Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Kilichotokea baada ya babu mzee kuibiwa nauli kwenye daladala
Updated at: 2024-05-25 16:54:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mzee mmoja alipanda Gari Stend; Wakati wa kugombania Siti, Akaibiwa Nauli.
Akasimama katikati ya Gari-Akasema; "Jamani Naomba Aliyeniibia Pesa yangu Arudishe Haraka, Tena Fasta kabla Sijafanya Tukio kama Nililofanya 1977" Abiria kuskia hivyo wakaogopa. Ikabidi Mwizi Ajitokeze, Akarudisha Pesa na Kuomba Msamaha! Mtu Mmoja akauliza, Mzee, Kwani 1977 Ulifanya nn? Si nilienda kwa Miguu mpaka Nyumbani! Uscheke Peke Yako, wa2mie na wengine ili nao wacheke!
Updated at: 2023-04-29 22:53:40 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..
Kwa wanywaji wazuri wa bia,
chupa ya kwanza 🍺 huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo… Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.
chupa ya pili 🍺🍺 kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi….
Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.
Bia ya tatu 🍺🍺🍺 huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana…. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza…..
Bia ya nne 🍺🍺🍺🍺 huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia….. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.
Bia ya tano 🍺🍺🍺🍺🍺 ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu……na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali’
Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.
Kuanzia bia ya sita 🍺🍺🍺🍺🍺🍺 na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. ……. …Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.
Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika…….
Kilichotokea kati ya mkaka na mdada walipokutana hotelini
Mkaka aliingia kwenye hoteli moja akaketi meza moja na mdada mrembo maarufu sana; MKAKA: Samahani dada sijui saa ngapi? MDADA: Nani kakwambia saa yangu ndio ya kuangalia kila mtu?
Updated at: 2024-05-25 18:08:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mkaka aliingia kwenye hoteli moja akaketi meza moja na mdada mrembo maarufu sana; MKAKA: Samahani dada sijui saa ngapi? MDADA: Nani kakwambia saa yangu ndio ya kuangalia kila mtu?
MKAKA: Samahani sana….jamaa akachukua Galaxy yake akapiga simu….aise saa ngapi saa hizi? mi ndio nimeingia toka USA nataka kurekibisha saa yangu ifwate muda wa huku. Na wewe uwahi kuchukua iPad nimekuja nazo tatu tu za zawadi. Halafu ntafutie mtoto mzuri nimumwagie midola niliyokuja nayo, ok ciao tuonane badae. MDADA: Kaka samahani saa hizi ni saa….. MKAKA: Achana na mimi wewe