Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Je, kwa nini akina mama wajawazito hawatakiwi kunywa pombe?

Featured Image

Wanawake wajawazito ambao hunywa pombe au kuvuta sigara
wanahatarisha afya na maisha ya mtoto aliye tumboni. Mtoto aliye
tumboni hurutubishwa kupitia damu ya mama. Kama mama atavuta
sigara au kunywa pombe, sumu illiyopo katika sigara au pombe
inapoingia kwenye damu yake itamfikia mtoto pia. Pombe hushambulia
moyo uendeleao kukua na ubongo wa mtoto aliye tumboni.
Akina mama wanaokunywa kupita kiasi wakiwa wajawazito
wanaweza kupata watoto wenye magonjwa ya moyo au mtindio
wa akili, kwa sababu chembechembe za ubongo hazikui vizuri.
Mara nyingi watoto huzaliwa na upungufu katika mwonekano
wa sura. Kwa mtoto pombe ni sumu kali, hata kama ni kwa kiasi
kidogo, itamdhuru.

Mama anaekunywa pombe anaweza kuwa hajali au kusahau
kujilinda mwili wake na mtoto anayekua.
Kama akipata maambukizo ya VVU na mtoto pia anaweza
akapata virusi vya UKIMWI.
Wanawake wanaovuta sigara wakiwa wajawazito wana
uwezekano mkubwa wa kuzaa watoto ambao hufariki ghafla bila
sababu ya kueleweka katika mwaka wao wa kwanza wa maisha.
Watoto wa akina mama wanaovuta sigara mara nyingi huzaliwa
na umbo dogo kuliko wengine kwa sababu watoto walipata
chakula kidogo walipokuwa bado tumboni mwa mama zao.
Ujumbe upo wazi: Wanawake wanaotaka watoto wenye afya
wasivute kabisa sigara wala kunywa pombe wakiwa wajawazito.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Msichana ambaye hajawahi kujamiiana anaitwa bikira, je mvulana huitwaje?

Msichana ambaye hajawahi kujamiiana anaitwa bikira, je mvulana huitwaje?

Neno β€œbikira” ni mtu yeyote ambaye hajawahi kujamii ana maishani mwake, awe mwanamke au mwana... Read More

Utoaji wa zawadi kwa kubadilishana na kujamiiana

Utoaji wa zawadi kwa kubadilishana na kujamiiana

Kutoa zawadi kwa mtu kwa kubadilishana ili kujamiiana
ni unyanyasaji mbaya. Iwapo mpokeaji w... Read More

Je, inachukua muda gani tangu mtu aambukizwe na VVU hadi vionekane kwenye damu?

Je, inachukua muda gani tangu mtu aambukizwe na VVU hadi vionekane kwenye damu?

Inakadiriwa huchukua miezi mitatu tangu kuambukizwa na VVU hadi i virusi hivyo vionekane kwenye d... Read More

Jinsi ya Kuonyesha Utambulisho Wako kwa Msichana

Jinsi ya Kuonyesha Utambulisho Wako kwa Msichana

Jinsi ya Kuonyesha Utambulisho Wako kwa Msichana

Kuonyesha utambulisho wako kwa msichana n... Read More

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Hatia Baada ya Kufanya Ngono

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Hatia Baada ya Kufanya Ngono

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Hatia Baada ya Kufanya Ngono

Karibu vijana wapendwa! Leo,... Read More

Je, Ni Vipi Kuepuka Kufanya Ngono Kwa Sababu ya Kubembelezwa?

Je, Ni Vipi Kuepuka Kufanya Ngono Kwa Sababu ya Kubembelezwa?

Je, Ni Vipi Kuepuka Kufanya Ngono Kwa Sababu ya Kubembelezwa? 😊✨

Karibu rafiki yangu!... Read More

Dalili za kwanza za msichana au mwanamke kuwa na mimba ni zipi?

Dalili za kwanza za msichana au mwanamke kuwa na mimba ni zipi?

Dalili moja i iliyo wazi zaidi ni kukosa hedhi. Mwanamke akijamii ana na mwanaume bila kutumia kinga... Read More
Madhara ya dawa za kulevya yanadumu kwa muda gani?

Madhara ya dawa za kulevya yanadumu kwa muda gani?

Ni vigumu sana kujibu swali hili kwa sababu muda wa madhara hutegemea sababu mbalimbali kama vile... Read More

Ukeketaji ni nini?

Ukeketaji ni nini?

Katika baadhi za jamii viungo vya uzazi vya nje vya msichana,
yaani kisimi au sehemu ya ndan... Read More

Je, kuna vipimo ambavyo vinaweza kugundua hali ya kuwepo kwa ualbino wakati kichanga kikiwa bado tumboni?

Je, kuna vipimo ambavyo vinaweza kugundua hali ya kuwepo kwa ualbino wakati kichanga kikiwa bado tumboni?

Hakuna kipimo rahisi cha kuwezesha kuonyesha kama mama
mjamzito amebeba kinasaba cha ualbino... Read More

Kwa nini watu wanaamini kuwa Albino hawana maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (VVU)?

Kwa nini watu wanaamini kuwa Albino hawana maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (VVU)?

Imani hiyo si kweli kabisa. Inawezekana ni kupotoshwa kwa
makusudi wa ukweli kuhusu jambo hi... Read More

Kwa nini mara nyingine uume hausimami?

Kwa nini mara nyingine uume hausimami?

Ili mwanaume aweze kujamii ana, ni lazima uume usimame na kuweza kupenya ukeni. Kama mvulana anasisi... Read More
πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About