Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
"Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako na……..
Updated at: 2024-05-25 18:06:32 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
"Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako na……..
Kabla hajamalizia sentensi simu
ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake.
Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku
jamaa anasikia
"Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile
nyumba yangu sasa nimeona niwatumie milioni
20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio.
Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama
ana mradi mwingine nimpe hela kidogo".Baada
ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa
akamuuliza,"eeenhee!!! ulikuwa unasema
umenichoka nikusanye nguo zangu halafu
iweje? Jamaa kwa upole akajibu "Nilikuwa
nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue".
Hii ndio ndoto ya harusi ya kila msichana anayotamani
GIRL: Baby, hebu niambie harusi yetu itakuwaje?
BOY: Yaani hii haijawahi kushuhudiwa, ngoja nikupe kionjo kidogo tu
GIRL: Enhee…
BOY: Kwanza siku ya kupeleka mahari nitaswaga zizi zima la ng'ombe napeleka kwa babu yako
GIRL: Ooh baby u care..
Updated at: 2024-05-25 18:05:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
GIRL: Baby, hebu niambie harusi yetu itakuwaje?
BOY: Yaani hii haijawahi kushuhudiwa, ngoja nikupe kionjo kidogo tu
GIRL: Enhee…
BOY: Kwanza siku ya kupeleka mahari nitaswaga zizi zima la ng'ombe napeleka kwa babu yako
GIRL: Ooh baby u care..
BOY: Siyo hivyo tu, baba yako ntamnunulia Range Rover Sport na mama mkwe ntampa Range Rover Evoque
GIRL: Baby u are awesome…
BOY: Halagu mdogo wako wa kiume ntampa Prado Tx, na hapo nimesukutua tu mdomo sijaanza kula….
GIRL: Enhee…na sisi??
BOY: Sisi tutachukua mtaa mzima Oysterbay, kila wiki tutaishi nyumba tofauti
Halafu siku ya harusi yetu tutakodi zile meli zinabeba makontena ndiyo iwe ukumbi wetu, itatupeleka hadi Maldives
GIRL: Baby I love you
BOY: Tukitoka hapo tunaenda honeymoon Bahamas….halafu tunaenda Taiwan shopping ya fenicha, kisha Japan shopping ua electronics, halafu tunaenda Dubai nikununulie vito vya thamani
GIRL: Ooh my sweetheart…halafu tukitoka huko??
BOY: Tukitoka huko nachukua ndoo ya maji nakumwagia uzinduke usingizini na ndoto yako imeishia hapo
Chezea paka wewe, Angalia kilichomkuta huyu na paka wake
Updated at: 2024-05-25 17:02:32 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa alichukua paka wake na kwenda kumtupa mbal,aliporudi nyumban alimkuta paka amekwisharudi,jamaa alikasirika sana.
Siku ya 2 akamchukua na kwenda naye zaid ya kilometa 50 akapiga chochoro za kutosha kisha akamtupa,akaanza safar ya kurud nyumban baada ya muda akampigia cm mkewe.Vp mke wangu huyo paka yupo? MKE:Ndio mume wangu tena ametulia hapa kwan imekuaje? JAMAA:hebu mpe cm anielekeze njia ya kurud nimepotea😳
Updated at: 2024-05-25 17:12:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Eti kuna mkaka alitembelewa na mama yake mzazi. Wakiwa sebuleni yeye, mama na mke wake, mke wake akaanza kuonekana tofauti kama vile anajiskia vibaya. Akaenda chumbani. Baada ya muda mfupi yule mkaka akamfuata. Wakakaa sana huko kisha mkaka akarudi sebuleni kuendelea kuongea na mama yake. Lakini zipu ya suruali yake ilikuwa wazi. Mama akamuuliza, mkeo anaendeleaje? Akamuambia, anajisikia vzr sasa. Nimempa panadol. Mama akatabasamu na kumwambia mwanaye, sawa. Lakini siku nyingine ukishatoa panadol ukumbuke kufunga pharmacy😂😂
Angalia huyu baba alichowafanya mtoto wake wa kike na boyfriend wake
Updated at: 2024-05-25 18:12:37 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
BABA OYEEEEEE💪💪 Soma hii…
Msichana alikuwa amekaa na baba yake kibarazani, mara akamuona MVULANA friend wake akija, yule mvulana alipokaribia tu, yule msichana akamwambia hivi:-
MSICHANA: Umekuja kuchukua kile kitabu chako, kinachoitwa "DADDY IS AT HOME?" by Ngozi Okafor
MVULANA: Hapana!, Nimekuja kuazima kitabu cha maombi kama kinaitwa "WHERE SHOULD I WAIT FOR YOU?" by Ngũgĩ wa Thiong'o
MSICHANA: Aaah! Hicho sina ila ninacho kimoja kinaitwa "UNDER THE MANGO TREE" by Chimamanda Adichie
MVULANA: Ooh! Vizuri, Basi usisahau kuja nacho kesho kitabu cha Okot p'Bitek kile kinachoitwa "CALL ME IN 5 MINUTES BEFORE" Utakapokuja shule.
MSICHANA: Usijali, tena nina kitabu kipya kinaitwa "I WON'T LET YOU DOWN" by Chinua Achebe
Baba mtu akawatazama kisha akasema
BABA: Vitabu vyote hivyo, mbona vingi sana, atavisoma vyote kweli
MSICHANA: Ndio Daddy, huyu mvulana yupo smart sana na ana akili atavisoma vyote hivyo!
BABA: Sawa! Usisahau kumpatia na kile ambacho nimekiweka pale juu ya meza, kinaitwa "I AM NOT STUPID, I UNDERSTOOD EVERYTHING YOU'VE BEEN SAYING" by Shakespeare!
Na kuna kingine nimekiweka juu ya kabati la vyombo, kinaitwa "IF YOU GET PREGNANT PREPARE TO GET MARRIED" by Wole Soyinka.