Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Dalili, athari, kinga na tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB)

Featured Image
Kifua kikuu ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya bacteria na kuenezwa kwa njia ya hewa. Mtu mwenye maambukizi ya kifua kifua kikuu akikohoa, kupiga chafya au kutema mate ovyo husambaza vijidudu hewa, huweza kumwabukiza mtu mwingine kama atakuwa hajaanza kutumia dozi ya kifua kikuu.

Dalili za kifua kikuu.

  1. Kukohoa kwa muda wa wiki mbili au zaidi
  2. Maumivu ya kifua
  3. Homa za usiku
  4. Kutoka jasho kwa wingi usiku
  5. Kupungua uzito
  6. Kukohoa damu
  7. Kukosa hamu ya chakula na mwili kuwa dhaifu

Athari za kifua kikuu.

  1. Ugonjwa huweza kuenea kwenye viungo vingine vya mwili.
  2. Watu wengine hupoteza maisha iwapo hawatapata tiba sahihi mapema.
  3. Watu wengine huambukizwa ugonjwa katika muda mfupi.
  4. Wagonjwa wa kifua kikuu hawazezi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendelea.
  5. Matibabu ya kifua kikuu huchua muda mrefu na ni gharama kubwa.

Kinga za ugonjwa wa kifua kikuu.

Ugonjwa huu unakingwa kwa chanjo ya kifua kikuu kwa kitaalamu (BCG) ambayo hutolewa mara tu mtoto anapozaliwa.
Ili kupunguza uwezekano wa kupata kifua kikuu zingatia yafuatayo;
  1. Kujenga na kuishi kwenye nyumba zinazoruhusu mzunguko kwa hewa ya kutosha (ziwe na madirisha makubwa ya kutosha)
  2. Epuka kukaa kwenye msongamano wa watu wengi
  3. Watoto wanyonyeshwe maziwa ya mama pekee kwa miezi sita na umlikiza kwa vyakula vyenye virutubisho ili kumjengea kinga imara
  4. Kula vyakula vyenye lishe bora
  5. Kutotema mate na makohozi ovyo ili kuziua usambaaji wa bacteria wasababishao Kifua kikuu.

Ratiba ya chanjo.

Chanjo ya kifua kikuu hutolewa baada ya mtoto kuzaliwa au anapofika kliniki kwa mara ya kwanza Iwapo kovu kwa mtoto halijajitokeza chanjo irudiwe katika kipindi cha miezi 3.

Tiba ya kifua kikuu (TB)

Ugonjwa wa kifua kikuu unatibika. Matibabu yake huchukua muda mrefu wa miezi 6 hadi 8 na ni ya gharama kubwa. Inashauriwa mgonjwa awahi matibabu mapema kwenye vituo vya kutolewa huduma za kinga. Ugonjwa wa kifua kikuu ni hatari, hata hivyo unakingwa kwa chanjo. Mzazi au mlezi hakikisha kila mtoto anapozaliwa anapata chanjo ya kuzuia kifua kuu โ€œKumbuka chanjo ya kifua kikuu (BCG) Itamkinga mtoto dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuuโ€.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Sababu na madhara ya tatizo la kukosa choo

Sababu na madhara ya tatizo la kukosa choo

Tatizo la kukosa choo (constipation) ni tatizo ambalo limekuwa likiwakumba watu wengi sana katika du... Read More
Aina ya vyakula vinavyotakiwa kwa wajawazito

Aina ya vyakula vinavyotakiwa kwa wajawazito

Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na ... Read More

Hizi ndizo sababu kwa nini ule Tende kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Hizi ndizo sababu kwa nini ule Tende kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Kitaalamu chakula unachokula leo ndio kinaamua hali ya afya yako kwa siku za usoni. Na ni muhimu ... Read More

Vyakula vinavyofaa kuliwa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Vyakula vinavyofaa kuliwa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Vyakula vinavyofaa kuliwa wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni vingi, leo tutaan... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa mdalasini na asali

Jinsi ya kutibu chunusi kwa mdalasini na asali

Mchanganyiko wa mdalasini na asali ni dawa nzuri ya kutibu chunusi.

Changanya asali viji... Read More

Jinsi ya kufanya kupunguza mwili kwa kupanga ulaji wa chakula

Jinsi ya kufanya kupunguza mwili kwa kupanga ulaji wa chakula

Ulaji wa vyakula vingi vya wanga na mafuta ni chanzo kikubwa cha unene na uzito kuongezeka. Vyaku... Read More

Njia za kutibu chunusi bila kwenda hospitali

Njia za kutibu chunusi bila kwenda hospitali

Chunusi ni nini?

Tezi Dume ni nini?