Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI

Featured Image

โœ๐ŸฝUkichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.

๐Ÿ‘‰๐ŸพKatika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la sabaโ€ au wale ambao hawakuingia darasani kabisa

๐Ÿ™‡๐Ÿฝ๐Ÿ“š Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi ๐Ÿก na ๐Ÿš— ๐Ÿš™magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!)

๐Ÿ‘‰๐ŸพWapo ๐Ÿ™‡๐Ÿฝ๐Ÿ“šwasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana

๐Ÿ‘‰๐ŸพLakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga

Hii inachangiwa na mambo mawili:-
๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ
I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli

๐Ÿ‘‰๐ŸพHata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio

๐Ÿ‘‰๐ŸพKadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

๐Ÿ™‡๐Ÿฝ๐Ÿ“šWasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika
๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

๐Ÿ‘‰๐ŸพKatika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.

โœ‹๐ŸพHuwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

๐Ÿค”Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani

๐Ÿ›ฃMtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti

๐Ÿ˜ŽUkitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze

๐Ÿ˜€๐Ÿ™๐Ÿฝ Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

JITAMBUE: Kipi hauna kati ya pesa na muda?

JITAMBUE: Kipi hauna kati ya pesa na muda?

Soma kidogo hapa.. Kuna watu wa aina NNE tunapoongelea pesa na muda.

1. WANA MUD... Read More

Hofu inavyo tugharimu katika safari ya ujasiriamali na Jinsi ya kuiepuka

Hofu inavyo tugharimu katika safari ya ujasiriamali na Jinsi ya kuiepuka

Wengi wetu tunapenda Mafanikio, tunapenda kufika mbali tunapeda kuwa kama Mengi siku moja.

... Read More

JITAMBUE : Maisha yako ya kesho hayalingani na maisha yako ya jana, Anza sasa

JITAMBUE : Maisha yako ya kesho hayalingani na maisha yako ya jana, Anza sasa

THERE IS NO FUTURE IN THE PAST.** Ukitaka kufanikiwa usiangalie nyuma yako kunanini na ulishindwa... Read More

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha boss na mwajiri wake

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha boss na mwajiri wake

BARUA YA BOSI ILIBADILI FIKRA ZANGU KUHUSU PESA KATIKA DAKIKA ZA MWISHO ZA MAISHA YANG... Read More

Kwa ushauri huu jitambue upate mafanikio

Kwa ushauri huu jitambue upate mafanikio

Ukiona unalala masaa 9 wakati Donald Trump analala manne tu. Afu unaamka huna nauli na bado kesho... Read More

Wazo mbadala kuhusu ajira au kupata kazi

Wazo mbadala kuhusu ajira au kupata kazi

Katika mambo ambayo nadhani nimeshawahi kujidanganya ni kufikiri kwamba nikipata kazi ndiyo utaku... Read More

Kanuni ya fedha ya matumizi na mipango ambayo itakusaidia ukiifuata

Kanuni ya fedha ya matumizi na mipango ambayo itakusaidia ukiifuata

Jifunze kanuni za fedha
kama ilivyoainishwa hapo chini.
Fedha inataki... Read More

Ilinde ndoto yako

Ilinde ndoto yako

Watu wengi wanajiuliza, โ€œSiri ya utajiri ni nini?โ€ Je ni mbinu gani zin... Read More

Jielewe, kipato chako kinakusaidia nini?

Jielewe, kipato chako kinakusaidia nini?

ASSET AND LIABILITY
Asset ni kitu... Read More

UJASIRIAMALI NA CHANZO CHA MTAJI

UJASIRIAMALI NA CHANZO CHA MTAJI

UJASIRIAMALI