Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

MADHARA YA SHISHA

Featured Image
Yafuatayo ni madhara ya shisha; 1.Kansa Licha ya kupita ndani ya maji, moshi wa shisha huwa na kiwango kikubwa cha carbon monoxide na nicotine ambazo humfanya mtumiaji awe kwenye hatari kubwa ya Kupata Tatizo la kansa ya koo, ama mapafu. 2.Matatizo ya Moyo Moshi na tumbaku husababisha mishipa ya damu ya artery Kuziba, Matokeo yakemoyo hushindwa kufanya kazi kwa ufanisi wake. 3.Huharibu Fizi (periodontal disease) Hii hutokana na kuongezeka kwa kiasi cha sumu ya nicotine kwenye damu na fizi matokeo yake ni kuharibika kwa fizi na kupata matatizo ya meno. 4. Fangasi na Kifua kikuu (TB) Kutokana na kutosafishwa vizuri kwa bomba za kuvutia shisha (hasa kutokana na wengi kujali kipato kuliko afya za watu) Mtumiaji hujiweka kwenye hatari kubwa ya Kupata magonjwa ya kuambukizwa kama fangasi, au hata vidonda vya tumbo kwa kuvuta kimelea cha helicobacteria. 5.Kuzaa Njiti (mtoto mwenye uzito mdogo) Hii ni kwa wanawake wanaotumia shisha wakiwa wajawazito. Pia mtoto huyo ni rahisi kuwa na magonjwa yanayohusiana na upumuaji. 6. โ€œNicotine Addictionโ€ Hii ni hali ya kuwa mtumwa wa Sumu ya Nicotine. Mtumiaji wa shisha huvuta kiwango sawa cha nicotine kama mvutaji wa sigara hii husababisha sumu hii hatari kuingia kwenye damu yake, matokeo yake hataweza kuishi bila kutumia shisha au sigara. 7.Kupoteza Uwezo za Kujamiiana. Utafiti unaonesha kuwa, wanawake wanaotumia shisha hupoteza hamu ya kujamiiana kwa kiasi kikubwa. Hali ni mbaya zaidi kwa wanaume kwani huchangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa nguvu za kiume. 8.Kuchakaa kwa ngozi. Kama ilivyo kwa watumiaji wa sigara, matumizi ya shisha huchangia kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa ngozi. Mtumiaji wa muda mrefu wa shisha huzeeka haraka zaidi ya asiyetumia. 9.Asthma na Allergy Zingine Uvutaji wa shisha huharibu utando laini uliopo kwenye njia za pua na koo, uharibifu huu unaweza kusababisha matatizo ya allergy, na asthma. 10.Kwa kuwa Haina Ladha kama ya sigara, watu wengi (hasa vijana) huona shisha ni mbadala mzuri wa sigara, bangi, na madawa mengine ya kulevya wakihisi haina madhara kumbe wanajiangamiza wenyewe!
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Faida za kiafya za Kula Matunda

Faida za kiafya za Kula Matunda

Matunda yote yana faida mwilini kiafya lakini matunda yanatofautiana kifaida. Zifuatazo ni faida ... Read More

Aina ya vyakula vinavyotakiwa kwa wajawazito

Aina ya vyakula vinavyotakiwa kwa wajawazito

Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na ... Read More

Tiba kwa kutumia maji

Tiba kwa kutumia maji

โญ•Tiba kwa kutumia majiโญ•
๐Ÿ’ง๐Ÿ’ง๐Ÿ’ง๐Ÿ’ง๐Ÿ’ง๐Ÿ’ง๐Ÿ’ง๐Ÿ’ง๐Ÿ’ง

Hamuwezi kuamini! mar... Read More

Vitu ambavyo mama mjamzito hapaswi kutumia

Vitu ambavyo mama mjamzito hapaswi kutumia

Vipo vitu mbalimbali ambavyo mama mjamzito hapaswi kuvitumia wakati wa ujauzito kwani vina athari... Read More

Umuhimu wa kupata chanjo

Umuhimu wa kupata chanjo

Siku zote sisi wanadamu huwa tunaambizana kuwa, kinga ni bora kuliko tiba, tukiwa na maana kwamba... Read More

Matumizi ya Mrehani (basil) kutibu presha ya kushuka

Matumizi ya Mrehani (basil) kutibu presha ya kushuka

Hii ni dawa nzuri ya kutibu shinikizo la chini la damu sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamin... Read More

Chanzo na Matibabu ya Tatizo la Mtindio wa Ubongo (Kupooza ubongo)

Chanzo na Matibabu ya Tatizo la Mtindio wa Ubongo (Kupooza ubongo)

Tatizo la Mtindio wa Ubongo au Kupooza ubongo kitaalamu ni Cerebral plasy (CP), ni hali ya kupooz... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia Mtindi na asali

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia Mtindi na asali

Kutumia mtindi na asali ni moja ya dawa rahisi zaidi za kutibu chunusi.

Unahitaji:

... Read More

Faida 10 za kula tende kiafya

Faida 10 za kula tende kiafya

Kila wakati unashauriwa na watalam wa afya ya kwamba unatakiwa kula tende kwa wingi ili kupata fa... Read More

Matumizi ya karoti na asali kutibu presha ya kushuka

Matumizi ya karoti na asali kutibu presha ya kushuka

Hatua za kufuata

1. Tengeneza glasi moja ya juisi ya karoti

2. ... Read More

Mchanganyiko wa asali na mdalasini una faida hizi

Mchanganyiko wa asali na mdalasini una faida hizi

Mchanganyiko wa mdalasini na asali unasaidia katika mambo ya aiana tofauti tofauti kama ifutavto:... Read More

Mbinu 11 za kufuata ili uweze kuacha pombe

Mbinu 11 za kufuata ili uweze kuacha pombe

Pombe ni kinywaji kinachotumiwa na watu wengi pasipo hata kufahamu athari zake. Pombe ina athari ... Read More

๐Ÿ“– Explore More Articles
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About