupewa nafasi na kipaumbele.

Wanawake wanapenda kuwa namba moja au kupendwa kuliko yeyote. Kumpenda mwanamke haikuishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Wanawake wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla na katika maisha yao.

ย 

Kuheshimiwa

Wanawake wanapenda kueshimiwa kwa maneno na matendo. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya. Wanawake hawapendi kukosewa heshima hasa mbele za watu, hata kama ni kwa mambo madogo madogo.

Kuridhishwa Kwenye tendo la ndoa

Mwanamke anapenda aridhishwe Kwenye tendo la ndoa. Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Utundu na ufundi unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo.

ย 

Nafasi ya kuongea na kujieleza

Wanawake wanapenda wapewe nafasi ya kuongea na kujieleza vile watakavyo. Mpe uhuru mpenzi wako kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali pale anapoongea sana. Kwa kawaida wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, wakati wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa hiyo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao.

ย 

Kusaidiwa katika shida na matatizo yao

Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.

Kubembelezwa

Wanawake hupenda kubembelezwa hasa pale wanapokuwa na huzuni. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa. Wanawake hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa.

Mfahamu zaidi Mwanamke kwa Kupitia Kitabu hiki kizuri cha SIRI ZA MWANAMKE
[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kuhamasisha Ushirikiano na Maendeleo ya Kibinafsi katika Mahusiano yako

Kuhamasisha Ushirikiano na Maendeleo ya Kibinafsi katika Mahusiano yako

Mahusiano ni jambo muhimu sana katika maisha yetu, hasa yale ya kimapenzi. Ndio maana ni muhimu s... Read More

Vidokezo vya Kufanya Msichana Aonekuwa Muhimu katika Maisha Yako

Vidokezo vya Kufanya Msichana Aonekuwa Muhimu katika Maisha Yako

Mwanamke ni hazina kubwa katika maisha ya kila mwanaume. Ni kiumbe chenye thamani, cha thabiti na... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu mipango ya kujitolea na kutoa msaada

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu mipango ya kujitolea na kutoa msaada

Leo tutaangalia jinsi ya kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu mipango ya kujitolea na kutoa msaada. ... Read More

Ulinzi wa Kinga: Je, Matumizi ya Kinga ni Jambo la Lazima?

Ulinzi wa Kinga: Je, Matumizi ya Kinga ni Jambo la Lazima?

Karibu kwenye makala hii kuhusu ulinzi wa kinga na umuhimu wake. Kila siku tunajikuta tukiwa kati... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kuunga Mkono Ndoto za Mwenzi wako

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kuunga Mkono Ndoto za Mwenzi wako

Mwenzi wako ni rafiki yako wa karibu na mtu anayekuaminu sana. Kwa hivyo, ni muhimu kuwa na ushir... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano ya Wazi na Msichana Wako

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano ya Wazi na Msichana Wako

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano ya Wazi na Msichana Wako

Ndoa ni muunganiko wa wawili kuwa ki... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Ushirikiano wa Kujenga na Kuunga Mkono Ndoto za Familia

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Ushirikiano wa Kujenga na Kuunga Mkono Ndoto za Familia

Kujenga ushirikiano wa familia ni jambo muhimu sana katika maisha. Kuweka kipaumbele cha kujenga ... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha usawa wa kijinsia na haki za wanawake

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha usawa wa kijinsia na haki za wanawake

Wapendwa wangu, katika ulimwengu wa leo, ni muhimu sana kujenga na kudumisha usawa wa kijinsia na... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujifunza na Kukuza Maarifa katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujifunza na Kukuza Maarifa katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujifunza na Kukuza Maarifa katika Familia

Familia ni kitovu ch... Read More

Kujenga Ushirikiano na Kusawazisha Majukumu katika Mahusiano ya Ndoa

Kujenga Ushirikiano na Kusawazisha Majukumu katika Mahusiano ya Ndoa

Kujenga Ushirikiano na Kusawazisha Majukumu katika Mahusiano ya Ndoa

Ndoa ni muhimu sana k... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu matarajio ya baadaye na ndoto za kibinafsi

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu matarajio ya baadaye na ndoto za kibinafsi

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu matarajio ya baadaye na ndoto za kibinafsi ni muhimu katika kujeng... Read More
Kujenga Ushirikiano wenye Uaminifu na Kujenga Imani katika Familia

Kujenga Ushirikiano wenye Uaminifu na Kujenga Imani katika Familia

Kujenga Ushirikiano Wenye Uaminifu na Kujenga Imani katika Familia

Familia ni moja ya vitu... Read More

๐Ÿ“– Explore More Articles
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About