Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Nia yako isishindwe

Featured Image

Nimejifunza jambo kubwa sana ambalo sote tuna lijua nalo ni "NIA".
Nimemtazama mwendesha pikipiki anaiwasha pikipiki kwa muda mrefu kwa kupiga kiki kwa kurudia rudia, akiamini lazima iwake ili aende anakotaka kwenda. Anajaribu kuwasha kwa kiki ikikataa anajaribu kwa starter, ikigoma anajaribu kuchomoa plug na kuangalia kama kuna tatizo, anajaribu tena na tena mpaka inawaka, anaanza safari yake.

Ingawa ametumia muda mwingi kuhangaika kuiwasha pikipiki yake lakini hakuzimia moyo na kuamua kuitelekeza ili atembee kwa miguu, ila alikua na "NIA" isiyozimika haraka mpaka atakapoona imewaka kwakua anaamini jana iliwaka, lazima na leo iwake hata kama imelala kwenye hali ya hewa ya namna gani.

Ikiwa tunakua na "NIA" ya kufanya mambo madogo madogo yatokee, na tunayasimamia kwa "IMANI" kabisa mpaka yanakua kweli, kwanini tunaogopa kusimamia mambo makubwa yatokee maishani mwetu?. Kwanini unadiriki kusema kwenu hakuna aliyewahi kufanikiwa, hakuna anae miliki gari ya thamanani, hakuna aliyejenga nyumba ya kifahari, hakunaโ€ฆhakunaโ€ฆ.

Kwanini "NIA" yako uilinganishe na kushindwa kwa hao wengine kwenu? Wewe ni mmoja wa tofauti, na ukiamua kujitenga kifikra mbali nao, na kufanya mambo makubwa kwa bidii bila kuzimia moyo, hakika utakua wewe kama wewe kuitwa MABADILIKO ya mafanikio katika hao wengi walioshindwa.

"NIA YAKO ISISHINDWE"

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Ujumbe wa leo kwa mtu anayetaka kufanikiwa katika maisha kiuchumi

Ujumbe wa leo kwa mtu anayetaka kufanikiwa katika maisha kiuchumi

Kila mtu aliyefanikiwa ukifuatilia historia yake pengine unaweza kukata tamaa kabisa Na kusema mi... Read More

Salamu za kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya

Salamu za kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya

KWAHERI MWAKA JANA. UMENIFUNZA MENGI.

Mwaka umefika mwisho, zimebaki siku tatu tu
kuin... Read More

Mambo 13 katika pesa ambayo unapaswa kuzingatia

Mambo 13 katika pesa ambayo unapaswa kuzingatia

1. Usikope pesa ya riba ili uanzishe biashara.
Usitegemee pesa ya mkopo kuianzishia biashara... Read More

UJASIRIAMALI NA CHANZO CHA MTAJI

UJASIRIAMALI NA CHANZO CHA MTAJI

UJASIRIAMALI