Jinsi ya kufanya kupunguza unene wa mwili kwa haraka
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Nichukue wasaa huu kukuarika rasmi ewe mpenzi na mfuatiliaji wa blog hii ya Muungwana blog, naomba nichukue walau dakika zako chache niweze kukueleza kinagaubaga ni kwa jinsi gani unaweza kupunguza mwili wako kwa kutumia hatua zifuatavyo:
1. Zingatia muda wa kula.
Watalamu wa masuala ya afya wanasema muda mzuri wa kula chakula ni masaa manne baada ya kuamka, pia chakula cha mchana kiliwe tena baada ya masaa nne mara baada ya kupata kifungua kinywa, na masaa takribani matatu kabla ya kulala, kufanya hivi huupa mwili wako mda wa kukimenโgenya chakula vizuri na kuyeyusha mafuta yaliyopo kwenye chakula pia. Hivyo unakumbuswa kufanya hivi kila wakati kama kweli unataka kupunguza mwili wako.
2. Epukana msongo wa mawazo
Msongo wa mawazo au stress hupelekea kula vyakula ambavyo sio sahihi kwa afya yako na kwa wingi kama vile pombe, snacks mfano crips, biskuti, pipi,c hocolate na kadhalika hata hivyo mwili huhifadhi mafuta kwa wingi kipindi ukiwa na stress, hivyo kila wakati epuka kula vyakula ambavyo vitakusababishaia kuwa mwili wenye mafuta.
3. Kutoruka mlo wa asubuhi(breakfast)
Wengi wetu tumejikuta tukimaintain kwa kuruka breakfast na baadae kujikuta tukifidia ule mlo kwa kula chakula kingi zaidi, Kufanya hivi sio kujipunguza bali kukufanya uzidi kunenepa zaidi, hivyo unatakiwa kuzingatia ya kwamba hauli chakula kingi kama mchana hukupata kifungua kinywa, unachotakiwa kufanya ni kula chakula cha kawaida tu.
4. Angalia aina ya chakula.
Aina ya vyakula sahihi tunavyopaswa kula ni vyakula vyenye protein kwa wingi kama vile mboga za majani na matunda kwa wingi pia ,wanga kidogo bila kusahau unywaji maji ya kutosha. Kufanya hivi kutakusaidia kuweza kupungua na kuwa na mwili wa kawaida
5. kupata usingizi wa kutosha
Inashauriwa kulala masaa 6 hadi 8, kwani Kutopata usingizi wa kutosha hufanya mwili wako kumenโgenya chakula taratibu .
Lakini pia diet tu haitoshi mazoezi nayo ni muhimu katika kupunguza uzito,hakikisha unafanya mazoezi walau mara tatu hadi nne kwa week kwa muda wa dakika 20 hadi 30.
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha mama mjamzito mimba yake kuharibika. Sababu kuu huwa ni...
Read More
Kitaalamu chakula unachokula leo ndio kinaamua hali ya afya yako kwa siku za usoni. Na ni muhimu ...
Read More
Katika urutubishaji yai la mwanamke linabeba chromosome X yani XX. Na mbegu ya mwanaume inabeba c...
Read More
Kuchagua vyakula sahihi kwa mlo wako inaweza kuwa changamoto na tungependa kuamini kwamba kupungua u...
Read More
Kukosa choo ni tatizo kubwa katika jamii zetu japo huwa halionekani kama ni tatizo. Hata hivyo ku...
Read More
Shelisheli lililokomaa huwa na uzito wa hadi kilo 6, ambapo mshelisheli unaweza kukua kwa urefu w...
Read More
Je unafahamu ya kwamba rangi ya mkoja inakupa matokea sahihi kuhusu afya yako? Kama jibu ni hapan...
Read More
Ili mtoto azaliwe akiwa na afya njema pamoja na akili timamu, akiwa tumboni lazima alishwe lishe ...
Read More
Maziwa ni chakula kikuu cha mtoto punde anapozaliwa. Mama anahitaji kuwa na Maziwa ya kutosha ili...
Read More
-Hii ni tezi ya wanaume yenye sifa zifuatazo.
~Ina umbo km yai(oval shape)
~Ina ukubwa ...
Read More
Zabibu huweza kutumika kama tiba ya shinikizo la chini la damu kama ifuatavyo
Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki,...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!