Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia asali
Welcome Back.
Updated at: 2024-05-25 10:34:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Asali hasa asali mbichi ya asili ni dawa nzuri sana ya kutibu chunusi. Asali ni antibiotiki ya asili ambayo husaidia kupunguza ukubwa wa chunusi na maumivu ya chunusi.
Asali inaweza pia kuzuia ngozi yako isipatwe na maambukizi mengine ambayo yangeweza kusababisha matatizo kwenye ngozi au makovu.
Hivyo asali inachukuliwa kama moja ya dawa za asili nzuri za kutibu chunusi unazotakiwa kuzijaribu.
Kwanza safisha ngozi yako vizuri na maji ya uvuguvugu kasha jipake asali moja kwa moja sehemu yenye chunusi. Iache kwenye ngozi kwa dakika 30 kisha jisafishe na maji safi ya uvuguvugu.
Updated at: 2024-05-25 10:35:27 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tezi dume (prostate), ni tezi iliyo kwenye kizazi cha mwanaume inayozalisha maji maji yanayobeba manii/shahawa. Inaizunguka urethra, mrija unaotoa mkojo kwenye kibofu kwenda nje. Tezi dume ya kila mwanaume huongezeka ukubwa kadri umri unavyoongezeka. Kadri tezi inapokua na kuongezeka ukubwa,inaweza kukandamiza urethra na kusababisha matatizo ya kibofu na matatizo ya kukojoa. Tezi dume inapoongezeka ukubwa huitwa ”benign prostatic hyperplasia” kwa kifupi ”BPH”. Hii sio saratani, na haiongezi hatari ya kupata saratani ya tezi dume.
Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na kansa kwa wanaume duniani. Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, satarani ya tezi dume kwa sasa inawapata sana wanaume kuanzia miaka 25. Lakini kabla ya kuendelea mbele hebu kwanza tujue tezi dume ni zipi.
Kama tulivyosema neno saratani ni jina la gonjwa ambalo hutokea wakati chembe chembe za uhai au seli katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili na kutengeneza vijiuvimbe vidogo vidogo. Kwa kawaida seli huwa zinajigawa, kupevuka na baadaye kufa kwa kufuata taratibu za mfumo wa mwili. Lakini seli za saratani hazifuati mfumo huo. Badala ya kufa, zenyewe huishi muda mrefu kuliko chembe chembe za kawaida na wakati huo huo huendelea kutengeneza seli nyingine na kuwa uvimbe wa saratani au tumour.
Tezi dume linapatikana katika mwili wa mamalia dume tu na pale seli katika kiungo hicho zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili hapo ndipo mtu hupata saratani ya tezi dume. Ugonjwa huu pia hujulikana kama saratani ya kibofu cha mkojo. Saratani ya tezi dume huwapata wanaume tu na hasa wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Kutokana na tafiti mbali mbali, saratani hii imethibitika kushika nafasi ya pili, ukiachia mbali saratani ya mapafu kwa kusababisha vifo vya wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea.
Tafiti za Chama cha Saratani cha Marekani (ACS) na cha Afrika Kusini (CANSA) zimebaini kuwa, mwanaume mmoja kati ya sita hupata saratani ya tezi dume katika uhai wake. Kutokana na takwimu za mwaka 2010 za dunia nzima, malaria iliua watu laki tano, kifua kikuu watu milioni 2.1, Ukimwi watu milioni 1.8 na saratani watu milioni 9.9. Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ni kubwa ikilinganishwa na ya magonjwa mengine. Dk Emmanuel Kandusi ambaye ni miongoni mwa waathirika wa saratani hiyo, na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume nchini Tanzania ya '50 Plus Campaign' anasema kuwa, ugonjwa huu ukitambuliwa mapema huweza kutibika kwa urahisi. Ameongeza kuwa, kutokana na ugonjwa huo kuwa hatari nchini, ifikapo mwaka 2020 unatarajiwa kuua watu milioni 20.
Kuna vihatarishi vingi vinavyochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Vifuatavyo ni baadhi yake:-
👉🏿Kwanza kabisa ni umri. Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume huongezeka sana hasa ukifikia umri wa karibu miaka 50 na kuendelea.
👉🏿Nasaba ni kihatarishi kingine ambapo wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu huwa katika hatarini ya kupata kansa hiyo kutokana na kurithi jeni za ugonjwa huo.
👉🏿Suala jingine ni lishe ambapo wanaume wanaopenda kula nyama au (red meat) na walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama huwa katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume.
Vilevile wataalamu wanatumbia kuwa, wanaume wasiopenda kufanya mazoezi, wanene na wenye upungufu wa virutubisho vya Vitamin E pia wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya kibofu cha mkojo.
Wanaume wengine walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na wale wenye asili ya Afrika (Weusi) ikilinganishwa na wazungu, wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali, wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi na wachimbaji madini, hususan aina ya cadmium.
Hayo yote yakiwa ni tisa, kumi ni je, dalili za saratani ya tezi dume ni zipi?Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani na zile za kuvimba kwa tezi dume au BPH.
Dalili hizo ni pamoja na,
1) Kupata shida wakati wa kuanza kukojoa.
2) Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa.
3) Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu.
4) Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku.
5) Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote
6) kutoa mkojo uliochanganyika na damu.
Pamoja na kueleza dalili hizo watu wanapashwa kutambua kuwa, mwanaume anapoanza kuona na kuhisi baadhi ya dalili hizo, anapaswa kujua kuwa, seli za saratani katika tezi dume lake huwa zina umri wa takribani miaka saba na kuendelea.
Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu nyigine za mwili, mgonjwa anaweza kuwa na maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni.
Aidha mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu na kadhalika.
Wanaume wanashauriwa kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya kibofu cha mkojo au prostate cancer kwa kuwa imegundulika kuwa wanaume wengi wakiziona na kuzihisi dalili hizo huona soni kwenda kumwona daktari na kufanyiwa uchunguzi.
Baadhi ya watu huzihusisha na magonjwa ya zinaa au na dhana potofu za kishirikina. Wapo wanaokwenda mbali zaidi hata kuuita ugonjwa huo kuwa ni wa walawiti huku wengine wakiurahisisha kwa kuuita kuwa ni ugonjwa wa utu uzima kana kwamba saratani ya tezi dume ni jambo la kawaida kwa watu wazee.
Mambo kama hayo hupelekea wanaume wengi kujinyanyapaa wenyewe na hata wengine kujitibu kwa uficho au kwa kutumia waganga wababaishaji mpaka pale mambo yanapokuwa yamewazidi ndipo hupelekwa mahospitalini na mara nyingine huwa wamechelewa na kupoteza maisha yao bure kwa ugonjwa ambao ungeweza kutibiwa mapema.
Kwa ajili hiyo tunatoa wito kwa wanaume kutoona soni na kuwa na tabia ya kufanyiwa uchunguzi wa afya kwa ujumla, na hasa tezi dume angalau mara moja kwa mwaka.
Kuna vipimo viwili ambavyo daktari anaweza kumpima mwanaume ikiwa ni hatua ya kwanza ya kugundua ugonjwa huo. Vipimo hivyo vya kwanza ni "Digital Rectal Exam (DRE)" na cha pili ni "Prostate Specific Antigen (PSA)". DRE pamoja na PSA huonesha uwepo wa tatizo kwenye tezi dume, lakini vipimo hivi havina uwezo wa kutofautisha iwapo tatizo hilo linamaanisha saratani au uvimbe katika tezi dume. Hivyo basi, ili kuweza kutofautisha kati ya magonjwa hayo mawili, kipimo kiitwacho Prostate biopsy hufanywa. Baada ya vipimo hivyo kama vitaashiria saratani ya tezi dume basi daktari anaweza kuamuru vipimo vingine ili kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huo kama vile transrectal ultrasound au prostate needle biopsy.
Kuna njia kadhaa za matibabu ya saratani ya tezi dume. Hata hivyo uamuzi wa njia gani itumike unategemea ushauri na maoni ya daktari kulingana na hatua ya ugonjwa ulipofikia na umri wa mgonjwa husika. Katika hatua za awali za ugonjwa, daktari anaweza kushauri mgonjwa atibiwe kwa kufanyiwa upasuaji na tiba ya mionzi.
Hii ni katika hali ambayo kwa wagonjwa wazee, daktari anaweza kushauri mgonjwa kuwa chini ya uangalizi tu bila kufanyiwa upasuaji au bila kupatiwa tiba ya mionzi.
Alpha 1-blockers kama vile doxazosin, prazosin, tamsulosin, terazosin, na alfuzosin ni dawa zilizo kwenye kundi la dawa zinazotumika kutibu shinikizo la juu la damu. Dawa hizi hulegeza misuli ya shingo ya kibofu na tezi dume. Hii huruhusu mkojo kutoka kwa urahisi. Watu wengi wanatumia dawa ya Alpha 1-blockers, na husaidia sana kupunguza dalili zao.
Finasteride na dutasteride ni dawa zinazopunguza kiwango cha homoni zinazotengenezwa na tezi dume,hupunguza ukubwa wa tezi dume, huongeza kiwango cha mtiririko wa mkojo, na kupunguza dalili zinazotokana na ukubwa wa tezi dume kuongezeka. Inaweza kuchukua miezi 3 hadi 6 kabla ya kuona mabadiliko makubwa katika dalili zako. Kutumia finasteride na dutasteride kunaweza kuwa na athari kama vile, kupungua kwa nguvu za kiume na hata kuwa hanithi.
Daktari anaweza kuagiza upewe dawa za antibiotiki ili kutibu kuvimba kwa tezi dume (prostatitis), mara nyingi prostatitis huambatana na kuongezeka kwa ukubwa wa tezi dume.
Upasuaji wa tezi dume unaweza kupendekezwa iwapo :
Uchaguzi wa aina maalum ya upasuaji, mara nyingi hutegemea ukali wa dalili ,ukubwa na umbo la tezi dume.
Iwapo saratani imesambaa na kuathiri sehemu nyingine za mwili, matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu au hormonal therapy, au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).
Tukumbuke kuwa, saratani ya tezi dume ni ugonjwa wa kawaida kama yalivyo magonjwa mengine na uchunguzi na matibabu ya mapema huweza kuokoa maisha ya waathirika wengi wa ugonjwa huo.
Updated at: 2024-05-25 10:35:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu zimetengenezwa kwa lengo la kuangamiza wadudu wanaoharibu mazao au wanaomdhuru binadamu. Hata hivyo kutokana na sababu kuwa lengo la dawa hizi ni kuangamiza, huathiri pia viumbe hai vingine akiwemo binadamu.
Takwimu kutoka shirika la afya duniani WHO zinabainisha kuwa kuna zaidi ya vifo 220,000 vitokanavyo na athari za sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia wadudu—viwatilifu.
Ikiwa unataka kuweka afya yako salama, basi karibu nikushirikishe athari 8 kiafya za dawa za kuulia wadudu — viwatilifu.
Watafiti mbalimbali wa maradhi ya saratani wanaeleza kuwa dawa za kuulia wadudu zinachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha seli za saratani mara zinapoingia kwenye mwili wa binadamu.
Hatari hii hutokea zaidi pale ambapo mtu anakula vyakula vilivyoathiriwa na sumu za dawa za kuulia wadudu.
Mwili wa binadamu huzalisha homoni mbalimbali zinazowezesha viungo mbalimbali kufanya kazi vyema.
Dawa za kuulia wadudu zinapoingia mwilini huathiri mfumo wa homoni wa binadamu na kuufanya usifanye kazi vyema.
Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa matatizo ya uzazi kati ya wanaume na wanawake huchangiwa kwa kiasi kikubwa na athari za dawa za kuulia wadudu.
Inaelezwa kuwa sumu hizi zinapoingia mwilini kupitia matunda au mbogamboga huharibu mfumo wa uzazi na kusababisha ugumba au utasa.
Madawa ya kuulia wadudu — viwatilifu huathiri pia mfumo wa ubongo hasa kwa watu wanaoyapulizia au kukaa nayo karibu kwa muda mrefu.
Maradhi kama vile Mild Cognitive Dysfunction (MCD) ambayo humfanya mtu ashindwe kutambua vyema maneno, rangi au namba huchangiwa kwa kiasi kikubwa na athari za dawa za kuulia wadudu.
Mama mjamzito anatakiwa kuchukua tahadhari nyingi sana wakati wa ujauzito ili kulinda afya yake na mtoto aliyeko tumboni.
Matumizi ya viwatilifu ndani ya nyumba au karibu na makazi kwa lengo la kuua wadudu kama vile mbu, chawa, kunguni, au utitiri kunaweza kumwathiri mama mjamzito na mtoto kwa kiasi kikubwa.
Inaelezwa kuwa sumu hizi zinaweza kusababisha mtoto kuzaliwa bila viungo vyote, kuzaliwa kabla ya wakati au hata kifo.
Kumekuwa na taarifa mbalimbali ulimwenguni zikieleza kuwa dawa za kuulia wadudu huharibu viungo muhimu vya mwili kama vile figo na ini.
Utafiti uliofanyika huko India ulibaini kuwa watu wengi waliokufa kutokana na maradhi ya figo waliishi katika mazingira yenye sumu za kuulia wadudu au kula vyakula vyenye mabaki ya sumu hizo.
Kutokana na watu wengi kutumia dawa za kuulia wadudu bila kuvaa vifaa vya kujikinga, wengi huvuta sumu zilizoko kwenye dawa hizo na kusababisha kuathiri mfumo wa upumuaji hasa mapafu.
Hivyo ili kujikinga na athari hii inashauriwa kuvaa vifaa bora vya kuzuia kuvuta sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia wadudu.
Kama ilivyo kwenye swala la kuathiri mfumo wa upumuaji, watumiaji wengi wa dawa za kuulia wadudu hawakingi ngozi zao kwa mavazi au vifaa maalumu vinavyoepusha athari za dawa hizo kwenye ngozi zao.
Ikumbukwe kuwa sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia wadudu zinaweza kuingia mwilini kirahisi kupitia ngozi na kusababisha athari nyingi za kiafya.
Naamini umeona jinsi ambavyo dawa za kuulia wadudu — viwatilifu zinavyoweza kuathiri afya ya binadamu ikiwa hazitatumiwa kwa uangalifu na kwa kufuata kanuni muhimu za matumizi yake.
Ikumbukwe kuwa vifo vingi na matatizo mbalimbali ya kiafya hutokana na mwili wa binadamu kukutana na sumu mbalimbali, hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:51 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anayekunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dumu 56 za soda kwa
mwaka.
Japokua kuna watu wamekiri kunywa hata zaidi ya soda moja kwa siku ambayo huenda wanakunywa zaidi ya hicho kipimo.
Biashara ya soda inalipa sana duniani kwani ni kinywaji cha pili
kinachoongoza kunywewa duniani baada ya maji.
Sasa ukiangalia mahusiano ya unywaji mdogo wa soda kila siku kiafya una madhara makubwa kuliko unywaji mdogo wa pombe kila
siku.
Yaani ni bora unywe chupa moja ya bia kila siku kuliko chupa moja ya soda kila siku.
Kunywa soda moja ni sawa na kunywa vijiko 10 vya sukari, baada ya kunywa sukari hupanda sana mwilini na kongosho hutoa homoni ya insulini nyingi ili kushusha sukari.
Muda unavyozidi kwenda insulini huendelea kuishiwa nguvu[insulin resisitance] na hali hii husababisha kisukari.
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Havard umegundua kwamba watu wanaokunywa soda hunenepa mara mbili zaidi ya wale ambao hawanywi hivyo kama uko busy unapunguza uzito na pia mnywaji wa soda basi unapoteza muda.
Soda ina kemikali inayoitwa phosporic acid ambayo huzuia mwili kuchukua madini ya calcium kwenye chakula ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya mifupa na misuli yenye afya kweye mwili wa binadamu.
Soda ina kemikali inayoitwa caffeine ambayo imehusishwa na cancer mbalimbali za mwili mfano kansa ya kongosho, kansa ya utumbo na magonjwa mengine kama presha ya damu na kansa ya matiti.
Soda haina lishe wala faida yeyote ile kwenye mwili wa binadamu hivyo huongeza kiasi kikubwa cha sumu mwilini ambacho ni hatari sana kwa afya mtumiaji.
Sumu hizo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa presha, na kuua figo.
Kila mtu anataka kuwa na meno masafi na meupe lakini baadhi ya soda zina kiasi kikubwa cha tindikali ambacho hushambulia na kuharibu meno kwa muda mfupi hivyo kama unasumbuliwa na meno basi huu ni muda mzuri wa kuachana nayo.
Soda nyingi zina tabia ya kumfanya mtu apate ulevi wa soda husika yaani kuna watu unakuta anapenda sana soda fulani na asipoinywa kwa siku atahisi kama amepungukiwa kabisa na kitu fulani mwilini.
Hii itakufanya uwe mtumwa wa mwili wako mwenyewe.
Sumu ambazo unazipokea kwenye soda zinazeesha mtu mapema sana yani kijana mdogo wa miaka 20 hujikuta anaonekana kama miaka 35.
Soda ina kiwango kikubwa cha madini ya sodium ambayo humfanya mtu abaki na maji kidogo na kwa muda mrefu atapata matatizo mengine ya kiafya kama mawe ya kwenye figo[kidney stone] na mawe kwenye nyongo ya binadamu.
Ni vizuri kubadili mfumo wako wa maisha na kuanza kunywa vitu ambavyo haviharibu mwili yaani badala ya kunywa soda basi tumia juice (unayoitengeneza mwenyewe) ambayo ni mbadala mkubwa wa soda, lakini pia unaweza kunywa maziwa na kadhalika.
Updated at: 2024-05-25 10:35:03 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hypotension ndio jina linalotumika kuelezea presha ya kushuka ambayo mpaka sasa chanzo chake hakijawa wazi. Kipimo cha presha huwa na namba mbili. Namba moja huwa juu na nyengine huwa chini. Hivyo basi namba ya juu kikawaida kwa mtu mzima inapaswa kuwa 100 hadi 139 na ya chini inapaswa kuwa 60 hadi 90. Hivyo basi pressure yako ikiwa chini ya 100/60 Ndio inajulikana kama Hyptension yaani pressure iko chini. Hypotension (haipo juu). Kwa watu wengi presha hii huwatia kizunguzungu na kuwaangusha. Presha hii ikiwa ya muda mrefu husababisha mtu kupata maradhi ya mshtuko.Watu wenye afya nzuri, hasa wakimbiaji, presha ya kushuka huwa ni dalili ya uzima kwao. Si rahisi kuziona dalili kwa mtu mwenye presha ya kushuka hata kama imedumu kwa muda mrefu. Mara nyingi matatizo ya kiafya huonekana pale mtu presha yake inaposhuka ghafla. Wakati huo wa matatizo ya kiafya, damu kidogo hufika katika ubongo. Hali hii humfanya mtu awe na kizunguzungu au kuumwa na kichwa. Kushuka ghafla kwa presha mara nyingi humtokezea mtu pale anapofanya jambo la haraka kama mtu aliyekaa na kutaka kusimama mara moja. Kitaalamu presha hii inajulikana kama postural hypotension, orthostatic hypotension, au neurally mediated orthostatic hypotension. Postural hypotension inachukuliwa ni hali ile ya kushindwa kwa mfumo wa mawasilianao unaojiendesha wenyewe mwilini kufanya kazi yake kikamilifu (autonomic nervous system). Mfumo huu huendesha na kuongoza vitendo visivyo vya hiari (involuntary vital actions), kama vile mapigo ya moyo kubadilika kutokana na jambo lililotokea kwa wakati uleopo. Kwa kawaida unapoinuka, kiwango fulani cha damu yako kinakuwa kimebaki sehemu ya chini (miguuni). Kukiwa hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa na mwili wako, hali hii itasababisha presha yako kushuka. Katika hali hii mwili wako unafanya nini ? Mwili wako unapeleka taarifa kwenye moyo na kuamuru uongeze usukumaji wa damu ambao utaizidi mishipa yako na kuifanya kuwa membamba hali itakayopelekea kuifanya presha yako kubakia ileile. Ikiwa jambo hili halikufanyika au limaefanyika polepole sana, presha yako itashuka ghafla. Hapa ndipo mtu unapomuona anaguka ghafla. Kwa ufupi athari ya maradhi ya presha ya kushuka na ya juu huongezeka kadri mtu anapokuwa na umri mkubwa na pia kubadilikabadilika kadri umri unavyoongezeka. Jambo jingine la kufahamu ni kuwa, ufikaji wa damu kikawaida kwenye ubungo unapungua kadri umri unavyoongezeka. Inakisiwa kiasi cha asilimia 10 mpaka 20 ya watu wenye umri unaozidi miaka 65, wanapata tatizo la presha yao kushuka.
Updated at: 2024-05-25 10:34:55 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwanini tunajamba? kwanini "ushuzi" unanuka?
Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi wetu,lakini
inaweza kukufanya ujisikie vizuri kujua kwamba ni tendo
la kawaida sana kwa mwili wa binadamu kutenda.Kila
mtu anajamba,hata Halle Berry nae hujamba.
1.Kujamba ni nini hasa?
Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa,ambayo
inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi.Baadhi ni hewa
tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa.Hewa ingine
husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu
kutoka kwenye damu,na baadhi ya gesi huzalishwa na
kemikali katika utumbo au bakteria.Kwa kawaida
"ushuzi" unakua na asilimia 59 ya gesi ya
nitrogen,asilimia 21 ni hydrogen,asilimia 9 ni carbon
dioxide,asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen.
Asilimia moja tu ya "ushuzi" inaweza kuwa hydrogen
sulfide na mercaptans,ambayo ndio ina sulfur ndani
yake,sulfur ndo hufanya "ushuzi" utoe harufu mbaya
Kujamba huambatana na sauti,hii ni kutokana na
"vibration" katika njia ya haja kubwa.Ukubwa wa mlio wa
kujamba hutegemea "presha" inayosukuma gesi itoke nje
na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.
2.Kwa nini Ushuzi hutoa Harufu mbaya?
Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa
mtu,vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio husababisha
hili.Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama
maharage,kabichi,soda na mayai.
3.Watu hujamba hadi mara 14 kwa siku
Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa
siku.Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi
cha miaka 6,anaweza kuzalisha nishati ya kutosha
kutengeneza bomu la atomiki.
4.Ushuzi husafiri kwa mwendo wa futi 10 kwa sekunde.
Harufu ya ushuzi huanza kusikika sekunde 10-15 baada
ya mtu kujamba,hiyo ni kwa sababu inachukua muda
mrefu kwa harufu kufikia pua.
5.Kujizuia Kujamba Inaweza Kuhatarisha Afya Yako
Madaktari hawajakubaliana moja kwa moja kama kujizuia
kujamba ni hatari kiafya.Baadhi ya wataalam wanafikiri
kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa
mmeng'enyo wa chakula,hivyo kujizuia kujamba
haitakuletea madhara.Wengine wanadhani kwamba
kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa
gesi,na pia inaweza sababisha bawasili (hemorrhoids).
6.Kwa Baadhi ya Tamaduni,Kujamba Sio Ishu
Wakati tamaduni nyingi zikichukulia tendo la kujamba
lifanywe kistaarabu,kuna baadhi ya tamaduni hawaoni
haya kujamba hadharani,na pia hufurahia tendo
hilo.Mfano kabila la Yanomami huko America ya
Kusini,kwao husalimiana kwa kujamba,na China
unaweza kupata kazi ya kunusa ushuzi! Katika Roma ya
zamani,Mfalme Claudius akihofia kwamba kujizuia
kujamba inaweza kuwa hatari kiafya,alipitisha sheria
kwamba ni ruhusa kujamba kwenye "banquets".
7.Ushuzi Unawasha Moto
Kama ilivyoandikwa hapo juu,methane na hydrogen
inayozalishwa na ushuzi inaweza sababisha moto.
8.Mchwa Hujamba Kuliko Wanyama Aina Zote
Ni ngumu kuamini kuwa mchwa ndo anawajibika na
matatizo yetu ya "Global Warming".Mchwa huongoza kwa
kujamba kwa wanyama,na hiyo huzalisha gesi ya
methane.
9.Ukiubana Ushuzi,Utakutoka Usingizini
Hata ujitahidi kuubana vipi,ushuzi utatoka mara
utapokua umepumzika,hasa ukiwa umelala.
10. Watu Hujamba Hata Baada ya Mauti Kuwafika
Maiti huendelea kutoa gesi hadi masaa matatu baada ya
mtu kufariki dunia,hii huambatana na milio ya
kujamba.Hali hii husababishwa na misuli kusinyaa.
UKIPATA NAFASI JAMBA MWANANGU
Updated at: 2024-05-25 10:35:05 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na asilimia 54 ya watu wazima hukoroma baadhi ya wakati huku asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati. Kukoroma baadhi ya wakati kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji. Hata hivyo kukoroma huko sio tu kwamba huharibu usingizi wa anayekoroma bali pia huwasumbua na kuwakeresha wanaolala karibu na mkoromaji. Wale wenye tabia ya kukoroma, hukoroma kila wanapolala na mara nyingi huchoka wanapoamka, na watu wa aina hii hushauriwa kumuona daktari na kushauriwa kuhusiana na tatizo hilo. Lakini kabla hatujaendela mbele ni bora tujue kukoroma hasa ni nini au hutokea vipi? Mtu huwa anakoroma pale kunapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na matokeo yake ni sauti inayosikika ya kukoroma. Kuingia au kutoka kwa hewa huweza kuzuiwa na sababu mbalimbali kama vile: • Kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi zitumike katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala. Kitendo hicho hupelekea nyama laini za pua na koo zijikusanye na kusababisha mkoromo. Kuna baadhi ya watu wanakoroma tu kipindi cha allergy (allergy season) au wanapatwa na matatizo ya sinus. Baadhi ya matatizo kama vile kupinda pua (deviated septum) au ukuta unaotenganisha tundu za pua na polyps za pua pia huweza kufanya pua zizibe na kusababisha kukoroma. Watu wengi wanaofanya operesheni za pua pia hupatwa na tatizo la kukoroma. • Kuwa na misuli dhaifu katika koo na ulimi. Misuli au nyama za koo na ulimi zinapokuwa dhaifu sana hulegea na kuanguka upande wa nyuma wa sehemu inayopita hewa. Suala hilo hutokea pale mtu anapolala fofofo au kuwa na usingizi mzito na kusababisha kukoroma. • Kuwa na misuli minene ya koo. Hii ni kwa wale watu wanene ambao hata nyama zao za koo pia hunenepa na kupanuka na suala hilo husababisha kukoroma, Pia watoto wenye tonsesi kubwa na adenoids baadhi ya wakati hukoroma. • Kuwa na kilimi kikubwa ni mojawapo ya sababu zinazosababisha kukoroma. Kilimi kirefu kinaweza kuzuia koo na pale kinapotikisika wakati hewa inapita kwa msukumo husababisha kukoroma. • Sababu nyinginezo zinazoweza kumsababishia mtu akorome anapolala ni kuwa na umri mkubwa au uzee, imeshuhudiwa kuwa watu wa makamo na wazee hukoroma, kwani misuli na nyama za koo huanza kuzeeka na kulegea kadri umri unayoongezeka. Vilevile wanaume wanakoroma zaidi kuliko wanawake hii ni kutokana na wanaume kuwa na njia nyembamba zaidi ya hewa kuliko wanawake. Kukoroma pia kunaweza kuwa ni tatizo la kurithi. Pombe, kuvuta sigara na matumizi ya baadhi ya dawa pia husababisha misuli ya koo ilegee na hivyo hupelekea mtu akorome. Kulala vibaya pia husababisha kukoroka kama vile kulala kichalichali, kwani hufanya nyama za koo zilegee na kuziba hewa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:54 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tezi dume kila mwanaume anazaliwa nayo ambayo inasaidia kutoa maji maji ambayo yanaweza kusaidia kutengeneza mbegu za kiume.
Maji maji hayo yana alkaline ambayo husaidia Wakati Wa tendo la ndoa asidi (acid) iliyopo Kwa mwanamke isiue mbegu za kiume.
Kwahiyo alkaline ikichanganyika na asidi tunapata neutral na hivyo kusaidia mbegu za kiume zisife zinapoingia Kwa mwanamke.
Kwenye uke kuna asidi ambayo inaua kila bacteria wanaoingia.
Acid+base=salt+water
Tezi dume endapo itakuwa zaidi ndo huweza kuleta madhara ambayo ni kufunga mkojo usitoke kwani hubana mrija unaotoka kwenye kibofu kwenda nje.
Tatizo hilo huwakumba zaidi wanaume zaidi ya miaka 50,60,80 japo sio wote.
Kinga yake.
1. Kunywa maji ya kutosha.
2. Kupunguza kula nyama nyekundu.
3. Kupunguza ulaji wa mafuta.
4. Kula matunda na mbogamboga.
5. Kushiriki tendo la ndoa angalau Mara moja au mbili Kwa wiki ili kupunguza maji maji kwenye tezi dume.
6. Kufanya mazoezi ya viungo.
Kwahiyo tezi dume ni kiungo ambacho wanaume huzaliwa nacho isipokuwa kinaleta madhara endapo kitakuwa kupita kiasi na hutibiwa na kupona.
Matibabu yake ni kufanya upasuaji na kupunguza ukubwa pamoja na kudhibiti homoni za ukuaji wake.
Tiba nzuri ya tezi dume ni kufuata ushauri hapo juu na si vidole
Updated at: 2024-05-25 10:34:52 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Updated at: 2024-05-25 10:35:03 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tatizo hili husimama lenyewe kama ugonjwa ingawa pia inaweza kuwa ni dalili kama mwanamke ni mjamzito, ananyonyesha au ametoa mimba au ameharibikiwa na mimba. Kusimama kwake kama ugonjwa ni pale yanapotoka wakati mwanamke hana historia ya dalili hizo hapo juu.
Tatizo hili huwapata wanawake wengi na kwa mujibu wa takwimu huathiri asilimia tano hadi 32 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa. Pamoja na kuwapata zaidi wanawake, hali ya kutokwa na majimaji katika matiti pia huweza kuwatokea wanaume watu wazima, vijana walio katika umri wa balehe, wa kike na wa kiume, watoto wachanga wa kike na wa kiume.
Matiti yanaweza kutoa majimaji endapo chuchu zitachezewa au kunyonywa mara kwa mara na kusababisha kuvuruga baadhi ya homoni mwilini.
Homoni zinazohusika zaidi na tatizo hili ni homoni ya ‘prolactine’.
Vilevile katika hali hii ya kutokwa na majimaji asilimia 50 ya matatizo chanzo chake bado hakijulikani.
Mama anayenyonyesha homoni zinazochangizwa na kusababisha matiti yatoe maziwa ni ‘Prolactin’, Estrogen’ na Progesterone.
Dawa nyingine zinazoweza kumfanya mtu atokwe na majimaji katika matiti ni dawa kama Methyldopa, madawa ya kulevya na dawa za magonjwa ya akili.
Pamoja na matatizo katika mfumo wa homoni, hali ya kusuguasugua kifua mara kwa mara, hali ya kuwa na hofu na wasiwasi au shauku f’lani, mfano ya kuhitaji kupata ujauzito husababisha kuamsha homoni za uzalishaji wa maziwa au hayo majimaji.
Vyanzo vingine ni matatizo kichwani kwenye tezi ya ‘pituitary au pituitary adenoma’.
Dawa nyingine zinazoamsha tatizo hili ni kama vile ‘Cimetidine’ ambazo hutibu vidonda vya tumbo.
Pia zipo dawa nyingine za asili ambazo hazijafanyiwa utafiti wa kutosha zinazoweza kusababisha tatizo hili.
Mwanamke mwenye tatizo hili la kutokwa na maziwa kwenye matiti wakati si mjamzito na wala hana historia ya kuwa na mimba, huwa hapati ujauzito.
Mwanaume mwenye tatizo hili hupungukiwa na nguvu za kiume, uzalishaji wa mbegu za kiume huwa mdogo.
Kwa vijana na watoto wa kiume au wa kike ni vema uchunguzi wa kina ufanyike.
Maziwa yanaweza kutoka tu yenyewe au kwa kuminyaminya matiti au chuchu.
Hufanyika hospitalini kwa madaktari wa masuala ya uzazi. Vipimo vya damu kuangalia homoni, matatizo katika matiti, na ikibidi CT-Scan vitafanyika kuangalia matatizo katika tezi ya Pituitary.
Wahi hospitali kwani athari ya tatizo hili ni kupoteza uwezo wa kuzaa.
Epuka kuchezea chuchu ziwe zako mwenyewe au za mpenzi wako au za mtoto kwani unaamsha homoni ambazo katika wakati huo hazitakiwi.