Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.

UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Je, kuna tofauti ya kiumri katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti ya kiumri katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti ya kiumri katika ngono/kufanya mapenzi? Ndio! Kuna tofauti kubwa sana kati ya wa... Read More

Njia za Kujenga Urafiki Mzuri na Msichana Kabla ya Kuwa na Uhusiano

Njia za Kujenga Urafiki Mzuri na Msichana Kabla ya Kuwa na Uhusiano

Karibu ndugu yangu kwenye makala hii ambao inazungumzia njia mbalimbali ambazo utaweza kutumia ku... Read More

Jinsi ya Kujenga Mazingira ya Kimapenzi Kabla ya Kufanya Mapenzi

Jinsi ya Kujenga Mazingira ya Kimapenzi Kabla ya Kufanya Mapenzi

Mapenzi ni muhimu katika maisha ya kila mtu. Lakini, ili uweze kuwa na mapenzi yasiyo ya kawaida ... Read More

Kujenga Ushirikiano wenye Upendo na Kuunda Amani na Furaha katika Familia

Kujenga Ushirikiano wenye Upendo na Kuunda Amani na Furaha katika Familia

Kujenga ushirikiano wenye upendo na kuunda amani na furaha katika familia ni jambo muhimu sana ka... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya ujasusi na ulinzi wa taifa

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya ujasusi na ulinzi wa taifa

Mapenzi ni muhimu sana katika maisha yetu na yanatakiwa kulindwa kwa kila hali. Hata hivyo, kuna ... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kuendeleza Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano

Kuweka Kipaumbele cha Kuendeleza Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano

Kuweka Kipaumbele cha Kuendeleza Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano

Kuwa na mahusiano... Read More

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kutokuelewana na Kukosa Msamaha katika Familia Yako

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kutokuelewana na Kukosa Msamaha katika Familia Yako

Familia ni nguzo muhimu sana katika maisha yetu na tunapaswa kuilinda kwa gharama yoyote ile. Hat... Read More

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha mume na mke

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha mume na mke

Mwanaume mmoja alimuoa mwanamke mrembo. Alikuwa akimpenda sana. Siku moja mwanamke alipatwa na ma... Read More

Je, kuna tofauti za kimwili katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za kimwili katika ngono/kufanya mapenzi?

Mapenzi ni sehemu muhimu katika maisha ya binadamu na inaweza kuwa njia ya kujifunza, kufurahia, ... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Ukarimu na Upendo katika Familia yako

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Ukarimu na Upendo katika Familia yako

Familia ni muhimu sana katika maisha yetu. Ni mahali ambapo tunapata upendo, msaada, na faraja. N... Read More

Jinsi ya Kuwa Msaada kwa Mwenzi wako: Kujenga Ushirikiano na Kuunga Mkono Ndoto zao

Jinsi ya Kuwa Msaada kwa Mwenzi wako: Kujenga Ushirikiano na Kuunga Mkono Ndoto zao

Jinsi ya Kuwa Msaada kwa Mwenzi wako: Kujenga Ushirikiano na Kuunga Mkono Ndoto zao

Mpenzi... Read More

Mwanamme: Jinsi ya Kuwa na Ushirikiano na Jamii na Wanaume Wenzako

Mwanamme: Jinsi ya Kuwa na Ushirikiano na Jamii na Wanaume Wenzako

Read More
πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About