Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Familia: Kuhamasisha Haki na Uadilifu

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Familia: Kuhamasisha Haki na Uadilifu

Leo nataka kuzungumzia juu ya suala la kukabiliana na mazoea ya kukosa usawa katika familia na ku... Read More

Jinsi ya Kuweka Malengo ya Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kuweka Malengo ya Ndoa na mke wako

Kuweka malengo ya ndoa na mke wako ni hatua muhimu katika kujenga msingi imara na kufikia furaha na ... Read More
Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Mipango ya Pamoja katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Mipango ya Pamoja katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Mipango ya Pamoja katika Familia

Katika famil... Read More

Kujenga Mazoea ya Kujali na Kuthamini ili Familia Iwe na Amani na Furaha

Kujenga Mazoea ya Kujali na Kuthamini ili Familia Iwe na Amani na Furaha

Habari za leo wapendwa wasomaji. Leo tutajifunza kuhusu jinsi ya kujenga mazoea ya kujali na kuth... Read More

Kujenga Ushirikiano wenye Mipaka na Heshima katika Mahusiano

Kujenga Ushirikiano wenye Mipaka na Heshima katika Mahusiano

Kujenga Ushirikiano wenye Mipaka na Heshima katika Mahusiano

Kutafuta mtu ambaye tutaweza ... Read More

Mipaka katika Uhusiano wa Kufanya Mapenzi: Kuweka na Kuzingatia Mahitaji Yako

Mipaka katika Uhusiano wa Kufanya Mapenzi: Kuweka na Kuzingatia Mahitaji Yako

Mipaka katika Uhusiano wa Kufanya Mapenzi: Kuweka na Kuzingatia Mahitaji Yako

Katika mahus... Read More

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kutoelewana na Kukosa Ufahamu katika Familia

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kutoelewana na Kukosa Ufahamu katika Familia

Leo tutazungumzia kuhusu njia za kupunguza mazoea ya kutoelewana na kukosa ufahamu katika familia... Read More

Jinsi ya Kusaidia katika Mipango ya Matarajio na Miradi ya mke wako

Jinsi ya Kusaidia katika Mipango ya Matarajio na Miradi ya mke wako

Kusaidia katika mipango ya matarajio na miradi ya mke wako ni muhimu sana katika kujenga uhusiano we... Read More
Ishara 10 za mwanamke aliyekuzimia na anayekupanda

Ishara 10 za mwanamke aliyekuzimia na anayekupanda

Ishara hizi zinaweza zikakusaidia kumgundua msichana anayekupenda, wasichana wanatofautiana ila w... Read More

Jinsi ya Kujenga Uaminifu katika Familia: Kuheshimu na Kutimiza Ahadi

Jinsi ya Kujenga Uaminifu katika Familia: Kuheshimu na Kutimiza Ahadi

Leo, tutajadili jinsi ya kujenga uaminifu katika familia kwa njia ya kuheshimu na kutimiza ahadi.... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kusawazisha Maisha ya Kazi na Maisha ya Familia katika Mahusiano

Kuweka Kipaumbele cha Kusawazisha Maisha ya Kazi na Maisha ya Familia katika Mahusiano

Leo hii, tunazungumza juu ya suala muhimu sana katika maisha yetu - jinsi ya kuweka kipaumbele ch... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha afya ya kimwili na akili

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha afya ya kimwili na akili

Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha afya ya kimwili na akili ni jambo muhimu kat... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About