Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Utajuaje kama una upungufu wa maji mwilini? Dalili ni hizi

Featured Image
Upungufu wa maji ni pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji. Ili mwili uweze kufanya kazi yake vizuri, kiwango cha maji mwilini hakipaswi kupungua hata kidogo, hivyo kila mtu ana wajibu wa kunywa maji ya kutosha kila siku ili kulinda kiwago chake cha maji kisipungue na kinapopungua ndipo hapo mwili huanza kuonesha dalili za kukaukiwa maji (dehydration).

Zifutazo ndizo dalili za upungufu wa maji mwilini;

Dalili za upungufu wa maji kwa mtoto.

Kwa kawaida, dalili za upungufu wa maji mwilini hujitokeza zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima au wazee. Dalili za upungufu wa maji mwilini kwa watoto huweza kusabababishwa ama na kuharisha, kutapika, kutokunywa maji au vimiminika vingine vya kutosha.

Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji huweza kuonesha dalili zifutazo:

  1. Kukojoa mara chache sana
  2. Mdomo na ulimi kukauka
  3. Mtoto kulia mara kwa mara na anapolia machozi hayatoki.
  4. Mtoto kutokuwa mchangamfu
  5. Macho, tumbo au mashavu kubonyea

Dalili za upungufu wa maji kwa wazee.

Dalili za upungufu wa maji kwa wazee ni tofauti na watu wazima. Wazee wa umri zaidi ya miaka 60 huwa na ngozi iliyosinyaa na hata ukiiminya, hubaki katika hali hiyo kwa muda na unapoikwaruza alama hubaki. Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa.

Dalili za upungufu wa maji kwa wajazito.

Upungufu wa maji mwilini kwa waja wazito ni hatari kwa mama pamoja na mtoto. Dalili zinazoweza kujitokeza kwa waja wazito ni pamoja na:
  1. Kukojoa mkojo wa njano nyeusi
  2. Kuumwa na kichwa.
  3. Mwili kukosa nguvu.
  4. Kichefuchefu na kutapika.
  5. Kukaukwa na mdomo.
Ili kujiepusha na matatizo ya upungufu wa maji na hatimaye kujikuta unakumbwa na dalili kadhaa zilizoelezewa hapo, ambazo ziko pia kwa watu wazima wengine, ni kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Hata utakapozidiwa na kukimbizwa hospitali, hakuna dawa nyingine utakayopewa zaidi ya maji (re-hydrating solution) . Kwa nini usubiri hali hiyo ikutokee wakati unaweza kuizuia kwa kunywa maji tu? Hivyo wito wetu kwako kuendelea kunywa maji mengi ya kutosha kadri uwezavyo hii itakusaidia sana kwa namna moja ama nyingine kuwa na afya bora
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Madhara ya kunywa maji baridi na faida za kunywa maji moto na asali

Madhara ya kunywa maji baridi na faida za kunywa maji moto na asali

UNYWAJI wa maji baridi, hasa katika joto kali kama la Dar es Salaam, ni kiburudisho kikubwa cha k... Read More

Mambo 10 yanayosababisha wanawake washindwe kupata mimba au wawe wagumba

Mambo 10 yanayosababisha wanawake washindwe kupata mimba au wawe wagumba

Ugumba ni nini ?
Hii ni hali ya wapenzi au mke na mume kutopata ujauzito. Ugumba unaweza kua... Read More

Tatizo la kutoka majimaji kwenye matiti

Tatizo la kutoka majimaji kwenye matiti

Tatizo hili husimama lenyewe kama ugonjwa ingawa pia inaweza kuwa ni dalili kama mwanamke ni mjam... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia maganda ya ndizi

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia maganda ya ndizi

Maganda ya ndizi ni dawa nyingine nzuri ya kuondoa chunusi. Unachohitaji ni kuwa tu na maganda ya... Read More

Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

Tezi Dume ni nini?